Asilimia 90 Dar hawana ajira

usiambini

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
627
558
WAKATI Dar es Salaam ikiongoza kwa kuwa na viwanda vingi nchini, imeelezwa kuwa, asilimia

90.4 ya wakazi wake hawana ajira.

Akiwasilisha hotuba yake bungeni mjini hapa jana kuhusu hali ya uchumi mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka wa fedha 2015/16, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema ni asilimia 9.6 pekee ya wakazi wa Dar es Salaam ndio walio na ajira licha ya mkoa huo kuwa na viwanda 516.

Mkoa huo unamiliki asilimia 29.2 ya viwanda vyote vilivyopo nchini ukifuatiwa na Arusha wenye viwanda 144 (asilimia 8.1), Shinyanga 101 (asilimia 5.7), Kilimanjaro 96 (asilimia 5.4) na Mwanza 88 (asilimia tano).

Akinukuu utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014, Dk. Mpango alisema watu wenye ajira katika jiji la Dar es Salaam walikuwa 1,927,367, sawa na asilimia 9.6 ya wakazi wote wa jiji hilo, wakati kwenye maeneo mengine ya mjini waliokuwa na ajira ni 5,131,422, sawa na asilimia 25.6 na maeneo ya vijijini walikuwa watu 12,971,350 (asilimia 64.8).

"Kutokana na utafiti huo, ilibainika kuwa, idadi kubwa ya kundi la watu walioajiriwa lilikuwa na umri wa kuanzia miaka 35 hadi 64, ambao walikuwa asilimia 42.5 ya waajiriwa wote," alisema Dk. Mpango.

Waziri huyo alieleza kuwa, utafiti huo ulionyesha nguvukazi ya taifa ilikuwa watu 25,750,116, sawa na asilimia 57 ya watu wote Tanzania Bara.

Alisema kati yao, wanawake walikuwa 13,390,678 (asilimia 52) na wanaume walikuwa 12,359,438 (asilimia 48).

Aidha, Dk. Mpango alisema katika utafiti huo ilibainika kuwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi walikuwa 22,321,924, wakati wasio na uwezo wa kufanya kazi walikuwa 3,428,192.

Kati ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi, Dk. Mpango alisema walioajiriwa walikuwa 20,030,139 na wasioajiriwa walikuwa 2,291,785."Sababu za watu wasio na uwezo wa kufanya kazi zilikuwa ni pamoja na ulemavu na ugonjwa wa muda mrefu," alisema.

Kuhusu uwiano wa ajira kitaifa, Waziri huyo alisema uwiano mkubwa zaidi ulikuwa kwenye maeneo ya vijijini (asilimia 82.2), wakati jiji la Dar es Salaam lilikuwa na uwiano mdogo zaidi wa asilimia 59.8).

Chanzo: Nipashe
 
Kheeee! Mbona wala vumbi kila mara huwa wanawapa risala wabeba maboksi kwamba huku mavumbini mambo ni mswano?

Kumbe huwa ni fiksi tu.
 
Arusha viwanda 8.1% VS Mwanza 5%,haya wapenda ligi mchezo umeishia hapo.

Viwanda vinavyozungumziwa hapo Arusha ni vile vya asili vya kutengeneza vitu kama shanga, mikufu ya culture, vile viatu vya asante Mchaga na zile sandalz za Kimasai wakati viwanda vya Mwanza ni vile vya uvuvi, kuna TBL, Koka, Pepsi n.k.
Yani ukichukua output ya kiwanda kimoja cha Mwanza kama TBL, ni sawa sawa na output ya viwanda vyooote vya Arusha.
Mchezo umeishia hapo!
 
AHAHAAHAHAHAHHAHA...NIMECHEKA KWA HIZI TAKWIMU ZA DR MPANGO...KWELI UKIWA MSOMI UNAFUMBA MACHO HUONI YANAYOENDELEA PEMBENI YAKO...UMEJIFUNIKA MAANDISHI YA WASOMI WENZIO.

HIVI ZILE AJIRA MIL 5 KWA MWAKA KWA MIAKA 10 YA LAISI ALIYEPITA ZILIKUWA HAZIINGIZWI KWENYE TAKWIMU?...

ANYWAY LABDA HIZO AJIRA KWA DAR NI ZA WAFANYAKAZI WA VIWANDANI TUU...SIE WALIMA NYANYA KWA KUMWAGILIA MAJI NDANI YA MABANDA YA PLASTIC YALE YA GREEN HOUSE YALE WANAITA HORTICULTURE AJIRA HIZO HAZIESABIKI...
WALA WALE WAKURYA WA KITUNDA TUMBUKA WANAOLISHA DSM KWA KUKU NA MAYAI HAWAMO KWENYE HIZO TAKWIMU.

SIPENDAGI KUITWA MSOMI NAJIONA KAMA NIMETUKANWA VILE...MAANA WENGI WAO NI VIPOFU WASIOONA UKWELI NJE YA MAKARATASI YALIYOEKSIPAYA TAKWIMU ZAKE.
 
Back
Top Bottom