Askari auawa kwa kisu na mtangazaji wa redio

Askari auawa kwa kisu na mtangazaji wa redio

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,024
Reaction score
59,684
Polisi.jpg

​

Babati
Askari polisi wa mjini Babati, Mkoa wa Manyara ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtangazaji mmoja wa redio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.Baadhi ya wakazi wa Babati walisema jana kuwa wanaume hao walikuwa wakimgombea mwanafunzi wa kidato cha pili walipokuwa baa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime alimtaja aliyeuawa kuwa ni Rashid Haruna (30) mwenyeji wa Mkoa wa Njombe.Kamanda Fuime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 usiku eneo la Kitalu X.

Alisema polisi wanamshikilia mwanafunzi huyo wakati uchunguzi zaidi kuhusu mauaji hayo ukiendelea.Kamanda Fuime alisema baada ya mtangazaji huyo kumchoma kisu askari huyo alikimbilia sehemu za Dareda.

"Kabla ya kifo chake alichomwa kisu mara 15 sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo mikononi, mgongoni, ubavuni na eneo la moyo," alisema Kamanda Fuime.Kamanda Fuime alisema mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Makete Mkoa wa Njombe kwa maziko.

Awali askari ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema siku ya tukio polisi huyo alimkuta msichana baa akiwa analumbana na mtangazaji. Alisema msichana huyo alimuomba askari ambaye ni mpenzi wake amsaidie kwani anang'ang'aniwa na mtu asiyempenda.

Chanzo: Mwananchi
 
Nilifikiri papuchi za gulioni tu ndiyo watu wanauana kumbe hata huko
 
Walikuwa wanagombea mwanamke?
kifo cha aibu sana poleni wafiwa wote.
 
Kwa hiyo Huyo mtangazaji tayari ana uhakika wa miaka thelathini kabla ya kesi ya mauaji
 
Mtangazaji shujaa sio???Pumbaaavu ww bia ya bavaria.
 
Hii hasara nyingine kwa taifa, yaani mtoto wa kidato cha pili anashinda baa, tena saa tano usiku!!!!! Kweli wazazi wameisha kama hali iko hivyo.
 
Wote hamshangai huyo muuaji hajatajwa jina!
Au mi ndo sijaliona?
 
Back
Top Bottom