Le poisson d'avril (Samaki wa Aprili)
Wazungu wameiita April Fool kwa jina la 'le poisson d'avril' (Samaki wa Aprili). Na sababu hii ni kutokana na jua linavyosogea kutoka nyumba ya zodiaki (nyota za unajimu) ya Pisces (Nyota ya samaki) ikielekea nyumba nyingine. Au kwa sababu ya neno la poisson ambalo maana yake ni samaki, hivyo ni ugeuzaji wa neno la 'passion' ambayo ina maana ya 'kuteseka'. Kwa hiyo ni alama ya kuteseka aliyovumulia Nabii 'Iysa (Alayhis Salaam) kama walivyodai Wakristo. Na madai yao haya yalitokea wiki ya kwanza katika mwezi wa April.
Baadhi ya makafiri wameiita siku hii 'Siku nzima ya wajinga' kama inavyojulikana Kingereza. Hii ni kwa sababu uongo wanaousema ili wale wanaousikia waamini kwa hiyo wanakuwa ni waathirika wa wale wanaowafanyia dhihaka.
Utajo wa mwanzo kabisa kwa Lugha ya Kingereza ilikuwa ni katika gazeti la Dreck. Siku ya pili ya Aprili 1698 M, gazeti hili lilitaja kwamba idadi kadha ya watu walialikwa kuhudhuria uoshaji wa watu weusi katika mnara wa London asubuhi ya siku ya mwanzo ya Aprili.
Tukio maarufu kabisa lililotokea Ulaya tarehe 1 Aprili lilikuwa wakati gazeti la Kingereza 'Evening star' lilipotangaza mwezi wa Machi 1746 M kwamba siku ya pili tarehe 1 Aprili, kutakuwa na gwaride la punda mji wa Islington Uingereza. Watu wakakimbilia kuwatazama wanyama hao na kulikuwa na zahma kubwa. Wakaendelea kusubiri na walipochoka kusubiri, waliuliza kutaka kujua hili gwaride litakuweko baada ya muda gani. Hawakupata jibu, hivyo wakatambua kuwa wamekuja kufanya maonyesho yao wenyewe kama kwamba wao ndio mapunda.
Mmoja wao ameandika kuhusu asili ya uzushi huu kwa kusema: Wengi wetu tunasherehekea siku inayojulikana kuwa ni April Fool, au ikiwa itafasiriwa kihalisi 'Siku ya Ujanja'. Lakini je, tunajua siri chungu inayohusikana na siku hii?