Itachukua miaka 11 kwa Deni la Serikali kuisha ikiwa hakutakuwa na Mkopo mwingine wowote kwa muda huo huku ikilipa Tsh. Trilioni 8.8 kila mwaka

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Sep 21, 2024
213
668
Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha, hadi kufikia Septemba 2024, zinaonesha Deni la Serikali lilifikia Tsh. Trilioni 98.5 ambapo kwa kipindi cha miaka 9 Deni hilo limeongezeka kwa Tsh. Trilioni 64.2.

Ili Tanzania iondokane na Deni hilo, itachukua miaka 11 kulipa kwa Wastani wa Tsh. Trilioni 8.8 kila mwaka na haitatakiwa kukopa kwa kipindi chote hicho.

Aidha, kwa takwimu za Septemba 2024 kutoka BoT, Deni la Taifa limefikia Dola za Marekani Bilioni 44.89 (Takriban Tsh. Trilioni 118.9) huku Deni la Serikali likichukua 83% ya Deni hilo.

Ukuaji wa Deni la Taifa unapaswa uendane na ukuaji wa uchumi wa nchi ili deni hilo liwe himilivu. Wakati Benjamin William Mkapa, Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa anamaliza muda wake mwishoni mwa mwaka 2005, Deni la Taifa lilikuwa Sh. trillioni 10.93 wakati uchumi wa taifa ukiwa na thamani ya Sh. trilioni 21.4 (Dola za Marekani bilioni 18.4).

Vivyo hivyo, wakati Rais wa Nne, Dk. Jakaya Kikwete alipokuwa anamaliza muda wake mwaka 2015, Deni la Taifa lilikuwa Sh. trilioni 41.82 wakati uchumi wa taifa ukiwa Sh. trlioni 84.28. Hii inaonesha kuwa, katika kipindi cha Dk. Kikwete, Deni la Taifa liliongezeka kwa asilimia 282.6 (zaidi ya mara mbili na nusu) kulinganisha na deni lililoachwa na Rais Mkapa.

Vilevile, Pato la Taifa lilikua kwa Sh. trilioni 62.88 sawa na asilimia 293.8 kutoka Sh. trlioni 21.44 hadi kufikia Sh. trilioni 84.28.

Katika kipindi cha Rais wa Tano, Dk. John Magufuli, Deni la Taifa liliongezeka hadi Sh. trilioni 72.3 kufikia mwezi Machi 2021 ikiwa ni ongezeko la Sh. 39 trilioni sawa na asilimia 72.8. Deni la Taifa lilikuwa ni asilimia 53.3 ya Pato la Taifa la Sh. trilioni 135.5 mwaka 2021.

Aidha, Deni la Taifa limefikia Sh. trilioni 111.3 mwezi Juni 2024. Ni ongezeko la Sh. trilioni 28.7 sawa na asilimia 54, ambapo uchumi wa taifa unatarajiwa kuwa wa thamani ya Sh. trilioni 230.91.

Ripoti ya Benki ya Dunia, "The World Bank Economic Report on Tanzania 2023", imetoa taarifa njema ya ukuaji uchumi wa nchi wa asilimia 5.2 kulinganishwa na ukuaji uchumi wa nchi mwaka 2022 wa asilimia 4.6.

Mbali na kuwapo ukuaji wa kuridhisha wa uchumi wa nchi, bado hali ya umaskini nchini haijapungua kwa kasi ya kuridhisha kutokana na kasi ya ongezeka la watu kwa kiwango cha asilimia tatu.

UHIMILIVU WA DENI LA TAIFA

Kabla mkopeshaji yeyote -- awe ni nchi, benki au mtu binafsi hajafanya uamuzi wa kukopesha fedha kwa mkopaji yeyote awe ni nchi, taasisi au mtu binafsi, ni lazima mkopeshaji awe na vigezo vya kumhakikishia kuwa mkopo atakaotolewa, utarejeshwa na mkopaji.

Vilevile, mkopaji naye anapaswa kuwa na uhakika wa kuwa na uwezo wa kurejesha mkopo anaotarajia kuuchukua kwa kuwa deni ni lazima lirejeshwe na mkopaji kwa aliyemkopesha.

Hivyo, nchi inapotaka kukopa huwa inafanyiwa tathmini ya uwezo wake wa kulipa mkopo unaoombwa ili mkopeshaji ajiridhishe kuhusu uwezo wa mkopaji kurejesha deni lililochukuliwa.

Vivyo hivyo, mkopaji naye anapaswa kujifanyia tathmini ya uwezo wake wa kulibeba deni analotarajia kulikopa na kujihakikishia kuwa ataweza kuwa na uwezo wa kulilipa deni hilo mara litakapoiva.

Kwa mfano, kwenye hotuba ya bajeti ya mwaka 2024/25, Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba (Mb), alisema kuwa kwa mujibu wa tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2023, Deni la Taifa bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

"Katika tathmini hiyo, viashiria vinaonesha kuwa kwa mwaka 2023/24; uwiano wa Deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 35.6 kulinganisha na ukomo wa asilimia 55; uwiano wa deni la nje kwa Pato la Taifa ni asilimia 19 kulinganisha na ukomo wa asilimia 40; na uwiano wa deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 113.2 kulinganisha na ukomo wa asilimia 180," alisema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo aliongeza kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2024, Deni la Taifa lilikuwa Sh. trilioni 91.7. Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Sh. trilioni 60.95 na deni la ndani lilikuwa Sh. trilioni 30.75. Deni hili lilikuwa limeongezeka kwa Sh. trilioni 19.4 sawa na asilimia 26.8 ya deni lililoachwa na Rais wa Tano.

Benki ya Dunia (WB) hutumia Mfumo wa Uhimilivu wa Madeni (Debt Sustainability Factors – DSF) kufanya tathmini ya hatari za uhimilivu wa deni katika nchi zinazoendelea (Developing Countries). Vigezo vinavyotumiwa na WB katika kutathmini uhimilivu wa Deni la Taifa ni pamoja na:

Kwanza; Uainishaji Uwezo wa Kubeba Deni (Debt-Carrying Capacity Classification) – Nchi zinaanishwa kulingana na uwezo wao wa kubeba madeni uliotathminiwa ambao husaidia kubainisha uwezo wa nchi wa kusimamia na kulipa madeni yao kwa ufanisi.

Pili; Viashiria vya Viwango vya Mzigo wa Deni (Threshold Levels for Debt Burden Indicators) – WB huweka viashiria vya viwango vya juu vilivyochaguliwa vya upimaji wa mzigo wa deni kwa nchi husika kama vile uwiano wa Deni la Taifa kwa Pato la Taifa ili kujihakikishia uwezo wa nchi zinazokopa kuwa na uwezo wa kiuchumi kulipa madeni husika.

Tatu; makadirio ya msingi na matukio ya Jaribio la Mfadhaiko (Baseline Projections and Stress Test Scernarios) – Kigezo hiki kinapima namna gani nchi itaweza kustahimili mishtuko ya kiuchumi ya nje na ndani katika kulisimamia deni la nchi vizuri na kuweza kulilipa deni hilo mara litakapoiva.

Nne: Ukadiriaji vihatarishi vya dhiki ya deni (Risk Ratings of Debt Distress) – kwa kuchanganya kanuni elekezi na uamuzi wa wafanyakazi. Benki ya Dunia inazipanga nchi kulingana na viwango vya vihatarishi vinavyoweza kuathiri usimamizi mzuri wa ulipaji madeni ya taifa.

Tano: Ishara za Vihatarishi vya Kiufundi (Mechanical Risk Signals) – Kielezo cha DSF huzalisha mawimbi ya vihatarishi vya kiufundi kulingana na ulinganisho wa viashiria vya deni vya chini ya hali ya msingi na mkazo na vizingiti vinavyohusika kusaidia katika kubainisha viwango vya hatari vya dhiki ya deni la nje na la jumla la taifa.

Sita; Uchambuzi wa Mwaka wa Uhimilivu wa Deni (Annual Debt Sustainability Analysis (DSA)) – Benki ya Dunia huhitaji kila nchi mdeni wake kufanya uchambuzi wa uhimilivu wa madeni ya nchi zinazoendelea kila mwaka ukionesha hali halisi ya uhimilivu wa madeni ya nchi. Takwa hili la Benki ya Dunia huzipa nchi zilizokopa fursa ya kujifanyia tathmini zenyewe ili kujiridhisha kuhusu uwezo wao wa kuhudumia madeni waliyonayo na kujitathmini kama wana uwezo wa kuendelea kukopa.

Saba; Mwongozo wa Uamuzi wa Ukopaji na Ukopeshaji (Guidance for Borrowing and Lending Decisions) - Benki ya Dunia ina miongozo inayoongoza mkopeshaji kumfanyia mkopaji tathmini ya uwezo wake wa kukopa na miongozo inayomwongoza mkopaji kujifanyia tathmini ya uwezo wa kubeba na kulilipa deni analofikiria kukopa.
 
Sisi na vikoba damu damu,sasatunawezaje kuishi bila kuwezeshwa na kausha damu tangu wandani hadi wa kimataifa.
 
Totalitarian tu, tunayo mirafi mingi sana ya kutuingizia mabilioni
 
Back
Top Bottom