Asilimia 45 mabosi wa BoT wakabiliwa kesi za ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asilimia 45 mabosi wa BoT wakabiliwa kesi za ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Sep 25, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asilimia 45 mabosi wa BoT wakabiliwa kesi za ufisadi
  Na Mwandishi wetu
  22nd September 2009
  B-pepe
  Chapa
  Maoni
  Jumla yao sasa ni watano
  Wapo pia maofisa waandamizi
  Ni za EPA, Majengo Pacha
  Zipo pia za uhujumu uchumi
  Benki Kuu ya Tanzania.

  Baada ya wakurugenzi wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kufikishwa kortini wiki iliyopita wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, ikijumuishwa na mkurugenzi mwingine mmoja ambaye tayari alikuwa anakabiliwa na kesi nyingine, inafanya karibu nusu ya wakurugenzi wa taasisi hiyo nyeti katika kusimamia uchumi wa nchi kuwa na kesi mahakamani, tathmini ya Nipashe inaonyesha.

  Kwa mujibu mfumo mpya wa BoT, kuna kurugenzi 11, huku 5 kati ya hizo, wakuu wake ambao walishika nyadhifa kwenye taasisi hiyo katika kipidi cha miaka walau mitano iliyopita, kujikuta wakifikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi tofauti za wizi, kuisababishia serikali hasara au uhujumu uchumi.

  BoT ina kurugenzi zifuatazo, Benki, Usimamizi wa Mabenki, Sera za Uchumi, Soko la Fedha, Usimamizi wa Mawasiliano, Rasilimali na Utawala, Mafunzo, Sheria, Mfumo Malipo wa Taifa na Sekta Ndogo ya Fedha (Microfinance).

  Kulingana na kesi zilizoko mahakamani wakurugenzi ngazi za juu watano BoT na maofisa wengine waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali kwa ujumla wao wameisababishia nchi hasara ya jumla ya Sh. 329,431,925,475.52, yaani Sh. bilioni 329.4. Idadi ya wakurugenzi waliofikishwa mahakamani ni sawa na asilimia 45.45 ya kurugenzi 11.

  Katika kesi ya kwanza, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa BoT, Amatus Liyumba, alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.1 kwenye mradi wa majengo pacha ya Benki.

  Kesi hiyo inatarajia kuanza kusikilizwa maelezo ya awali Ijumaa ijayo mbele ya jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwe, wanaosikiliza shauri hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

  Liyumba anadaiwa kwamba, akiwa kama Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, alipindisha mkataba wa BoT kuhusu mradi wa ujenzi wa maghorofa pacha na hivyo kuongeza kiasi cha fedha zilizokuwa zikihitajika katika ujenzi.

  Ilidaiwa kuwa kutokana na Liyumba kupindisha mkataba huo, aliisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 153,077,715.71 ambazo ni sawa na Sh. 221,197,299,200.96.

  Kesi nyingine ni ile inayowakabili wakurugenzi wanne wa benki hiyo, Simon Jengo, Kisima Kimango, Bosco Kimela na Ally Bakari waliofikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala wiki iliyopita na kusomewa mashitaka matatu ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali ya hasara ya Sh bilioni 104.1.

  Aidha miongoni mwa washitakiwa hao Kimela pia anakabiliwa na kesi ya wizi wa Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) mali ya BoT na kufanya idadi ya kesi za kuchota fedha za benki zinazomkabili kufikia mbili.

  Katika mashitaka yao yaliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Samuel Maweda, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa mshitakiwa wa kwanza Jengo akiwa Mkurugenzi wa Benki na wa pili Kimango akiwa Naibu Mkurugenzi wa Fedha, mwaka 2004 kwa lengo la kumdanganya mwajiri, waliandaa rasimu ya ziada kwa wasambazaji wa noti yenye mkataba wa mwaka 2001, kwa lengo la kumpotosha mwajiri wao.

  Ilidaiwa kuwa mwaka 2005, mshitakiwa wa kwanza akiwa mtumishi wa umma aliagiza kuchapishwa kwa thamani kubwa ya fedha ikilinganishwa na iliyoandaliwa na kitengo cha BoT akiwa na lengo la kumpotosha mwajiri wake.

  Katika shitaka la tatu, washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kwa kutumia nyadhifa zao walishindwa kutekeleza majukumu yao kwa kuandaa rasimu ya ziada yenye mkataba wa mwaka 2001 ilionyesha thamani ya juu wa kuchapisha kiwango cha noti kuliko mkataba halali unavyoeleza.

  Ilidaiwa kuwa kwa kitendo cha washitakiwa kufanya hivyo, kiliisababishia serikali hasara ya Sh. 104,158,536,146.

  Hata hivyo, kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi pale upelelezi utakapokamilika na shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu.

  Kesi hiyo imeahirishwa itatajwa Oktoba 2, mwaka huu.

  Pia, kesi nyingine ni ile ya wizi wa Sh milioni 207.2 za Epa mali ya benki hiyo, inayowakabili aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Madeni, Imani Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Madeni Ester Komu na Kaimu Mwanasheria wa BoT, Bosco Kimela. Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Jopo la Mahakimu Watatu Ignas Kitusi, Catheline Revocat na Eva Nkya wanaosikiliza katika Mahakama ya Kisutu.

  Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa BoT, kwa kutumia nyadhifa zao na kutokuwa makini walipitisha malipo yasiyo halali ya Sh. 207, 284, 391.44, mali ya Benki hiyo kupitia kampuni ya Rashhas ya Tanzania na General Marketing ya nje ya nchi, ambapo waliisababishia serikali upotevu wa kiasi hicho cha fedha.

  Mwakosya, Komu na Sofia Joseph, ambaye naye ni Mwanasheria wa BoT, wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa benki hiyo kwa kutumia nyadhifa zao na kutokuwa makini walipitisha malipo yasiyo halali ya Sh. bilioni 3.8 mali ya BoT.

  Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya jopo la mahakimu watatu Samuel Kirua, Beatrice Mutungi na Ilivin Mugeta katika Mahakama ya Kisutu.

  Ilidaiwa kuwa washitakiwa bila kuhakiki uwepo wa deni hilo waliisababishia serikali upotevu wa Sh 3,868,805,737.13, kwa Kampuni ya Mwibare Farm ya Tanzania na Lakshmi Textile Mills Ltd ya Mumbai.

  Hata hivyo, Liyumba na Kimela wako gerezani wakisubiri kesi zao kusikilizwa wakati, Komu, Joseph na Mwakosya wako nje kwa dhamana.

  CHANZO: NIPASHE

  This is the Bank of Tanzania or i must say a Big Boat ndio maana wanapita mitaani wakijidai kuwa wao ndio fedha nchini kumbe ni wezi. Je Tutafika????
   
 2. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bado sana kuna kashfa nyingi sana hazijaguswa. Percent itaongezeka tu...
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wasiishie BOT peke yake. Mashirika mengi ya UMMA yanatafunwa kwelikweli. Waende pia NSSF, PPF, DAWASA, DAWASCO, TANESCO, MNH, UDSM.....na Agencies zilizoanzishwa miaka ya hivi karibuni kama TEMESA, EWURA, SUMATRA,....
  Nchi hii inatafunwa ni balaa!?
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  nchii hiii imetawaliwa na wizi kila kona ,basi waanzishe sheria kama ya China labda tutapata kuendelea ,wanatuumiza sana hawa watu
   
 5. Foma Limao

  Foma Limao New Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni mwanzo tu wa mapambano dhidi ya uozo wote, hopeful one day haki na ukweli vitachukua mkondo wake.
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Labda ingekuwepo independent watchdog itakayochaguliwa na walalahoi kuchunguza mashirika ya umma otherwise itakuwa kupeleka kesi ya Nyani kwa Ngedere...
   
 7. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani hawa jamaa wamejenga majumba ya kifahari yenye thamani kubwa sana. ukiuliza,oooh other businesses. Jamani watz tuache haya mambo ya kusema other businesses kumbe hakuna lolote ni wizi na rushwa.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hatari kubwa sana, kama hazina kuu ya kuhifadhi fedha zetu watu wanaiba namna hiyo.

  balaa kubwa
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ishu ni kwamba independent watchdog wanakuwapo but effectiveness yao itakuwa kubwa kama hao watchdog watakuwa truly independent na si waganga njaa. Hawa watu walipoingia BOT wengi wao walikuwa watu wa kawaida leo hii wana utajiri wa kutupa wakijidai eti marupurupu kumbe dili zenyewe hizi
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tumezoea kuona haya Tanzania yetu, Watu wanasema kuwa Ufisadi haupo nani wa kulaumiwa
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haya ni mambo ya kufanya JMK apewe sifa kamili na za dhati, kabla ya JMK hatujaona Rais yeyote wa Tanzania akiyashughulikia haya madudu japo, angalau kidogo.

  Leo tunamuona JMK yupo cool, anayashughulikia haya madudu systematically, bila udikteta, bila upuuzi, na napenda kuwahakikishia wa Tanzania, hakuna atakaeponyoka, wote zao zikifika watashughulikwa ipasavyo.

  Ahsante Jakaya Mrisho Kikwete, wenye macho tunayaona, wenye masikio tunayasikia. Wasio na macho wala masikio, tutawaona humu, hata mazuri kama haya watakuwa hawayaoni wala hawayasikii!
   
 12. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutampa sifa siku atakayojisalimisha kortini kwa kuingia madarakani kwa kutimia fedha zilizoibiwa kwenye akaunti za EPA.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama una ushahidi kwa nini usiende mahakamani? unangoja nini?
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Sep 25, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Habari hii imekanushwa vikali na uongozi wa BOT, angalieni kwenye magazeti ya Majira na HabariLeo ya leo tr 25/09/2009.
   
 15. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Watasema nini hao, si wanataka kuonekana kuwa wanafanya kazi nzuri.

  Nimeshawaambia Kikwete ni hatari, mnakataa. Mngekuwa ni wafanya kazi wa BoT ndio mngefahamu ni nini ninachozungumza. Si kwema huko sasa hivi.

  SIMBA MWENDA POLE NDIO MLA NYAMA. Kikwete anaweza!!!!!
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Sep 25, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ama kweli ukimpenda kipofu utamwita ana makengeza! Sasa umeanza kubisha hata kabla hujaona taarifa yenyewe ya BOT inasema nini? Na kama umeiona basi ipinge kwa hoja na sio kwa general comments kuhusu utawala wa Kikwete!
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie binafsi sijaiona hiyo taarifa majira labda mtu aipost hapa jamii but hata wakikanusha watabakia kukanusha kwa madai kuwa hawa watu kesi yao ipo mahakamani na inshughulikiwa hivyo basi jamii isikimbilie kuhukumu but ishu inakuja watufafanulie utajiri wao wameupata wapi. Vikao visivyokwisha kila siku, Overtime za uongo, semina zisizokwisha na training mtu anasoma masters miaka minne au mtu anaenda kufanya mitihani ya bodi anachukua study leave ya mwaka. Hao ni watu wa chini. wa juu ndio aibu tupu madudu yanafumuka kila siku. Kiukweli BOT inahitaji kufumuliwa yote abakie ndulu peke yake wengine wafanyiwe uhakiki upya
   
Loading...