Mh! Sikio la kufa halisikii dawa ni baada ya Miss Tanzanian2006, Wema Abraham Sepetu kuendeleza sakata la vihoja visivyokuwa na kichwa wala miguu na kuweza kufunguliwa mashitaka mengine tena yatokana na wizi.
Kwani Mrembo huyo aliweza tena kurudishwa na kufunguliwa tena mashitaka mengine, na kuswekwa tena rumande kwenye kituo cha Polisi cha Kijitonyama kilichopo hapa jijiji.
Si pekeyake bali akiwa na mpenzi wake Jumbe, wamefunguliwa mashitaka ya wizi a televisheni, redio ikiwemo na microwave.
Wema pamoja na Jumbe wamefunguliwa jalada namba KJN/RB/1977/09 linalohusiana na wizi huo, na kubainisha kuwa mrembo huyo alibeba vitu hivyo kutoka kwao na kupotea navyo kwa mpenzi wake huyo ambako alijichimbia kwa siku kadhaa.
Mbali na kuibka na vioja vingine bado kesi yake ya kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa mpenzi wake, mwigizaji maarufu, Steven Kanumba inaendelea katika Mahakama ya Kinondoni.
Kwani mama mzazi wa mrembo huyo akiwemo na dada yake walionekana ndani ya kituo cha Kijitonyama, kuhusiana na suala hilo.
Na imeelezwa walikuwa wanataka waelezwe vilipo vitu hivyo ili wawatoe nje kwa dhamana.
Siku chache za usoni hali ya Wema ilionekana kubadilika baada ya mama yake kumtafutia kazi, lakini siku chache zilizopita tabia yake ilibadilika tena na kuanza kurejea usiku nyumbani katika eneo la Sinza jirani na Lion Hotel ambako ni nyumbani kwa dada yake anakoishi baada ya kuibuka kwa tafrani mahakamani siku alipowekewa dhamana mwezi uliopita.
Jumbe amekuwa akituhumiwa kumfundisha mrembo huyo kutumia dawa za kulevya, na alishindwa hata kumwekea dhamana alipolazimika kulala mahabusu.
Imeelezwa alipotea kwa dada yake eneo la Sinza kwa zaidi ya siku mbili na walikuwa hawajui aliko na baadaye ilielezwa alirejea tena kwa Jumbe ambaye ndugu zake wanamtuhumu kuwa 'amemchezea mrembo huyo ambaye anaonekana kutosikia .