Asili ya jina Kilimanjaro

Asili ya jina Kilimanjaro

Inasemekana kwamba katika jiji la Dar kilikuwa na mtu aliyeitwa MUSA HASSAN..huyu jamaa alikuwa mbabe sana anaogopwa balaa!..kama unavyojua jiji la dar asili yake ni kabila la wazaramo...basi yule MUSA HASSAN alikuwa anaenda mitaa flani hivi kutisha watu, wale wenyeji wa pale wakawa wanajifungia ndani huku wakiwaambia watoto wao "MWANA NYAMALA, MSASANI KOKWIZA" yaani (Mwanangu nyamaza Musa Hassan anakuja).... basi hayo maeneo yakaitwa MWANANYAMALA na kule alipokuwa akiishi MUSA HASSAN pakaitwa MSASANI.
Hii hata kama ni chai inaendana na uhalisia.
 
Kiboriloni Moshi. Hili jina limetokana na neno "Kibo Only" mzungu alifika maeneo hayo akiwa na lengo la kuona vizuri vilele vya mlima Kilimanjaro, cha ajabu aliishia kuona kilele kimoja cha Kibo pekee. Ndipo alipojikuta akiropoka Kibo only, wachaga wakajua amesema kiboroloni. Ikawa ndio jina
Niliwahi kusikia Kibo alone, hapa unasema Kibo only?
 
Inasemekana kwamba Asili ya jina Kilimanjaro ni kwamba
mzungu alikwenda marangu na
akakutana na mzee wa kichaga miaka
hiyo ya nyuma na akauliza huu mlima
unaitwa nini? mzee wa kichaga akajibu
"Kilema Kyaro" akiwa anamaana ni
mlima wa ajabu kwa jinsi ulivyokuwa
ukichemka volcano. Basi mzungu
akapotosha jina na kuuita kilima-njaro!
lakini asili yake ni "KILEMA KYARO"
Hebu na wewe tupe asili ya majina ya mikoa ,wilaya ,vijiji,kata na mitaa unayoifahamu
Kilema_kisichowezekana
Kyaro_safari. .....yaani hapafikiki
 
Inasemekana kwamba katika jiji la Dar kilikuwa na mtu aliyeitwa MUSA HASSAN..huyu jamaa alikuwa mbabe sana anaogopwa balaa!..kama unavyojua jiji la dar asili yake ni kabila la wazaramo...basi yule MUSA HASSAN alikuwa anaenda mitaa flani hivi kutisha watu, wale wenyeji wa pale wakawa wanajifungia ndani huku wakiwaambia watoto wao "MWANA NYAMALA, MSASANI KOKWIZA" yaani (Mwanangu nyamaza Musa Hassan anakuja).... basi hayo maeneo yakaitwa MWANANYAMALA na kule alipokuwa akiishi MUSA HASSAN pakaitwa MSASANI.

Kokwiza peke yake ikakosa eneo
 
Kiboriloni Moshi. Hili jina limetokana na neno "Kibo Only" mzungu alifika maeneo hayo akiwa na lengo la kuona vizuri vilele vya mlima Kilimanjaro, cha ajabu aliishia kuona kilele kimoja cha Kibo pekee. Ndipo alipojikuta akiropoka Kibo only, wachaga wakajua amesema kiboroloni. Ikawa ndio jina

Kabla ya wazungu wao walipaitaje
 
Kule kolomije kulikuwa na mzungu aliyeishi miaka ya nyuma aliyeitwa Jonathan, baada ya kuona wenyeji wanashindwa kutamka hilo jina kwa ufasaha, akashauri wawe wanamwita tu J.
Aliwaambia "Call me J". Eneo hilo likaitwa kwa Kolomije.
 
Inasemekana kwamba Asili ya jina Kilimanjaro ni kwamba
mzungu alikwenda marangu na
akakutana na mzee wa kichaga miaka
hiyo ya nyuma na akauliza huu mlima
unaitwa nini? mzee wa kichaga akajibu
"Kilema Kyaro" akiwa anamaana ni
mlima wa ajabu kwa jinsi ulivyokuwa
ukichemka volcano. Basi mzungu
akapotosha jina na kuuita kilima-njaro!
lakini asili yake ni "KILEMA KYARO"
Hebu na wewe tupe asili ya majina ya mikoa ,wilaya ,vijiji,kata na mitaa unayoifahamu
"ANOTHER SCHOOL OF THOUGHT" kabla ya kuja kwa dini za wageni wachagga walikuwa wanauabudu mlima huu. Kumbuka asili ya mchagga kabla ya dini walikuwa wanaabudu mawingu/anga. Akiamka asubuhi lazima atazame juu mawinguni na kushukuru . Ndio maaana ya neno " RUWA" mawingu, RUWA -MANGI ... nk.

Sasa waliamini mlima ni wa Mungu na wakawa wanauita " KILIMA (mlima) KYA (wa)RUWA (Mungu) ... "KILIMAKYARUWA".....Mzungu akashindwa kutamka akasema KILIMANJARO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom