Asili ya Majina ya Utani ya Wachezaji

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,605
2,000
1. Kizota - hili lilitokana na mkutano wa CCM wa Kizota ambapo Mwalimu Nyerere alikuwa anauliza maswali ya kebehi na kusubiri watu wajibu japo maswali yalikuwa yanajijibu; jina hili alipewa Said Mwamba kutokana na kuwapiga chenga za kebehi za kusubiria mabeki tena!

2. Boli Zozo - hili lilitokana na mfungaji wa Stella Artois iliyoigalagaza Simba kwenye mechi ya fainali ya CAF; jina hili alipewa James Tungaraza wa Yanga kutokana na uwezo wake wa kuifunga Simba; nilishuhudia kwa macho yangu mwenyewe akiwafunga mabao mawili nunge!

3. Chabala - hili lilitokana na uwezo wa ajabu wa kudaka penalti, mashuti ya ana kwa ana na washambuliaji na kudaka mipira katika miguu yao kama kipa wa zamani wa Zambia; jina hili alipewa Companero kabla akiwa golikipa kabla hajabadilishwa na Kocha Wenga na kuwa mshambuliaji na winga wa kutisha!
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,605
2,000
Tunaomba wanahistoria wa soka watueleze asili ya majina haya ya utani:

1. Tingisha
2. Ninja
3. Kaburu
4. Mzee wa Kiminyio
5. Tekelo
6. Mensah
7. Zigzag
8. Scania
9. Sure Boy
10. Golden Boy
11. Ball Juggler
 
Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,952
2,000
HAMISI THOBIAS 'GAGA' nasikia jamaa alikuwa na magamba sana enzi za utoto wake.(mungu ailaze roho yake pema peponi amina)
Focus Lukas 'STANDARDIZER' alikuwa attacking midfilder na alipata jina hili kwa sababu ya kuweza kuitoa timu yake kwenye kufungwa na hatimaye kushinda.
 
Mkosoaji

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
363
195
Mkuu Camponero, kwa ufahamu wangu asili ya baadhi ya haya majina na wenye nayo ni kama ifuatavyo:-

1. Sanifu Lazaro 'Tingisha'- Hili jina alilipata akiwa RTC Kigoma kutokana na umahiri wake wa kufumania nyavu

2. Salum Kabunda 'Ninja'- Salum Kabunda wakati anaibuka kama beki wa kati Tukuyu Stars miaka ya katikati ya 1980, alikuwa na staili moja ya kuhamisha mpira kwa kuruka na miguu yote. Kwa kuwa wakati ule Michael Dudikoff alikuwa katoa filamu yake ya 'American Ninja', mdau Kabunda akakwaa jina hilo.

6. Juma Pondamali 'Mensah'- Miaka ya 70, inasemekana huko Ghana kulikuwa na kipa maarufu aliyechezea Asante Kotoko aliyejulikana kwa jina la Mensah. Huyu kipa alikuwa mahiri sana kiasi cha kupelekea kipa wa zamani wa Yanga na Pan African, Juma Pondamali kubatizwa jina hilo miaka ya 1980.

7. John Makelele 'ZigZag'- Marehemu huyu, mojawapo wa washambuliaji hatari wa Pamba miaka ya mwishoni 1980s, uwezo wake wa kupiga chenga za kuyumba zilimbatiza jina hilo kutoka kwa mashabiki.

8. Godwin Aswile 'Scania'- Alikuwa beki pacha wa Kabunda katika kikosi cha Tukuyu Stars kilichobeba ubingwa mwaka 1986, inasemekana umbo lake la miraba minne na umahiri wake katika kuwafunika washambuliaji ulimfanya abatizwe jina hilo.

