Asili ya jina Kilimanjaro

Asili ya jina Kilimanjaro

jina la wilaya ya Same nilisikia lilitokana na wazungu kuona sehemu zote za wilaya hiyo zinafanana ndio wazungu wakawa wanatamka kila mara neno 'same' ya kiingereza kwa maana kila mahali kunafanana, hatimaye ndio ikaitwa Same.
 
Inasemekana kwamba katika jiji la Dar kilikuwa na mtu aliyeitwa MUSA HASSAN..huyu jamaa alikuwa mbabe sana anaogopwa balaa!..kama unavyojua jiji la dar asili yake ni kabila la wazaramo...basi yule MUSA HASSAN alikuwa anaenda mitaa flani hivi kutisha watu, wale wenyeji wa pale wakawa wanajifungia ndani huku wakiwaambia watoto wao "MWANA NYAMALA, MSASANI KOKWIZA" yaani (Mwanangu nyamaza Musa Hassan anakuja).... basi hayo maeneo yakaitwa MWANANYAMALA na kule alipokuwa akiishi MUSA HASSAN pakaitwa MSASANI.
Wamakonde halichi hawa
 
Kiboriloni Moshi. Hili jina limetokana na neno "Kibo Only" mzungu alifika maeneo hayo akiwa na lengo la kuona vizuri vilele vya mlima Kilimanjaro, cha ajabu aliishia kuona kilele kimoja cha Kibo pekee. Ndipo alipojikuta akiropoka Kibo only, wachaga wakajua amesema kiboroloni. Ikawa ndio jina
Kibo alone and not kibo only
 
Weee K.I.A.Z.I kweli. Bila mzungu huwezi andika kitu. Majina yote yapo kabla ya wazumgu.
Singida ni neno la kibarbeig au mang'ati ISINGIDA maana yake pundamilia.Inasemekana ziwa singida kulikuako pundamilia wengi sana.Hivyo hao mang'ati walipofika wakawakuta wakinywa maji.Mzugu akashindwa kuita hao punda isingida na kuita singida mpaka leo.
 
Serengeti ni matokeo ya wajerumani kushindwa kutamka neno la kimasai siringeti likiwa na maana sehemu tambarare mwisho wake usioonekana
 
huyo mzungu alikuwa hajawahi kuona mlima ko ikabidi aulize eti kile ni nini????
kweli!!!!?!
 
Inasemekana kwamba katika jiji la Dar kilikuwa na mtu aliyeitwa MUSA HASSAN..huyu jamaa alikuwa mbabe sana anaogopwa balaa!..kama unavyojua jiji la dar asili yake ni kabila la wazaramo...basi yule MUSA HASSAN alikuwa anaenda mitaa flani hivi kutisha watu, wale wenyeji wa pale wakawa wanajifungia ndani huku wakiwaambia watoto wao "MWANA NYAMALA, MSASANI KOKWIZA" yaani (Mwanangu nyamaza Musa Hassan anakuja).... basi hayo maeneo yakaitwa MWANANYAMALA na kule alipokuwa akiishi MUSA HASSAN pakaitwa MSASANI.
Umetisha mkuu
 
Asili ya Chekereni. Mzungu alimwambia mchaga aangalie kama treni inakuja " Check Train" lakini kwa kuwa mchaga hakuelewa akamwambia mwenzake "anasema Chekereni" na ikawa hivo mpaka leo ndo mana Chekereni unaona kuna reli ipo pale ndio asili ya jina hilo
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji3] [emoji3] [emoji3] kwa mshana jr maeneo hayo!!
 
Ukweli ni huu: Kwa lugha ya Kichaga cha Marangu jambo likishindikana wanasema 'Kyalema' Safari moja inaitwa 'kyaro' nyingi zinaitwa 'shiaro' Wachaga wa zamani hizo walijaribu kupanda huo mlima mara kadhaa wakashindwa. Kwa hivyo wakauita ule mlima 'Kyilema Shiaro' (yaani mlima ulioshinda safari) Wazungu walipokuja wakaambiwa huo mlima unaitwa 'Kyilema Shiaro' Wakatamka 'Kilima Njiaro" wakaandika hivyo hivyo Kilimanjaro
 
Zanzibar kuna sehemu kunaitwa Bububu, asili yake kuna bubu alikuwa anaogelea mtoni wakati anaogelea akawa anazama, hivyo ikabidi aombe msaada, ndio ile kuita bu bu bu, pakaitwa ivyo
Na pale panapoitwa mchamba wima hebu tupe historia yake sheikh
 
Ukweli ni huu: Kwa lugha ya Kichaga cha Marangu jambo likishindikana wanasema 'Kyalema' Safari moja inaitwa 'kyaro' nyingi zinaitwa 'shiaro' Wachaga wa zamani hizo walijaribu kupanda huo mlima mara kadhaa wakashindwa. Kwa hivyo wakauita ule mlima 'Kyilema Shiaro' (yaani mlima ulioshinda safari) Wazungu walipokuja wakaambiwa huo mlima unaitwa 'Kyilema Shiaro' Wakatamka 'Kilima Njiaro" wakaandika hivyo hivyo Kilimanjaro
kama kuna ukweli vile
 
Mlima Kilimanjaro ni muunganiko wa maneno mawili, ambayo ni Mlima na neno Njaro, neno njaro maana yake ni Mungu. Kabla ya ujio wa wazungu wenyeji waliokuwa kandokando ya huo mlima walikuwa wakiamka asubuhi wanageukia huko mlimani na kuutemea mate kama ishara ya kuabudu, walikuwa wanaamini ndio Mungu wao hivyo kitendo cha kuutemea mate ni ishara ya ibada ili uweze kufanikiwa. Maelezo hayo niliyapata shule ya msingi somobla histioria miaka hiyo.
 
Na pale panapoitwa mchamba wima hebu tupe historia yake sheikh
Ilikuwa ni sehemu ya jumuuya (public) penye bomba la maji watu wakioga pale mahala pa wazi. Ndio asili yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom