Asili ya jina la Afrika utokana na jina. ALKEBU-LAN

Asili ya jina la Afrika utokana na jina. ALKEBU-LAN

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Hatupaswi kuendelea kuita bara letu AFRICA na kuanza kuita jina lake halisi la ALKEBU-LAN, kama jinsi ma babu zetu walivyo kua wakiliita hapo awali, ALKEBU-LAN lenye maana ya "ASILI YA UHAI DUNIANI"

Jina la Africa halina maana yoyote wala hali akisi jambk lolote kutoka kwenye lugha zetu za asili.

Kuna baadhi ya simulizi zina sema asili ya jina hili la Africa limetokana na jina la mzungu alie fika Africa mwanzoni mwa karne ya 8 alieitwa Leo Africanus

Dola yenye nguvu wakati huo ya Roma walitaka kuharibu muunganiko iliopo kati ya waafrika na utamaduni wao kwa kubadiri majina ya koo, nchi na kubadiri jina la bara zima ilikua ni moja ya mbinu walio itumia,
Jina lilibadirishwa baada ya vita ya ghafla kati ya Roma ikiongozwa na Publius Cornelius Scipio dhidi Carthage,.
Waroma walipo mkamata Carthage wali badili jina na kuliita bara letu Africa

Baadhi ya simulizi zisizo rasmi zinasema kua msafiri huyo alie itwa Leo Afrianus alitaka bara la Africa liitwe Africa neno kutoka lugha ya kigiriki "a-phike"

Pia kuna wanao amini kua neno, "Africa" limetoka kwenye neno la Kilatini "aprica" lenye maana ya jua kali.

Kutokana vyanzo vifuatavyo vya Kenematic Histori of Africa, The definition of Alkebulan vinasema kua "Jina halali la bara la Africa ni Alkebulan, Alkebu-lan " chanzo cha uhai ulimwenguni au Bustani ya Eden

Alkebulan ni neno kongwe zaidi kutumika kama jina la bara la Africa na lenye asili ya lugha ya hindigenous Lugha iliotumika na wa Moor, Wanubi, Wanumidi, waKhart na wa Ethiopia

Kwa watu wa magharibi hasa Waroma walio liita bara hili afrika ilimaanisha "The land Afer " kwa tafasiri isio rasmi ambapo wao walianzia Africa Carthage ambayo ni Tunisia ya sasa kua nchi hii ilikuja baadae baada ya uumbaji na ni ya mwisho kuumbwa.

Asili ya neno hili la na maana yake kiingerza cha kale kutoka Uingereza ni "dust" yani uchafu
Neno Afri lililo anzishwa Afrika
-the Phoenician `far, the dust; yaani taka taka au uchafu
– maana nyingine iliyo tolewa kwenye kiingireza cha america ya kusini ni (mahali bila baridi).

Mwana historia Leo Africanus (1495-1554) anazungumzia asili ya neno la kigiriki phrike(φρικε, lenye maana ya Baridi na kutisha), ambapo ukiweka "a" yenye maana ya kukanusha basi neno hilo linakua nchi bila baridi na ya kutisha

Licha ya kua hoja yake haikutililiwa maanani baada ya utofauti wa kimatamshi kati ya ph na f kumefanya wana zuoni kutupilia mbali hoja yake hiyo..

Kwahiyo jina la asili la bara la Afrika ni lipi?

Kama nilivyosema hapo awali mwanzo kabisa liliitwa "Alkebulan". Neno "Alkebulan" lenye maana chanzo cha uhai kwa mwanadamu au Bustani ya Edeni

Pia ikumbukwe kua kabla ya neno "Alkebulan" kutolewa na kuanza kutumia Africa kuna hilo lilitumika zaidi Afrika ya kaskazini

Mwishoni mwa karne ya 17 jina la Afrika lilikua jina jipya masikioni mwa watu, jina walilo leta wazungu sababu wakati huo wazungu walipo safiri kwenye maeneo tofauti walipenda kutumia majina ya kilatini kuliko majina ya lugha nyingine

Maeneo mengi yaliitwa Afruca(pamoja na Africa lenye) na lilitumika tu kwenye baadh ya maeneo madogo madogo ya Africa ila jina la sili na kongwe zaidi ni ALKEBULAN.
 
kwanini neno Alkebulan linahusishwa na lugha ya Kiarabu, ilhali ni jina la kale la Afrika?

Hii hapa ni sababu kuu:

1. Mawasiliano ya kihistoria kati ya Afrika na Waarabu

Kabla ya ukoloni wa Ulaya, kulikuwa na uhusiano wa karibu wa kibiashara, kiutamaduni, na kidini kati ya Afrika ya Kaskazini na Mashariki (kama Zanzibar, Pwani ya Kenya, Somalia, Ethiopia) na ulimwengu wa Kiarabu. Waarabu walikuwa na ushawishi mkubwa, hasa kupitia:

Biashara ya Bahari ya Hindi

Dini ya Uislamu

Uenezi wa lugha ya Kiarabu kama lugha ya dini, elimu na biashara


Kwa hivyo, baadhi ya majina ya maeneo au dhana yaliyoenea Afrika yalichukuliwa au kutafsiriwa kwa lugha ya Kiarabu, hata kama yalitokana na asili ya Kiafrika.

2. "Alkebulan" kama neno lililopitia lugha ya Kiarabu

Kuna ushahidi kuwa neno Alkebulan halikutokana moja kwa moja na Kiarabu, bali lilichukuliwa na Waarabu au wasomi wa Kiarabu walipokuwa wakielezea bara hili, kwa kutumia muktadha wao wa lugha. Hivyo, ni kama tafsiri ya dhana ya Kiafrika kwa Kiarabu — sio kwamba Waarabu waliipa jina, bali waliandika au kulihifadhi kwa maandishi yao.

3. Ukosefu wa maandiko ya kale barani Afrika

Lugha nyingi za Kiafrika hazikuwa na maandishi ya muda mrefu kabla ya ujio wa Waarabu na baadaye Wazungu. Kwa hiyo, taarifa nyingi kuhusu historia ya Afrika zilihifadhiwa kupitia maandishi ya Waarabu au Wagiriki, hata kama zilitokana na maarifa ya Kiafrika.


---

Kwa kifupi: Waarabu hawakuanzisha jina Alkebulan, bali walilihifadhi au kulitumia kwa maandiko yao kwa sababu wao walikuwa na mifumo ya maandishi na walihusika sana na Afrika kabla ya ukoloni wa Ulaya.
 
Neno "Alkebulan" linatoka katika lugha za kale za Kiafrika, hasa linahusishwa na lugha ya Kiarabu cha kale au lugha za Kusini mwa Sahara kama Kikushiti au Kibantu fulani za zamani. Ingawa asili yake halisi inabishaniwa na wanahistoria na wasomi, tafsiri ya jumla ya "Alkebulan" ni:

"Mama wa wanadamu" au "Ardhi ya wanadamu weusi".



Ni mojawapo ya majina ya kale sana yaliyotumika kuelezea bara la Afrika kabla ya kuitwa "Africa" na Warumi.

Kwa hivyo, "Alkebulan" si neno la Kiswahili moja kwa moja, lakini linaweza kueleweka kwa wasemaji wa Kiswahili kutokana na maana yake ya kihistoria na tamaduni za Kiafrika.
 
haya ni baadhi ya majina ya kuiita afrika endapo litabadilishwa maana jina ndio kila kitu:-
•Land of Gods
•Holy Land
•Land of the Sun
•Garden of Eden
•Motherland
•Alkebulan
•Ancient Afrika
•Aethiopia
•Kemet
 
Back
Top Bottom