Asitafutwe mchawi

Hapa abiria wanakuwa kimya na kila mtu yupo busy na simu yake, gazeti au kuangalia video
Ila yakitokea haya tunasema ni mipango ya Mungu
Tukemee vitendo vyote vinavyohatarisha maisha yetu
 
Safi sana mkuu, hivyo ni vitu muhimu kuvitambua
Kiongozi mimi nilipitia VETA kwenda kubadilisha Leseni Daraja C ukweli kati wanafunzi 100 wote madereva wakubadilisha Leseni tuliulizwa swali la ALAMA za barabara to be Frank the entire class we got it wrong!
 
Kiongozi mimi nilipitia VETA kwenda kubadilisha Leseni Daraja C ukweli kati wanafunzi 100 wote madereva wakubadilisha Leseni tuliulizwa swali la ALAMA za barabara to be Frank the entire class we got it wrong!
Kwa maana hii lazima tutafute mchawi, yawezekana ni Mulugo.
 
Hii hatari sasa? Kama wana haraka si wangekwenda tangu jana yake?
 
Kipanya ameshawasha indiketa ya kushoto anawahi kulala kushoto kabla ya kukutana uso kwa uso na wanaokuja.

Ndio maana Ajali zetu mara nyingi ni za uso kwa uso.

Halafu mwangalie Konda wa Kipanya alivyotoa kichwa chake nje
 
Mistari hiyo, hairuhusiwi kumpita mwenzako, cha ajabu Basi ndio kwanza hana wasi na amepakia Abiria hapo.

Pili Kibao kinaonesha njia haijanyooka, umeshatahadharishwa, na mara nyingi ukishaona alama hiyo mwendo inatakiwa kasi ya 80 cha ajabu unaweza kuta Basi hapo yuko 140.

Hatuzingatii sheria za Barabarani ndio maana Ajali haziishi, hazipungui.



 
MKUU HARUFU
Sasa hivi kuna nafuu sana barabarani hasa kwa Mabasi ya kwenda mikoani wamebaki wakorofi wachache sana hili nimelishuhudia mwenyewe nilienda Singida mwezi uliopita mwendo ulikuwa wa spidi isiyozidi 80!
Nilikuwa nikiangalia spidi kwenye smartphone yangu.
 
Afadhali.

Kiongozi nashukuru sana kwa kunifahamisha kinachoendelea hivi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…