Asitisha mawasiliano baada ya kumkatalia kumpa dressing table

Asitisha mawasiliano baada ya kumkatalia kumpa dressing table

wanatamani

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
415
Reaction score
145
Habari wana jamvi.

Mimi ni kijana nina mahusiano na msichana mmoja yapatayo mwaka sasa. Lakini ghafla amesitisha mawasiliano baada ya kunitumia meseji akiniomba nimpatie dressing table yangu ambayo ipo ndani kwangu naitumia, nilimweleza siwezi kutoa kitu ndani ambacho nimenunua kwa ajili ya ndani kwangu kumpatia yeye.

Labda asubiri nimtafutie pesa akanunue yake, hapo ndio chanzo cha kustisha mawasiliano na mimi. Naomba maoni yenu hii ndio itakuwa sababu au ilikuwa ni kutafuta sababu na ameipatia hapo na je ni sahihi kutoa kitu cha ndani ya nyumba kama kabati, dressing au kitanda kumpatia girlfriend apeleke kwake.

Ushauri please
 
Kesho atataka kitanda

Kesho kutwa atataka viti

Mtondogoo atataka achukue kabati la vyombo
 
Kama kaipenda ahamie mtumie wote.mkuu hujui siasa kwenye mapenzi? there is a soft way of saying no! sasa we umemjibu "siwezi kukupa" thats harsh! ungemwambia "'mamy hii haikufai,mambo yakikaa sawa ntakununulia nzuri zaidi kuna mahali niliiona"
afu asuburi mpaka Yesu aje nayo!
 
Huyo umemuokota wapi? mtu gani aelewi kusubiria.?
 
Huyo mwanamke atakua kutoka vijijini na bado haja polish,ivi unamwambie mwanamme unataka dressing table yake?
kwani Mkuu bado unamzimia michezo yake au ni basi tuu, nisije kwambia achana nae kumbe bado mitindo ya Kanga moko inakuzingua...
 
Kuna watu watata sana aiseeee ngekuwa mimi namwambia nenda weee safar njema khaaaa au alikuwa anatafuta sababu ya kukata mawasiliano na sio dressing table.
 
Kamnunulie wanja wa kwendea kwenye vigodoro
 
Dressing table kitu gani si umpe tu! We mwanaume kwenye dressing table unaweka nini? Deodorant,cologne,lotion vinatosha hata kikabati cha bafuni!
 
Safari moja huanzisha nyingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom