Asilimia Kubwa ya Ulichowahi Kusikia Kuhusu Nyoka ni Uongo na Hadithi za Kutunga Tu!

Katika ulimwengu wa sasa ni rahisi sana kupata taarifa mbalimbali kuhusu viumbe hai. Lakini ni ajabu sana kwamba asilimia kubwa ya taarifa hizo ni uongo na masimulizi ya kutunga tu! Hii ni mojawapo tu ya sababu kwanini watu wanahitaji kuelimishwa kuhusu viumbe hai na mazingira yao.
Miongoni mwa taarifa ambazo zimekuwa za uongo na kupotosha sana ni kuhusu maisha ya nyoka. Katika makala hii ndogo tutaangalia kwa ufupi maisha ya nyoka na uhusiano wao na mazingira kwa njia ya maswali na majibu.

1. SWALI; Je, nitumie dawa gani kuzuia nyoka wasikaribie nyumbani kwangu?
JIBU; Hakuna dawa yoyote ambayo ni mahususi kwa kuwazuia nyoka kukaribia nyumbani kwako. Inawezekana kuna watu wanajitangaza kuwa wanauza dawa za kufukuza nyoka lakini uhalisia ni kwamba, asilimia kubwa ya dawa hizo ni za uongo na madhara yake kwenye mazingira ni makubwa zaidi ya unavyoweza dhania.
Namna sahihi na rahisi ya kuwazuia nyoka kukaribia nyumba yako ni kuziba njia zote wanazoweza tumia kukaribia na kuingia ndani ya nyumba yako. Unaweza kufanya hivi kwa kujenga ukuta kuzunguka nyumba yote na kuziba nyufa za aina yoyote kwenye msingi. Vilevile unaweza kuziba nafasi za wazi pembeni au chini ya milango ambazo nyoka wanaweza jipenyeza na kuingia ndani ya nyumba yako.
Kumbuka kuwa nyoka wengi huingia kwenye nyumba za watu kutafuta chakula, hasahasa panya. Hivyo basi, kama nyumbani kwako kuna panya jiandae kukutana na nyoka siku moja!

2. SWALI; Je, nyoka wote wana sumu?
JIBU; Hapana, siyo nyoka wote wana sumu. Ni wastani wa nyoka mmoja kati ya nyoka watano ama chini ya 20% ya nyoka wote waliopo duniani ndiyo wanaweza kuwa na sumu. Kwa uhakika zaidi, nyoka wenye sumu hujumuisha swila na aina zake, vifutu na aina zake pamoja na baadhi tu ya nyoka wa miti. Asilimia kubwa ya nyoka tunaokutana nao huwa hawana sumu! Kumbuka kuwa, nyoka wote wenye sumu pamoja na wasiokuwa na sumu wanafaida kubwa sana kimazingira zaidi ya unavyoweza fikiria! Hivyo basi unapaswa kuwaheshimu.

3. SWALI; Je, nyama ya nyoka na mifupa yake inasumu na inaweza kunidhuru endapo nitaila au mifupa kunichoma?
JIBU; Ndiyo, ni kweli kuna baadhi ya nyoka wameamua kujihami kwa mtindo huo endapo ikitokea wakauliwa na kuliwa na wanyama wengine. Sumu iliyopo miilini mwa nyoka hao inaweza kumdhuru mnyama huyo. Kama unapenda kula nyoka itabidi ulizingatie hili!

4. SWALI; Je, nyoka wenye sumu wanaweza kuzaliana na nyoka wasio na sumu na kutoa watoto chotara?
JIBU; Hapana, haiwezekani.

5. SWALI; Je, nyoka wanaweza uma wakiwa wamezama ndani ya maji?
JIBU; Ndiyo, nyoka wote hata wale wenye sumu wanaweza kuuma wakiwa wamezama ndani ya maji.

6. SWALI; Je, nyoka hupenda kufukuza binadamu?
JIBU; Hapana! Nyoka wengi hupenda kufukuza viumbe wale tu ambao ni chakula chao hasa hasa wenye umbo dogo ambao wanaweza wakawameza kwa urahisi (Kumbuka baadhi ya nyoka kama chatu na anakonda wakubwa sana wanaweza kummeza binadamu lakini hawamfukuzi bali wanamnyemelea pasipo yeye kujua na kumvamia ghafla tu. Kwa kizungu inaitwa "Ambush"). Nyoka wengi huchagua kukimbia endapo binadamu atawakaribia kwani humuona kama ni hatari kwao. Ikitokea nyoka akakimbia kuelekea upande wako, mara nyingi ni kwa sababu ameona kuwa upande huo ndiyo kuna usalama zaidi (Ukiwa umeziba njia kati yake na mahali penye usalama).
Endapo nyoka akihisi kutishiwa maisha yake, hapo ndipo ataamua kujihami kwa kukuuma/kukung'ata kama vile tu kiumbe chochote kinavyoweza kujihami. Wakati mwingine nyoka anaweza kuuma kutokana na mshtuko kama akikanyagwa au akisogelewa kwa ghafla sana. Hivyo basi kwa sababu hii ni muhimu kuwa makini kwa kuangalia mahali unaposhika au unapokanyaga hasahasa gizani.

7. SWALI; Je, nikiona mtoto wa nyoka inamaanisha kuwa mama yake pia atakuwa maeneo jirani na hapo?
JIBU; Inawezekana ila kwa kiwango kidogo sana! Nyoka wengi hutafa mayai na kuyaacha yajiangua yenyewe (Isipokuwa chatu ambaye huatamia mayai yake na baadhi ya nyoka ambao huzaa badala ya kutaga). Watoto wa nyoka wanapojitotoa huanza maisha yao binafsi bila ya uangalizi wa mama zao.

8. SWALI; Je, nikimuona nyoka na kumtambua kuwa ana sumu ninpaswa kumuua?
JIBU; Hapana!!! Usijaribu kumuua nyoka. Licha ya kuwa nyoka wana faida kubwa katika mazingira, asilimia kubwa ya watu wanaoumwa na nyoka ni wale wanaojaribu kuwauwa. Hivyo basi kitendo cha wewe kujaribu kumuua nyoka ni sawa kabisa na wewe kuhatarisha maisha yako. Kumbuka kuwa kiumbe yoyote yule akitishiwa maisha anaweza fanya vitu ambavyo hukutarajia. Hata binadamu vilevile.
Kitu cha kufanya ukikutana na nyoka na ukamtambua kuwa ni nyoka mwenye sumu ni kumuacha aende zake. Kama yupo karibu na makazi ya watu ni vema ukatoa taarifa kwa wataalamu wa maswala ya nyoka waje kumkamata na kumuondoa eneo hilo.

9. SWALI; Je, niking'atwa na nyoka ninaweza kuinyonya sumu na kuitema chini?
JIBU; Hapana, usijaribu kufanya hivyo kwani ni sawa tu na kusambaza sumu zaidi. Kitu cha kufanya endapo umeumwa na nyoka ni kutafuta kwa haraka(siyo kukimbia) msaada katika kituo cha afya. Usipoteze muda kwa kuanza kujipiga picha na kuweka mtandaoni!

10. SWALI; Je, nyoka wote wenye sumu wana macho kama ya paka?
JIBU; Ndiyo na hapana! Usitumie njia hii pekee kumtambua nyoka mwenye sumu kwani siyo nyoka wote wenye sumu wana macho kama ya paka (au alama ya kisu ya karata).

11. SWALI; Je, nyoka wote wenye sumu wana vichwa vyenye umbo la pembe tatu?
JIBU; Ndiyo na hapana! Kwa mara nyingine usitumie njia hii pekee kumtambua nyoka mwenye sumu kwani siyo nyoka wote wenye sumu wana vichwa vyenye umbo la pembe tatu.

12. SWALI; Je, nyoka wanatumia mkia wao kuchapa au kuchoma watu?
JIBU; Hapana, nyoka wengi hujiami kwa kukimbia, kujificha, kuigiza amekufa na mara chache kuuma. Na vilevile nyoka hawana kucha kwenye mikia kama wengi wanavyoamini.

### JE, UNAPENDA KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSI NYOKA NA VIUMBE HAI WENGINE?
Kama una swali uliza na kama kuna vitu unavielewa kuhusu nyoka usisite kuchangia kwa manufaa ya wengi!

View attachment 1236148
Swali langu linatoka No. 9
Tumekua tukiambiwa pale unapong'atwa na Nyoka ni Vizuri kufunga Kamba sehemu ya juu kidogo toka sehemu uliyong'atwa, Je! Ni sahihi?
 
Ni kweli hata kwenye mashamba ya bangi na tumbaku wanapenda sana
Kaka inawezekena unajua mengi lakini naomba nikuambie hili...NYOKA WANAPENDA MOSHI WA BANGI..Sijui kama watafiti wametafiti hili lakini mimi Binafsi nachoma hasa nikiwa safarini, kuna kipande kipo kati ya Tinde mpaka Isaka huwa nikifika hapo natoa kitu. Kuna nyoka wawili hapo wana rangi flani kama kijiv si kijibu, zaid mara saba nnavyokuambia ninawakuta hapo yaan wakiona raia anakuja wanashuka juu ya mTi kuna miti kama mitatu pale alaf wanajichanganya na majani wanatafuta kule moshi unapoelekea wanatulia wanasikilia kitu, mara zote hizo nimekuwa nikiwapiga picha na vids ninazo pia, na nasema hivi Nyoka wanapenda Moshi wa Bangi, na madereva wanalijua hili, hata ukienda kukata gogo ktk pori usilolijua kama utakuwa na msuba snake hatokudhuru hata kama utajichanganya ktk anga zake
 
13. Swali ? Je Nyoka ndio kiumbe asiopendwa na wanadamu kuliko vyote ?

JIBU NI NDIO nasio na Wanadamu tu, bali na Mungu pia, Kwani nyoka ndio aliyesababisha tukafukuzwa Eden, maisha yamekuwa magumu kwaajili ya Nyoka.
Acha kulisha watu matango pori
 
Mdau ukiumwa na nyoka kama kwa haraka sana kojoa uweke mkojo eneo ulilogongwa na nyoka na mwingine kunywa ili kufuata taratibu za kukufikisha hosp hapo unasemaje
Katika ulimwengu wa sasa ni rahisi sana kupata taarifa mbalimbali kuhusu viumbe hai. Lakini ni ajabu sana kwamba asilimia kubwa ya taarifa hizo ni uongo na masimulizi ya kutunga tu! Hii ni mojawapo tu ya sababu kwanini watu wanahitaji kuelimishwa kuhusu viumbe hai na mazingira yao.
Miongoni mwa taarifa ambazo zimekuwa za uongo na kupotosha sana ni kuhusu maisha ya nyoka. Katika makala hii ndogo tutaangalia kwa ufupi maisha ya nyoka na uhusiano wao na mazingira kwa njia ya maswali na majibu.

1. SWALI; Je, nitumie dawa gani kuzuia nyoka wasikaribie nyumbani kwangu?
JIBU; Hakuna dawa yoyote ambayo ni mahususi kwa kuwazuia nyoka kukaribia nyumbani kwako. Inawezekana kuna watu wanajitangaza kuwa wanauza dawa za kufukuza nyoka lakini uhalisia ni kwamba, asilimia kubwa ya dawa hizo ni za uongo na madhara yake kwenye mazingira ni makubwa zaidi ya unavyoweza dhania.
Namna sahihi na rahisi ya kuwazuia nyoka kukaribia nyumba yako ni kuziba njia zote wanazoweza tumia kukaribia na kuingia ndani ya nyumba yako. Unaweza kufanya hivi kwa kujenga ukuta kuzunguka nyumba yote na kuziba nyufa za aina yoyote kwenye msingi. Vilevile unaweza kuziba nafasi za wazi pembeni au chini ya milango ambazo nyoka wanaweza jipenyeza na kuingia ndani ya nyumba yako.
Kumbuka kuwa nyoka wengi huingia kwenye nyumba za watu kutafuta chakula, hasahasa panya. Hivyo basi, kama nyumbani kwako kuna panya jiandae kukutana na nyoka siku moja!

2. SWALI; Je, nyoka wote wana sumu?
JIBU; Hapana, siyo nyoka wote wana sumu. Ni wastani wa nyoka mmoja kati ya nyoka watano ama chini ya 20% ya nyoka wote waliopo duniani ndiyo wanaweza kuwa na sumu. Kwa uhakika zaidi, nyoka wenye sumu hujumuisha swila na aina zake, vifutu na aina zake pamoja na baadhi tu ya nyoka wa miti. Asilimia kubwa ya nyoka tunaokutana nao huwa hawana sumu! Kumbuka kuwa, nyoka wote wenye sumu pamoja na wasiokuwa na sumu wanafaida kubwa sana kimazingira zaidi ya unavyoweza fikiria! Hivyo basi unapaswa kuwaheshimu.

3. SWALI; Je, nyama ya nyoka na mifupa yake inasumu na inaweza kunidhuru endapo nitaila au mifupa kunichoma?
JIBU; Ndiyo, ni kweli kuna baadhi ya nyoka wameamua kujihami kwa mtindo huo endapo ikitokea wakauliwa na kuliwa na wanyama wengine. Sumu iliyopo miilini mwa nyoka hao inaweza kumdhuru mnyama huyo. Kama unapenda kula nyoka itabidi ulizingatie hili!

4. SWALI; Je, nyoka wenye sumu wanaweza kuzaliana na nyoka wasio na sumu na kutoa watoto chotara?
JIBU; Hapana, haiwezekani.

5. SWALI; Je, nyoka wanaweza uma wakiwa wamezama ndani ya maji?
JIBU; Ndiyo, nyoka wote hata wale wenye sumu wanaweza kuuma wakiwa wamezama ndani ya maji.

