Asilimia 45 mabosi wa BoT wakabiliwa kesi za ufisadi
Na Mwandishi wetu
22nd September 2009
B-pepe
Chapa
Maoni
Jumla yao sasa ni watano
Wapo pia maofisa waandamizi
Ni za EPA, Majengo Pacha
Zipo pia za uhujumu uchumi
Benki Kuu ya Tanzania.
Baada ya wakurugenzi wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kufikishwa kortini wiki iliyopita wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, ikijumuishwa na mkurugenzi mwingine mmoja ambaye tayari alikuwa anakabiliwa na kesi nyingine, inafanya karibu nusu ya wakurugenzi wa taasisi hiyo nyeti katika kusimamia uchumi wa nchi kuwa na kesi mahakamani, tathmini ya Nipashe inaonyesha.
Kwa mujibu mfumo mpya wa BoT, kuna kurugenzi 11, huku 5 kati ya hizo, wakuu wake ambao walishika nyadhifa kwenye taasisi hiyo katika kipidi cha miaka walau mitano iliyopita, kujikuta wakifikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi tofauti za wizi, kuisababishia serikali hasara au uhujumu uchumi.
BoT ina kurugenzi zifuatazo, Benki, Usimamizi wa Mabenki, Sera za Uchumi, Soko la Fedha, Usimamizi wa Mawasiliano, Rasilimali na Utawala, Mafunzo, Sheria, Mfumo Malipo wa Taifa na Sekta Ndogo ya Fedha (Microfinance).
Kulingana na kesi zilizoko mahakamani wakurugenzi ngazi za juu watano BoT na maofisa wengine waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali kwa ujumla wao wameisababishia nchi hasara ya jumla ya Sh. 329,431,925,475.52, yaani Sh. bilioni 329.4. Idadi ya wakurugenzi waliofikishwa mahakamani ni sawa na asilimia 45.45 ya kurugenzi 11.
Katika kesi ya kwanza, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa BoT, Amatus Liyumba, alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.1 kwenye mradi wa majengo pacha ya Benki.
Kesi hiyo inatarajia kuanza kusikilizwa maelezo ya awali Ijumaa ijayo mbele ya jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwe, wanaosikiliza shauri hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Liyumba anadaiwa kwamba, akiwa kama Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, alipindisha mkataba wa BoT kuhusu mradi wa ujenzi wa maghorofa pacha na hivyo kuongeza kiasi cha fedha zilizokuwa zikihitajika katika ujenzi.
Ilidaiwa kuwa kutokana na Liyumba kupindisha mkataba huo, aliisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 153,077,715.71 ambazo ni sawa na Sh. 221,197,299,200.96.
Kesi nyingine ni ile inayowakabili wakurugenzi wanne wa benki hiyo, Simon Jengo, Kisima Kimango, Bosco Kimela na Ally Bakari waliofikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala wiki iliyopita na kusomewa mashitaka matatu ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali ya hasara ya Sh bilioni 104.1.
Aidha miongoni mwa washitakiwa hao Kimela pia anakabiliwa na kesi ya wizi wa Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) mali ya BoT na kufanya idadi ya kesi za kuchota fedha za benki zinazomkabili kufikia mbili.
Katika mashitaka yao yaliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Samuel Maweda, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa mshitakiwa wa kwanza Jengo akiwa Mkurugenzi wa Benki na wa pili Kimango akiwa Naibu Mkurugenzi wa Fedha, mwaka 2004 kwa lengo la kumdanganya mwajiri, waliandaa rasimu ya ziada kwa wasambazaji wa noti yenye mkataba wa mwaka 2001, kwa lengo la kumpotosha mwajiri wao.
Ilidaiwa kuwa mwaka 2005, mshitakiwa wa kwanza akiwa mtumishi wa umma aliagiza kuchapishwa kwa thamani kubwa ya fedha ikilinganishwa na iliyoandaliwa na kitengo cha BoT akiwa na lengo la kumpotosha mwajiri wake.
Katika shitaka la tatu, washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kwa kutumia nyadhifa zao walishindwa kutekeleza majukumu yao kwa kuandaa rasimu ya ziada yenye mkataba wa mwaka 2001 ilionyesha thamani ya juu wa kuchapisha kiwango cha noti kuliko mkataba halali unavyoeleza.
Ilidaiwa kuwa kwa kitendo cha washitakiwa kufanya hivyo, kiliisababishia serikali hasara ya Sh. 104,158,536,146.
Hata hivyo, kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi pale upelelezi utakapokamilika na shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu.
Kesi hiyo imeahirishwa itatajwa Oktoba 2, mwaka huu.
Pia, kesi nyingine ni ile ya wizi wa Sh milioni 207.2 za Epa mali ya benki hiyo, inayowakabili aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Madeni, Imani Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Madeni Ester Komu na Kaimu Mwanasheria wa BoT, Bosco Kimela. Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Jopo la Mahakimu Watatu Ignas Kitusi, Catheline Revocat na Eva Nkya wanaosikiliza katika Mahakama ya Kisutu.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa BoT, kwa kutumia nyadhifa zao na kutokuwa makini walipitisha malipo yasiyo halali ya Sh. 207, 284, 391.44, mali ya Benki hiyo kupitia kampuni ya Rashhas ya Tanzania na General Marketing ya nje ya nchi, ambapo waliisababishia serikali upotevu wa kiasi hicho cha fedha.
Mwakosya, Komu na Sofia Joseph, ambaye naye ni Mwanasheria wa BoT, wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa benki hiyo kwa kutumia nyadhifa zao na kutokuwa makini walipitisha malipo yasiyo halali ya Sh. bilioni 3.8 mali ya BoT.
Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya jopo la mahakimu watatu Samuel Kirua, Beatrice Mutungi na Ilivin Mugeta katika Mahakama ya Kisutu.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa bila kuhakiki uwepo wa deni hilo waliisababishia serikali upotevu wa Sh 3,868,805,737.13, kwa Kampuni ya Mwibare Farm ya Tanzania na Lakshmi Textile Mills Ltd ya Mumbai.
Hata hivyo, Liyumba na Kimela wako gerezani wakisubiri kesi zao kusikilizwa wakati, Komu, Joseph na Mwakosya wako nje kwa dhamana.
CHANZO: NIPASHE
This is the Bank of Tanzania or i must say a Big Boat ndio maana wanapita mitaani wakijidai kuwa wao ndio fedha nchini kumbe ni wezi. Je Tutafika????