1. Kizota - hili lilitokana na mkutano wa CCM wa Kizota ambapo Mwalimu Nyerere alikuwa anauliza maswali ya kebehi na kusubiri watu wajibu japo maswali yalikuwa yanajijibu; jina hili alipewa Said Mwamba kutokana na kuwapiga chenga za kebehi za kusubiria mabeki tena!
2. Boli Zozo - hili lilitokana na mfungaji wa Stella Artois iliyoigalagaza Simba kwenye mechi ya fainali ya CAF; jina hili alipewa James Tungaraza wa Yanga kutokana na uwezo wake wa kuifunga Simba; nilishuhudia kwa macho yangu mwenyewe akiwafunga mabao mawili nunge!
3. Chabala - hili lilitokana na uwezo wa ajabu wa kudaka penalti, mashuti ya ana kwa ana na washambuliaji na kudaka mipira katika miguu yao kama kipa wa zamani wa Zambia; jina hili alipewa Companero kabla akiwa golikipa kabla hajabadilishwa na Kocha Wenga na kuwa mshambuliaji na winga wa kutisha!
Huyo Sanifu Lazaro aliwatingisha sana mabeki wa timu pinzaniTunaomba wanahistoria wa soka watueleze asili ya majina haya ya utani:
1. Tingisha
2. Ninja
3. Kaburu
4. Mzee wa Kiminyio
5. Tekelo
6. Mensah
7. Zigzag
8. Scania
9. Sure Boy
10. Golden Boy
11. Ball Juggler
2. Salum Kabunda 'Ninja'- Salum Kabunda wakati anaibuka kama beki wa kati Tukuyu Stars miaka ya katikati ya 1980, alikuwa na staili moja ya kuhamisha mpira kwa kuruka na miguu yote. Kwa kuwa wakati ule Michael Dudikoff alikuwa katoa filamu yake ya 'American Ninja', mdau Kabunda akakwaa jina hilo.
8. Godwin Aswile 'Scania'- Alikuwa beki pacha wa Kabunda katika kikosi cha Tukuyu Stars kilichobeba ubingwa mwaka 1986, inasemekana umbo lake la miraba minne na umahiri wake katika kuwafunika washambuliaji ulimfanya abatizwe jina hilo.
Nakumbuka huyu jamaa Abdallah Suleiman aliibuka kwenye Taifa Cup akiwa na timu ya mkoa wa Kilimanjaro,alikuwa winga mkali sana, ndiye wa kwanza kuitwa Kaburu, Kaburu wa pili ni huyu kiongozi wa timu yangu ya Simba ya Dar, japo kulikuwa na "maKaburu" wengine wadogowadogo.Mkuu jina la Kaburu si alipewa Kenneth Mkapa wa Yanga, ama?
Mkuu umetisha sana kwa kuongezea tu kutoka mkoani kwetu kule kuliwahi kutokea mawinga fulani wawili Celestine "Sikinde" Mbunga na Steven Mapunda "Garincha" hawa watu wawili kwa nyakati tofauti mmoja akicheza Yanga na mwingine Simba ilikuwa hatari sana.Mkuu Camponero, kwa ufahamu wangu asili ya baadhi ya haya majina na wenye nayo ni kama ifuatavyo:-
1. Sanifu Lazaro 'Tingisha'- Hili jina alilipata akiwa RTC Kigoma kutokana na umahiri wake wa kufumania nyavu
2. Salum Kabunda 'Ninja'- Salum Kabunda wakati anaibuka kama beki wa kati Tukuyu Stars miaka ya katikati ya 1980, alikuwa na staili moja ya kuhamisha mpira kwa kuruka na miguu yote. Kwa kuwa wakati ule Michael Dudikoff alikuwa katoa filamu yake ya 'American Ninja', mdau Kabunda akakwaa jina hilo.
6. Juma Pondamali 'Mensah'- Miaka ya 70, inasemekana huko Ghana kulikuwa na kipa maarufu aliyechezea Asante Kotoko aliyejulikana kwa jina la Mensah. Huyu kipa alikuwa mahiri sana kiasi cha kupelekea kipa wa zamani wa Yanga na Pan African, Juma Pondamali kubatizwa jina hilo miaka ya 1980.
7. John Makelele 'ZigZag'- Marehemu huyu, mojawapo wa washambuliaji hatari wa Pamba miaka ya mwishoni 1980s, uwezo wake wa kupiga chenga za kuyumba zilimbatiza jina hilo kutoka kwa mashabiki.
8. Godwin Aswile 'Scania'- Alikuwa beki pacha wa Kabunda katika kikosi cha Tukuyu Stars kilichobeba ubingwa mwaka 1986, inasemekana umbo lake la miraba minne na umahiri wake katika kuwafunika washambuliaji ulimfanya abatizwe jina hilo.
9. Abubakar Salum 'Sure Boy'- Kwa wale wazee wa miaka ya 1980, hawatasahau fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1986 uwanja wa Taifa DSM. Yanga walikuwa wameshalala mabao 2-0 kwa El-Merreikh ya Sudan kukiwa kumesalia chini ya dakika 10 mchezo uishe, ndipo Abubakar Salum (akiwa hajulikani) alipoingizwa na kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika tano. Yanga walipoteza mchezo huo kwa penalti, lakini wanazi wa Jangwani wakawa wamepata shujaa mpya waliyembatiza jina la 'Sure Boy'.
10. Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' later 'DHL'- Sina uhakika, pengine kutokana na umahiri wake wa kutafuta na kufunga magoli muhimu alipokuwa akiichezea Simba enzi zake. Mogella alikuja kujulikana pia kama DHL pale alipoichezea Yanga kwa ufanisi wake wa krosi kama winga msimu wa mwaka 1993 na kuiwezesha kutwaa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kule Uganda.
11. Malota Soma 'Ball Juggler'- Labda kutokana na uwezo wa kumiliki mpira. Wenye kujua zaidi watasaidia hapa.
Mkuu nadhani ilikuwa Stella Abidjan..maana nakumbuka Stella Artois kilikuwaga kilagi maaruf sana kipindi kile...