6. SWALI; Je, nyoka hupenda kufukuza binadamu?
JIBU; Hapana! Nyoka wengi hupenda kufukuza viumbe wale tu ambao ni chakula chao hasa hasa wenye umbo dogo ambao wanaweza wakawameza kwa urahisi (Kumbuka baadhi ya nyoka kama chatu na anakonda wakubwa sana wanaweza kummeza binadamu lakini hawamfukuzi bali wanamnyemelea pasipo yeye kujua na kumvamia ghafla tu. Kwa kizungu inaitwa "Ambush"). Nyoka wengi huchagua kukimbia endapo binadamu atawakaribia kwani humuona kama ni hatari kwao. Ikitokea nyoka akakimbia kuelekea upande wako, mara nyingi ni kwa sababu ameona kuwa upande huo ndiyo kuna usalama zaidi (Ukiwa umeziba njia kati yake na mahali penye usalama).
Endapo nyoka akihisi kutishiwa maisha yake, hapo ndipo ataamua kujihami kwa kukuuma/kukung'ata kama vile tu kiumbe chochote kinavyoweza kujihami. Wakati mwingine nyoka anaweza kuuma kutokana na mshtuko kama akikanyagwa au akisogelewa kwa ghafla sana. Hivyo basi kwa sababu hii ni muhimu kuwa makini kwa kuangalia mahali unaposhika au unapokanyaga hasahasa gizani.

7. SWALI; Je, nikiona mtoto wa nyoka inamaanisha kuwa mama yake pia atakuwa maeneo jirani na hapo?
JIBU; Inawezekana ila kwa kiwango kidogo sana! Nyoka wengi hutafa mayai na kuyaacha yajiangua yenyewe (Isipokuwa chatu ambaye huatamia mayai yake na baadhi ya nyoka ambao huzaa badala ya kutaga). Watoto wa nyoka wanapojitotoa huanza maisha yao binafsi bila ya uangalizi wa mama zao.

8. SWALI; Je, nikimuona nyoka na kumtambua kuwa ana sumu ninpaswa kumuua?
JIBU; Hapana!!! Usijaribu kumuua nyoka. Licha ya kuwa nyoka wana faida kubwa katika mazingira, asilimia kubwa ya watu wanaoumwa na nyoka ni wale wanaojaribu kuwauwa. Hivyo basi kitendo cha wewe kujaribu kumuua nyoka ni sawa kabisa na wewe kuhatarisha maisha yako. Kumbuka kuwa kiumbe yoyote yule akitishiwa maisha anaweza fanya vitu ambavyo hukutarajia. Hata binadamu vilevile.
Kitu cha kufanya ukikutana na nyoka na ukamtambua kuwa ni nyoka mwenye sumu ni kumuacha aende zake. Kama yupo karibu na makazi ya watu ni vema ukatoa taarifa kwa wataalamu wa maswala ya nyoka waje kumkamata na kumuondoa eneo hilo.

9. SWALI; Je, niking'atwa na nyoka ninaweza kuinyonya sumu na kuitema chini?
JIBU; Hapana, usijaribu kufanya hivyo kwani ni sawa tu na kusambaza sumu zaidi. Kitu cha kufanya endapo umeumwa na nyoka ni kutafuta kwa haraka(siyo kukimbia) msaada katika kituo cha afya. Usipoteze muda kwa kuanza kujipiga picha na kuweka mtandaoni!

10. SWALI; Je, nyoka wote wenye sumu wana macho kama ya paka?
JIBU; Ndiyo na hapana! Usitumie njia hii pekee kumtambua nyoka mwenye sumu kwani siyo nyoka wote wenye sumu wana macho kama ya paka (au alama ya kisu ya karata).

11. SWALI; Je, nyoka wote wenye sumu wana vichwa vyenye umbo la pembe tatu?
JIBU; Ndiyo na hapana! Kwa mara nyingine usitumie njia hii pekee kumtambua nyoka mwenye sumu kwani siyo nyoka wote wenye sumu wana vichwa vyenye umbo la pembe tatu.

12. SWALI; Je, nyoka wanatumia mkia wao kuchapa au kuchoma watu?
JIBU; Hapana, nyoka wengi hujiami kwa kukimbia, kujificha, kuigiza amekufa na mara chache kuuma. Na vilevile nyoka hawana kucha kwenye mikia kama wengi wanavyoamini.

### JE, UNAPENDA KUJIFUNZA ZAIDI KUHUSI NYOKA NA VIUMBE HAI WENGINE?
Kama una swali uliza na kama kuna vitu unavielewa kuhusu nyoka usisite kuchangia kwa manufaa ya wengi!

View attachment 1236148
 
13. Swali ? Je Nyoka ndio kiumbe asiopendwa na wanadamu kuliko vyote ?

JIBU NI NDIO nasio na Wanadamu tu, bali na Mungu pia, Kwani nyoka ndio aliyesababisha tukafukuzwa Eden, maisha yamekuwa magumu kwaajili ya Nyoka.
Sio kwa kusingiziwa huko
 
  • Kicheko
Reactions: vvm
Back
Top Bottom