Habari zenu humu,
Kutokana na historia ya mwafrika enzi za ulimbombo kabla ya mzungu, babu zetu walituhadithia kwamba hapakuwepo nguo, wanasema walifunika mbele tu tena kwa magome ya mti, na ngozi za wanyama tena ngozi walivaa machief au watu maarufu katika jamii.
Najiuliza tena hivi kipindi hicho kwa uvaaji ule je heshima ilikuwa hamna? Au ilikuwepo? Maana nauhakika walikuwa nusu uchi zaidi ya hata vimini tuvionavyo sasa,nauhakika kwa uvaaji ule wa mababu walivyokuwa na kazi za kuinama nyuma kote kulibaki wazi, na waliishi na familia zao na mabinti zao.
Swali hapa kama ilikuwepo tangu mababu je kinachoonyesha kwamba sahivi kuvaa kimini au kanga moja kuwa ni kukiuka maadili ni nini? Je; Maadili ya mtanzania asili yake ni nguo au utupu?Je kwanini pamoja na kujistiri hivi watu wanazidi kuwa na tabia za kinyama? Tunaposema maadili na tamaduni za asili ya mtanzania ni kujistiri tunatumia historia gani?
Naomba mwenye kujua atujuze hapa kwanini sahivi nguo tunazo lakini tabia ni mbaya zaidi ya enzi za mababu walioishi uchi?