ASILI YA NENO "KARIAKOO"

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,518
2,000
H

Kumbukumbu ya wapagazi Waingereza kwenye Sanamu ya Askari, Dar es Salaam.


Wapagazi Waafrika upande wa jeshi la Kijerumani
Kikosi cha wapagazi (ing . Carrier Corps ) kilikuwa kitengo cha jeshi la Uingereza wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia .


Kiliujumuisha wanaume Waafrika walioajiriwa au kulazimishwa kubeba mzigo wa jeshi la Uingereza kwenye mapigano ya Vita Kuu ya Kwanza katika Afrika ya Mashariki dhidi jeshi la Wajerumani lililoongozwa na Paul von Lettow-Vorbeck .
Waingereza walikuwa na tatizo kusafirisha chakula, risasi na mahitaji mengine kwa ajili ya jeshi kubwa katika maeneo pasipo na barabara wala reli.
Jeshi la kikoloni la Uingereza lilitumia wanejeshi Waingereza, Wahindi na wazungu wa Afrika Kusini hasa wakati wa miaka ya kwanza ya vita. Wanajeshi hao walizoea kusafiri na kiwango cha mzigo wa binafsi.
Kinyume chake kamada Mjerumani von Lettow-Vorbeck aliwahi kuandaa jeshi la askari Waafrika walioweza kutumia vyakula vilivyopatikana hata porini na wasiozoea kuwa na mizigo mingi. Kwa hiyo Wajerumani walitumia wapagazi wachache kuliko Waingereza ingawa hata wao waliajiri au kulazimisha Waafrika kufanya kazi hii kwa ajili ya mahitaji yao.
Upande wa Waingereza wanajeshi wao hawakuzoea vyakula vya mahali. Kwa hiyo kazi ya kusafirisha kilogramu 1 ya
mchele kutoka mabandari ya pwani hadi kufikia wanajeshi barani ilihitaji mara nyini kilogramu 50 za mchele zilizohitajika kulisha wapagazi waliobeba akiba.
Kwa kazi hii kubwa utawala wa kikoloni wa Waingereza ulianzisha kitengo cha pekee kilichoitwa "Carrier Corps". Ilitumia takriban wanaume 400,000 Waafrika kwa kazi zake, na katika muda wa vita kwa jumla takriban milioni 1 Waafrika walikuwa sehemu ya kikosi cha wapagazi upande wa Uingereza. Imekadiriwa ya kwamba angalau 95,000 kati ya hao walikufa, wengi kutokana na njaa na magonjwa
[1] . Usimamizi wa kazi ya kujenga kikosi hiki kilikuwa chini ya Mwingereza Oscar Ferris Watkins aliyewahi kufika Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (yaani Kenya) kama mtawala wa kikoloni mwenye cheo cha mkuu wa wilaya.
Kuna kumbukumbu ya wapagazi mahali mbalimbali kama vile
kwenye sanamu ya Askari huko Dar es Salaam (Tanzania)
kwenye makumbusho ya Vita Kuu huko Kenyatta Avenue , Nairobi.
kwenye makumbusho ya Vita Kuu huko Mbala (jina la kikoloni lilikuwa Abercorn) katika Zambia
Miji mingi katika Afrika Mashariki ina sehemu zinazoitwa kwa majina kama " Kariakoo " kama Dar es Salaam na
Dodoma au " Kariakor" huko Nairobi. Ni mahali ampo wapagazi waliostaafu katika kikosi cha wapagazi walijenga nyumba zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom