Asilimia 97 ya wanaume Hawaoi wanawake waliosota nao

Raymanu KE

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
6,819
12,568
Kama mada inavyojieleza hapo juu Ni Kwamba asilimia kubwa ya wanaume kamwe hawawezi kuwaoa wanawake/ wachumba wao waliosota nao kipindi kirefu. Wanaume tunafeli Sana kwenye hili suala.Binafsi sijaoa ila hi ishi huwa naiona kwa wanaume wengi especially rafiki zangu.

Wanaume tuna tabia ya kubadili malengo yetu tulioweka na wachumba zetu( especially suala la ndoa) pale tunapopata unafuu wa maisha.Unakuta jamaa Ana mwanamke wake labda tuseme amepush naye kwa muda wa miaka 5 Hadi wamewekeana ahadi ya kuoana baada ya muda fulani. Hapa jamaa atakuwa Bado anajichanga changa anaishi kwa kuunga unga tu na mwanamke wake anampenda Sana licha ya jamaa kuwa na uchumi mbaya.Mwanamke anakuwa ndiye wa kumtia moyo na kumpa matumaini kwamba ipo siku watatusua tu, pia hampigi mizinga ya ajabu ajabu anashukuru kwa kile kdgo anachopewa na huyu jamaa wake.

Sasa kimbembe kinaanza kuonekana pale jamaa anapoanza kupata unafuu wa maisha. Tuseme amepata mchongo mzuri huko mjini na anapiga hela ndefu. Jamaa anaanza kushoboka na totoz za mjini anamsahau kbsa mwanamke wake aliyekuwa anamtia moyo kila siku.Jamaa anaanza kumdharau kutomsikiliza mixer kumtukana huyu mwanamke wake eti kisa amepata chombo huko mjini
Kimasihara tu jamaa anaamua kumuoa kbsa yule king'asti wake wa mjini na kuja naye vijijini.

Wanaume tunakwamaga wapi lakini? Au tuseme tamaa zetu ndo huwa zinatuponza kwenye hili?

Mbona tusiwaoe wanawake tuliosota nao muda mrefu ila tunaamua kuwapiga chini na kuwakimbilia wanawake wengine.

Tunafeli Sana aisee!
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu Ni Kwamba asilimia kubwa ya wanaume kamwe hawawezi kuwaoa wanawake/ wachumba wao waliosota nao kipindi kirefu.Wanaume tunafeli Sana kwenye hili suala.Binafsi sijaoa ila hi ishi huwa naiona kwa wanaume wengi especially rafiki zangu.
Hiyo ni kawaida ktk maisha, hata wewe jamaa zako uliosota nao ukifanikiwa huwezi kuendelea kuwa nao.Mwanamke km hujamuoa bado huyo ni rafiki tu km rafiki wengine tofauti ni ile kuwa mnapeana tunda,kwa hiyo ukishapata uelekeo mzuri wa maisha lazima utafute manzi mnayeendana nae.
 
Wewe unaweza kuamini mtu aliyekupa mwili wake kabla ya kumuoa, maana yake anaweza kumpa mtu mwingine.

Nafikiri wanawake wangekuwa wanawakazia hao jamaa sidhani kama wangefika huko mambo ya ndoa mnafanyia uchumbani ndio hasara yake.

Tukae kwenye mstari wa Mungu tu tuishi kama Mungu anavyotaka hayo yote sio rahisi kutokea
 
Wewe unaweza kuamamini mtu aliyekupa mwili wake kabla ya kumuoa, maana yake anaweza kumpa mtu mwingine

Nafikiri wanawake wangekuwa wanawakazia hao jamaa sidhani kama Wangefika huko mambo ya ndoa mnafanyia uchumbani ndio hasara yake

Tukae kwenye mstari wa Mungu tu tuishi kama Mungu anavyotaka hayo yote sio rahisi kutokea
Nimekuelewa mkuu
 
Ila wanawake pia wanachangia kutokuolewa na hao waliosota nao...
Unaeza ona mwanamke anamvumilia jamaa ila nyuma ya pazia anamsimanga balaa kutokana na hali yake mwaho wa siku mwanaume anaweka kisasi flani hvi akitoboa ndio hvo
 
Back
Top Bottom