Askari 12,000 wakwama kulipwa mshahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari 12,000 wakwama kulipwa mshahara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbori, Oct 13, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  HALI siyo shwari ndani ya Jeshi la Polisi nchini baada ya askari wake zaidi ya
  12,194 kukosa mishahara kutokana na
  mabadiliko ya mfumo wa malipo
  kwenye mtandao wa kompyuta, uliobadilishwa na Wizara ya Fedha.
  Mpaka sasa, jumla ya askari 27,398
  wamekwishalipwa kupitia benki baada ya kuwasilisha akaunti zao Benki ya NMB, lakini askari waliosalia ambao ni
  zaidi ya 12,194 bado hawajapata mishahara yao kutokana na ofisi za uhasibu ndani ya Jeshi la Polisi
  kushindwa kuandaa malipo.

  Habari zilizopatikana kutoka ndani ya
  Jeshi la Polisi na kuthibitishwa na baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa pamoja na Msemaji wa jeshi hilo, Adivera Senso, zinaeleza kwamba
  mishahara ya askari hao ilipaswa kuwa
  imelipwa tangu Septemba 23 mwaka huu, lakini hadi leo askari hao
  hawajalipwa. Mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo
  alilidokeza Mwananchi kuwa tatizo hilo
  linatokana na Wizara ya Fedha kuipa zabuni kampuni moja kubadilisha mfumo huo wa malipo ambao pia uliwahusu
  wahasibu wote nchini. Alisema chini ya mfumo huo mpya wa
  Epicor-9 wahasibu wote waliopo ndani
  ya wizara hiyo walitakiwa kubadilisha
  utaratibu wa utoaji hundi na ulipaji na
  watumishi wote na kwamba mishahara
  yao lazima ianze kupitia Benki ya NMB. “Tatizo lilitokea baada ya Wizara ya
  Fedha kutoa mwongozo juu ya mfumo wa programu mpya ya kompyuta ya
  Epicory-9 ya uhasibu kubadilika kutoka
  programu ya zamani ya Epicor-7.
  Katika mabadiliko haya askari waliarifiwa kutumia Benki ya NMB, hivyo askari
  ambao walikuwa hawajafungua akaunti
  zao waliendelea kupokea malipo yao kwa wahasibu, lakini nao sasa
  mishahara imekwama,” alieleza
  mfanyakazi huyo.

  Mkoa wa Mwanza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,
  Liberatus Barlow alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na kwamba sehemu kubwa ya askari ambao hawajalipwa mishahara yao imetokana na wao kuchelewa
  kuwasilisha akaunti zao za benki. “Tunalo hilo tatizo, ni kubwa lakini
  makao makuu wametuhakikishia kwamba wanalifanyia kazi. Ila limetokana na baadhi ya askari wetu kushindwa kutekeleza maagizo haraka,
  utaona hawa ambao hawajapokea mishahara ni sehemu ya askari
  wachache, lakini wale wenzao ambao
  walikamilisha utaratibu wa kufungua
  akaunti benki wamepokea mishahara
  yao,” alifafanua Kamanda Barlow.

  Mkoani Tabora Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa
  Polisi Mkoa wa Tabora, Edward Bukombe
  alisema hajapata malalamiko kutoka kwa askari ambao hawajalipwa kwa
  kuwa asilimia kubwa ya askari wake walishakamilisha utaratibu wa kulipiwa mishahara yao kupitia benki.
  Alisema hata kama tatizo hilo
  litakuwapo, basi athari yake itakuwa siyo kubwa ikilinganishwa na mikoa mingine ambako kuna idadi kubwa ya
  askari ambao hawajalipwa mishahara.

  Mkuu wa Ofisi ya Wizara ya Fedha
  mkoani Mwanza, Godfrey Kiabula
  alisema mkoa wake ulikuwa katika harakati za kuhakikisha malipo yanafanyika haraka na kwamba askari
  hao wataanza kulipwa leo. “Mie niko nje ya ofisi, lakini
  ninachofahamu ni kuwa utaratibu
  ulikuwa ukifanyika kuhakikisha
  wanalipa askari hao, nadhani watalipwa
  kuanzia kesho (leo),” alieleza ofisa huyo
  kwa simu.

  Mkoa wa Dar es Salaam Jijini Dar es Salaam pia inaelezwa kuwa
  hali siyo shwari baada ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Ukonga
  kuwabana maofisa wa wizara hiyo juzi
  kuhusu malipo ya mishahara yao hali ambayo ilimlazimu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP)
  Said Mwema kuwaamuru wahasibu wa
  jeshi hilo kwenda Wizara ya Fedha
  kutafuta ufumbuzi wa askari hao
  waweze kulipwa.
  “Ninakwambia hapa kwetu hali ilikuwa mbaya, jana FFU walifanya vurugu
  tukalazimika kukimbia ofisi, na baada ya
  hali kutulia, IGP aliagiza twende Wizara
  ya Fedha kushughulikia mishahara ili
  askari walipwe,” alieleza mmoja wa maofisa wa polisi kutoka Idara ya Uhasibu.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijha
  alipoulizwa kwa njia ya simu alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala lolote kwa vile alikuwa katika kikao na
  kuomba kuwasiliana naye siku nyingine. “Kwa sasa niko kwenye kikao nipe nafasi kwanza, nitalifuatilia suala hili
  kujua ukubwa wa tatizo lenyewe.
  Siwezi kuzungumza lolote hapa nilipo,
  naomba tuwasiliane kesho," alisema na kukata simu.

  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso alisema taarifa za askari wa FFU
  kufanya vurugu ni za upotoshaji na
  kwamba hana taarifa za IGP kutoa
  maagizo kwa wahasibu kwenda Wizara
  ya Fedha. “Nilikuwa kwenye vikao tangu asubuhi,
  sasa jambo hili siwezi kulieleza kwa
  sasa mpaka kuwasiliana na mikoani
  kujua ni askari wangapi ambao mpaka
  sasa hawajalipwa,” alisema.
  Chanzo: Mwananchi, October 13.
   
 2. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Wakija madukani na magengeni msiwakopeshe wauaji hao wakiwa na bunduki na vitu vizito wanajisahau kuwa wao ni binadamu kama wengine utasikia ua huyo pigaa.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,504
  Likes Received: 19,918
  Trophy Points: 280
  mambo ya kina dr Ndalichako na baraza la mitihani na islamic knowledge
   
 4. M

  Manyiri Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 27, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Serikali dhaifu jeshi dhaifu unategemea nini? eti hao ndo wanaotegemewa kulinda mali zetu wakati wao wana njaa hawajalipwa mishahara.Nasikia nawao ili fedha iingie benki lazima watoe rushwa kwa wahasibu wa makao makuu ya polisi DAR KAZI IPO NCHI HII.
   
 5. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,858
  Likes Received: 4,242
  Trophy Points: 280
  Wazee wa kutumiwa km ped, wanakumbukwa siku kukiwa na mikutano ya CDM! inabidi wajitafakari.
   
Loading...