9. Abubakar Salum 'Sure Boy'- Kwa wale wazee wa miaka ya 1980, hawatasahau fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1986 uwanja wa Taifa DSM. Yanga walikuwa wameshalala mabao 2-0 kwa El-Merreikh ya Sudan kukiwa kumesalia chini ya dakika 10 mchezo uishe, ndipo Abubakar Salum (akiwa hajulikani) alipoingizwa na kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika tano. Yanga walipoteza mchezo huo kwa penalti, lakini wanazi wa Jangwani wakawa wamepata shujaa mpya waliyembatiza jina la 'Sure Boy'.

10. Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' later 'DHL'- Sina uhakika, pengine kutokana na umahiri wake wa kutafuta na kufunga magoli muhimu alipokuwa akiichezea Simba enzi zake. Mogella alikuja kujulikana pia kama DHL pale alipoichezea Yanga kwa ufanisi wake wa krosi kama winga msimu wa mwaka 1993 na kuiwezesha kutwaa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kule Uganda.

11. Malota Soma 'Ball Juggler'- Labda kutokana na uwezo wa kumiliki mpira. Wenye kujua zaidi watasaidia hapa.
 
hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,574
2,000
mkosoaji umenipeleka mbali sana....mpira pesa haimati ila unaucheza kutoka moyoni achana na watoto wa siku hizi hawa!
 
Mkosoaji

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
363
195
Haya majina ya zamani ya kiasili yalikuwa na mvuto tofauti na siku hizi wanafananishwa tu na masupastaa wa ulaya kama Adebayor, Ballack, Cannavaro na wengineo.
 
Isaac

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
928
1,000
kuna mchezaji anaitwa John Boko "Adebayor" vipi siku tukicheza na Togo?
 
Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,458
2,000
1. Kizota - hili lilitokana na mkutano wa CCM wa Kizota ambapo Mwalimu Nyerere alikuwa anauliza maswali ya kebehi na kusubiri watu wajibu japo maswali yalikuwa yanajijibu; jina hili alipewa Said Mwamba kutokana na kuwapiga chenga za kebehi za kusubiria mabeki tena!

2. Boli Zozo - hili lilitokana na mfungaji wa Stella Artois iliyoigalagaza Simba kwenye mechi ya fainali ya CAF; jina hili alipewa James Tungaraza wa Yanga kutokana na uwezo wake wa kuifunga Simba; nilishuhudia kwa macho yangu mwenyewe akiwafunga mabao mawili nunge!

3. Chabala - hili lilitokana na uwezo wa ajabu wa kudaka penalti, mashuti ya ana kwa ana na washambuliaji na kudaka mipira katika miguu yao kama kipa wa zamani wa Zambia; jina hili alipewa Companero kabla akiwa golikipa kabla hajabadilishwa na Kocha Wenga na kuwa mshambuliaji na winga wa kutisha!

Mkuu nadhani ilikuwa Stella Abidjan..maana nakumbuka Stella Artois kilikuwaga kilagi maaruf sana kipindi kile...
 
NG'OTIMBEBEDZU

JF-Expert Member
Aug 11, 2010
1,077
1,500
Tunaomba wanahistoria wa soka watueleze asili ya majina haya ya utani:

1. Tingisha
2. Ninja
3. Kaburu
4. Mzee wa Kiminyio
5. Tekelo
6. Mensah
7. Zigzag
8. Scania
9. Sure Boy
10. Golden Boy
11. Ball Juggler
Huyo Sanifu Lazaro aliwatingisha sana mabeki wa timu pinzani

Kabunda alikuwa bingwa wa kupiga watu mateke kama maninja wa kwenye sinema

Abdallah Suleiman ,Alikuwa white kama wale wa kule bondeni na jinsi aliyokuwa myanyasaji kwa mabeki kama makaburu vile.

Ni Abeid Mziba alikuwa mchawi wa vichwa, wakamfananisha na yule mchawi maarufu enzi hizo aliitwa Tekero (Yanga bwana...!)

Juma Pondamali alikuwa hodari golini kama yule kipa maarufu wa Ghana enzi hizo

John Makelele alikuwa anachambua mabeki kwa staili ya mshono wa nguo wa zigzaga

Godwin Aswile, alikuwa na nguvu mithili ya gari aina ya Scania

Zamoyoni Mogela mwana wa dhahabu, thamani yake ilikuwa kama dhahabu enzi hizo
 
NG'OTIMBEBEDZU

JF-Expert Member
Aug 11, 2010
1,077
1,500
2. Salum Kabunda 'Ninja'- Salum Kabunda wakati anaibuka kama beki wa kati Tukuyu Stars miaka ya katikati ya 1980, alikuwa na staili moja ya kuhamisha mpira kwa kuruka na miguu yote. Kwa kuwa wakati ule Michael Dudikoff alikuwa katoa filamu yake ya 'American Ninja', mdau Kabunda akakwaa jina hilo.

8. Godwin Aswile 'Scania'- Alikuwa beki pacha wa Kabunda katika kikosi cha Tukuyu Stars kilichobeba ubingwa mwaka 1986, inasemekana umbo lake la miraba minne na umahiri wake katika kuwafunika washambuliaji ulimfanya abatizwe jina hilo.

Salum Kabunda alipewa jina "Ninja", akiwa Yanga na si Tukuyu Stars.

Godwin Aswile hakucheza pamoja na Kabunda Tukuyu Stars, pacha wa Aswile Tukuyu Stars alikuwa Selemani Mathew Luwungo na wote walihamia Yanga baadae, na vilevile kwa nyakati tofauti wakatua Simba.
 
NG'OTIMBEBEDZU

JF-Expert Member
Aug 11, 2010
1,077
1,500
Mkuu jina la Kaburu si alipewa Kenneth Mkapa wa Yanga, ama?
Nakumbuka huyu jamaa Abdallah Suleiman aliibuka kwenye Taifa Cup akiwa na timu ya mkoa wa Kilimanjaro,alikuwa winga mkali sana, ndiye wa kwanza kuitwa Kaburu, Kaburu wa pili ni huyu kiongozi wa timu yangu ya Simba ya Dar, japo kulikuwa na "maKaburu" wengine wadogowadogo.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,276
2,000
Razak Yusuph - Caleca huyu alichezea African Sports ya Tanga

Hivi huyu Celestine Sikinde Mbunga jina lake limekaa kama nick fulani

Juma Amir Maftah - Pele wa Mwanza alipata jina akiwa Pamba ya Mwanza baadae Simba na mwanawe Amir Maftah anakipiga hadi sasa sijui simba au Yanga

Nakumbuka kuna kina Itutu Kigi walikuwa wakali wa CDA Dodoma Simba ikamchukua nick name siikumbuki
japo Charles Hilary alikuwa anawapa majina sana akiwafanisha na wachezaji wa ulaya kina Terry Butcher na Garl Lineaker Paul Parker n.k

Nawakumbuka Rostam Ndunguru John Bosco baadae Yanga - Nyota Nyekundu (Red Star) Maskani Mtaa wa Kongo kwa wauza mitumba hata jengo lao litakuwa limeliwa na wajanja wanakula kodi au ndio walishaliuza. hii timu nilikuwa naipenda sana
 
Anselm

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
1,711
1,500
Mkuu Camponero, kwa ufahamu wangu asili ya baadhi ya haya majina na wenye nayo ni kama ifuatavyo:-

1. Sanifu Lazaro 'Tingisha'- Hili jina alilipata akiwa RTC Kigoma kutokana na umahiri wake wa kufumania nyavu

2. Salum Kabunda 'Ninja'- Salum Kabunda wakati anaibuka kama beki wa kati Tukuyu Stars miaka ya katikati ya 1980, alikuwa na staili moja ya kuhamisha mpira kwa kuruka na miguu yote. Kwa kuwa wakati ule Michael Dudikoff alikuwa katoa filamu yake ya 'American Ninja', mdau Kabunda akakwaa jina hilo.

6. Juma Pondamali 'Mensah'- Miaka ya 70, inasemekana huko Ghana kulikuwa na kipa maarufu aliyechezea Asante Kotoko aliyejulikana kwa jina la Mensah. Huyu kipa alikuwa mahiri sana kiasi cha kupelekea kipa wa zamani wa Yanga na Pan African, Juma Pondamali kubatizwa jina hilo miaka ya 1980.

7. John Makelele 'ZigZag'- Marehemu huyu, mojawapo wa washambuliaji hatari wa Pamba miaka ya mwishoni 1980s, uwezo wake wa kupiga chenga za kuyumba zilimbatiza jina hilo kutoka kwa mashabiki.

8. Godwin Aswile 'Scania'- Alikuwa beki pacha wa Kabunda katika kikosi cha Tukuyu Stars kilichobeba ubingwa mwaka 1986, inasemekana umbo lake la miraba minne na umahiri wake katika kuwafunika washambuliaji ulimfanya abatizwe jina hilo.

9. Abubakar Salum 'Sure Boy'- Kwa wale wazee wa miaka ya 1980, hawatasahau fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1986 uwanja wa Taifa DSM. Yanga walikuwa wameshalala mabao 2-0 kwa El-Merreikh ya Sudan kukiwa kumesalia chini ya dakika 10 mchezo uishe, ndipo Abubakar Salum (akiwa hajulikani) alipoingizwa na kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika tano. Yanga walipoteza mchezo huo kwa penalti, lakini wanazi wa Jangwani wakawa wamepata shujaa mpya waliyembatiza jina la 'Sure Boy'.

10. Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' later 'DHL'- Sina uhakika, pengine kutokana na umahiri wake wa kutafuta na kufunga magoli muhimu alipokuwa akiichezea Simba enzi zake. Mogella alikuja kujulikana pia kama DHL pale alipoichezea Yanga kwa ufanisi wake wa krosi kama winga msimu wa mwaka 1993 na kuiwezesha kutwaa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kule Uganda.

11. Malota Soma 'Ball Juggler'- Labda kutokana na uwezo wa kumiliki mpira. Wenye kujua zaidi watasaidia hapa.
Mkuu umetisha sana kwa kuongezea tu kutoka mkoani kwetu kule kuliwahi kutokea mawinga fulani wawili Celestine "Sikinde" Mbunga na Steven Mapunda "Garincha" hawa watu wawili kwa nyakati tofauti mmoja akicheza Yanga na mwingine Simba ilikuwa hatari sana.
Mwenye ufahamu kuhusu asili ya hizi nick name zao anaweza kutujuza.
Halafu kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa anakwenda kwa jina la Mohamed Hussein "Mmachinga" aliyepewa jina la Mmachinga kutokana na asili yake kuwa kule watokeako Wamachinga - Mtwara.
 
popiexo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
742
195
Daud Salum " Brece Lee" RIP
Ahmed Amasha "Mathematician"
Athuman Juma Chama "Jogoo"
"GeneraLi" Juma Mkambi
Sunday Juma, Mfukuza upepo
Said Sued "Scud"
Athuman Maulid " Big Man"
Ayub Salim "Beki Mstaarabu"
Frank Kasanga "Bwalya"
Mao Mkami "Ball Dancer"
Octavia Mrope "OC"
Deo Njohole "OCD"
Method Mogella "FUNDI" RIP.
Silvatus Ibrahim "Police"
Nonda Shaban "Papii"
Athuman Abdallah "China"
Hussein Mwakuruzo "Ruga"
"Captain" Issa Athuman
Ezekiel Grayson "Juju man"
"Zico wa Kilosa" Said Mrisho
Makumbi Juma "Homa ya Jiji"
Michael Poul "Nylon"
Khalid Bitebo "Zembwela"
Visent Peter "Pinokyo"

Popiexo "Urimbo" Maana mpira ulikuwa unanata.
 
Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
9,172
2,000
sanifu lazaro 'mkuu wa mkoa'
victor costa 'nyumba'
sunday manara 'computer'
kitwana manara 'popat'
ally yusufu 'tigana'
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom