Asiyesikia la mkuu....!

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
8,315
7,730
Jamaa fulani alikuwa na tabia ya kuj…ba kwa nguvu kila aamkapo asubuhi. Mkewe alikerwa sana na tabia hiyo, alimkataza akachoka, siku moja akamwonya kuwa iko siku badala ya pumzi, utumbo utakuja kumtoka. Jamaa alicheka sana kusikia hilo. Siku moja mke alilazimika kuamka alfajiri awatengeze kuku kwa ajili ya sherehe, alipowatoa utumbo wale kuku akakumbuka alichowahi kumwambia mumewe akaamua kumtisha, akamnyatia mumewe ambaye alikuwa bado amelala na kumuwekea utumbo kwenye pajama lake na kurudi jikoni. Muda si mrefu mwanaume aliamka na kufanya mambo yake kama kawaida, lakini akahisi kitu cha baridi ndani ya suruali, ile kuvuta si akakuta utumbo. Akapiga ukelele,’Mama yangu nimekufa’. Mke wake aliposikia akacheka peke yake. Kimya cha kama nusu saa kilipita. Hatimaye jamaa akamfuata mkewe jikoni akiwa amelowa jasho pajama nzima.
JAMAA: Mke wangu yale uliosema leo yametokea.
MKE: Yepi jamani?
JAMAA: Mke wangu utumbo si umetoka kama ulivyosema
MKE: Pole mume wangu, sasa?
JAMAA: Namshukuru Mungu, nimejitahidi nimeweza kuurudisha ndani wote.
MKE: Mungu wangu umefanyaje?
 
cjakuelewa ulivyosema kuji...ba maanake ni nini?
 
hahahaaaa huyo aliepoteza mbavu mwambie azitafute halafu azirudishe kama mwenzie...!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom