Asili na chimbuko la kabila Wanyantuzu

Asili na chimbuko la kabila Wanyantuzu

Think2

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
2,193
Reaction score
3,958
ASILI NA KOO ZA BANANTUZU AU WANYANTUZU.

Utangulizi.

Wanyantuzu au Banantuzu hawa ni kundi la Wasukuma wa Mashariki ya Usukuma, wanaofahamika kama Bana-Kiya au Wanakiya.

Bana-Kiya au Wasukuma wa Mashariki wanaopatikana mkoani Simiyu huzungumza kisukuma Cha rahaja inayoitwa KIMNAKIYA.
Rahaja ya Kimnakiya imegawanyika mara mbili;
■Rahaja ya kwanza ni ile inayozungumzwa wilaya za Bariadi na Itilima, ambayo hufahamika kama "GINANTUZU" au KINYANTUZU. ■Rahaja ya pili ni ile inayozungumzwa wilaya za Maswa na Meatu ambayo na yenyewe hufahamika kama JINANG'WAGALA au KINANG'WAGALA.

ASILI, CHIMBUKO NA KOO ZA BANANTUZU.
Asili ya jina BANANTUZU linaanzia katika Utemi wa Ntuzu Kwa Mtemi Ndaturu ambaye alitawala Utemi huo Hadi uhuru na Kufutwa kwa mamlaka ya kitemi kiserikali Mwaka 1962/1963.

BANANTUZU maana yake ni watu au wenyeji wa Utemi wa Ntuzu japo kuwa Kwa sasa Wasukuma wote wanaotokea Bariadi hujiita BANANTUZU nafikiri hili ni jina ambalo Wasukuma wa Utemi wa Kanadi, Itilima na Dutwa hujumuishwa kutokana na Kuongea kisukuma Cha rahaja moja inayotofautiana kidogo sana.

Lakini pia Wasukuma wa Utemi wa Ntuzu ndiyo Wasukuma waliokuwa na Watawala wenye nguvu na ushawishi mkubwa kiutawala Kuliko temi zingine za Bariadi.

BANANTUZU ambao ndiyo Wasukuma wenyeji wa Wilaya ya Bariadi Wana Koo zao maarufu sana ambazo ni Babinza, Bachama, Bakwaya, Baasi nulu Bashi, Bahunda, Baseka nulu Basega, Babungu, Bakamba, Bayemba, Balong'we, Basamba, Balega, Bakamba nk. Ndiyo maana Banantuzu wengi Wana majina ya ukoo ya wanawake kama vile Minza, Nchama, Nkwaya, Ng'wasi, Ng'hunda, Nseka, Mungu, Nkamba, Nyemba, Long'we, Nega nk.

ASILI NA CHIMBUKO LA BANANTUZU.
BANANTUZU ni Chimbuko la Mwingiliano wa kabila la Wasukuma na Makabila kutoka jirani na Usukuma kama vile Wataturu, Wanyamwezi,Wamasai, Washashi, Wazinza, Wanyiramba, Watindiga na Wadzabe au Wasandawe, Wanyaturu. nk. Wasukuma -Banantuzu Wana Mwingiliano na Wasukuma wa Mwanza na Shinyanga na ndiyo maana baadhi ya Koo zilizopo Bariadi Zina asili ya kutoka Mwanza kama vile Bakwimba (Nkwimba), Bagolo(Ngolo), Bakela (Nkela), Batimba (Ntimba) na Basiya(Nsiya) na Bakamba (Nkamba) kutoka Shinyanga.

Wasukuma -Banantuzu Wamekuwa na Mahusiano ya Karibu sana na Makabila ya kutokea Mashariki ya Usukuma kama vile Wamasai, Wataturu, Wanyiramba, Wanyaturu na Wadzabe nk. Ushahidi huu unaonekana katika maswala ya kiimani hasa pale makuani wa jadi wa napokuwa wanaagua huwa wanataja majina ya Wakurugenzi wa Wataturu na Wamasai lakini pia Wasukuma huwa Wanaomba upande wa Mashariki wakiwataja Bahanya au Bakula Batale bha Balatulu na Bamasayu. Vile vile uganga wa Umanga ambao ndiyo uganga maarufu Usukumani hasa Bariadi una asili au ulienezwa Usukumani na Balatulu Kwa Wasukuma kuzaliwa kidawa na Walatulu.

Lakini pia Wataturu Wanahistoria ya kuishi Usukumani miaka mingi iliyopita hasa maeneo ya Kanadi, ambapo pia kulikuwa na Mganga maarufu aliyefahamika Kwa jina la SITA na Mpwa wake NINDWA au Nyindwa. Inaaminika kuwa Ng'alang'ayi na Sinana ni moja ya Wataturu wa mwanzo kuishi Usukuma ya Mashariki.

Lakini pia ukiwa Wilaya ya Itilima Kuna eneo Linaitwa Gambasingu ambalo linahusishwa na kuishi Kwa Wataturu maeneo hayo. Wataturu waliozamia Usukumani Walifanya baadhi Yao kuoleana na Wasukuma na ndiyo maana ukiwa Bariadi Kuna Wasukuma wana maumbile ya kitaturu na kimasai kabisa.

Lakini pia Kuna tambiko la KANUDA linalohusishwa na Wamasai nafikiri Wasukuma wa Bariadi Wanafahamu namna Tambiko Hilo linavyofanyika, na Wasukuma wengi wa Bariadi Wana majina ya KANUDA.

pia Wana majina ya kitaturu kama vile, Singu, Magina, Sugilo, Lagu, Gamawishi, Wishi au Weshi nk. Hii inaonesha wazi kuwa Kuna mahusiano ya Karibu kati ya Wasukuma na Wataturu na Wamasai.

Wasukuma -Banantuzu ni moja ya Wasukuma maarufu walioshiriki katika kufuata biashara ya chumvi ya Nyaraja Mkoani manyara ambapo huko walikutana na Makabila ya kutoka Singida kama vile Wanyiramba na Wanyisanzu pia Wanyaturu na kuanzisha mahusiano ya kuoleana, ambapo Wasukuma walipendezwa na wanawake weupe kutokea Kwa Makabila hayo.

dhahiri kuwa asili ya Wasukuma wa ukoo wa Babungu ni makabila ya Wabungu na Wanyiramba.
NB; Msukuma kwa mwanamke mweupe humwambii kitu ,sura sio shida zao wao ni weupe tu basi 😁
Source; Bujora sukuma historical site
 
Asante sana Mkuu kwa andiko lako japo nina swali. Na huwa nasahau kuwauliza wakubwa hivi inakuwaje pale unapomsalimia mkubwa wako. Unaanza kusema Ee Minza, Ee Nkwaya, Ee Nseka hayo yote ni majina ya Kike.

Swali jingine je Wanyantuzu ukoo wao umepitia kwa Mama au umepitia Baba

Yaani ni matrilineal society au Patriline society?
 
Kwa mama na wanasalimiana kupitia mjina ya mama zao
 
Cha kuongezea Ni wachawi sana , mali zao nyingi wanazipata katika ushirikina . Ukiingia anga zao kwa kumuharibia biashara au kazi umekwisha . Pia ndiyo jamii ya wasukuma wenye dharau sana .
Uchawi hauna kabila mkuu kila sehemu kn warozi
 
Kwa mama na wanasalimiana kupitia mjina ya mama zao
Hapana Mkuu nime notisi kitu
Mama yangu au Wajomba zangu huwa wananisalimia Ng'wamayo na Mimi naitikia Eee Minza

Baba au Shangazi zangu huwa wananisalimia Ng'waBaba naitikia Eee Minza

Swali langu Wasukuma /Wanyantuzu Je ukoo wao umepitia kwa Mama au umepitia Baba?
 
Asante sana Mkuu kwa andiko lako japo nina swali. Na huwa nasahau kuwauliza wakubwa hivi inakuwaje pale unapomsalimia mkubwa wako. Unaanza kusema Ee Minza, Ee Nkwaya, Ee Nseka hayo yote ni majina ya Kike.

Swali jingine je Wanyantuzu ukoo wao umepitia kwa Mama au umepitia Baba

Yaani ni matrilineal society au Patriline society?
Wasukuma wote ni patrilineal ukoo wote ni kwa baba.

Kuhusu salamu kuanza kwa E minza, enkwaya , esega na enkwimba ni, kuonesha heshima, kutii mamlaka ya mkubwa , asili ya mhusika anayesalimiwa na kutambua tu mapokeo ya Mila.

Ukimsalimia hivyo Kama ni mzazi atakujibu nghw'abhabha, (baba yake)kama ni kaka, dada, atakujibu "ngw'aguku" (babu yenu ) Kama ni babu au Bibi atakujibu ngw'anene") (yeye maana ndiyo anakuwa mwenye ukoo )
Kama ni hamhusiani basi salamu inakuwa kwa kutaja mababu zenu tu kama ngw'akija na mwingine atajibu kwa kutaja babu yako "ngw'amaduka"
 
ASILI NA KOO ZA BANANTUZU AU WANYANTUZU.

Utangulizi.

Wanyantuzu au Banantuzu hawa ni kundi la Wasukuma wa Mashariki ya Usukuma, wanaofahamika kama Bana-Kiya au Wanakiya.

Bana-Kiya au Wasukuma wa Mashariki wanaopatikana mkoani Simiyu huzungumza kisukuma Cha rahaja inayoitwa KIMNAKIYA.
Rahaja ya Kimnakiya imegawanyika mara mbili;
■Rahaja ya kwanza ni ile inayozungumzwa wilaya za Bariadi na Itilima, ambayo hufahamika kama "GINANTUZU" au KINYANTUZU. ■Rahaja ya pili ni ile inayozungumzwa wilaya za Maswa na Meatu ambayo na yenyewe hufahamika kama JINANG'WAGALA au KINANG'WAGALA.

ASILI, CHIMBUKO NA KOO ZA BANANTUZU.
Asili ya jina BANANTUZU linaanzia katika Utemi wa Ntuzu Kwa Mtemi Ndaturu ambaye alitawala Utemi huo Hadi uhuru na Kufutwa kwa mamlaka ya kitemi kiserikali Mwaka 1962/1963.

BANANTUZU maana yake ni watu au wenyeji wa Utemi wa Ntuzu japo kuwa Kwa sasa Wasukuma wote wanaotokea Bariadi hujiita BANANTUZU nafikiri hili ni jina ambalo Wasukuma wa Utemi wa Kanadi, Itilima na Dutwa hujumuishwa kutokana na Kuongea kisukuma Cha rahaja moja inayotofautiana kidogo sana.

Lakini pia Wasukuma wa Utemi wa Ntuzu ndiyo Wasukuma waliokuwa na Watawala wenye nguvu na ushawishi mkubwa kiutawala Kuliko temi zingine za Bariadi.

BANANTUZU ambao ndiyo Wasukuma wenyeji wa Wilaya ya Bariadi Wana Koo zao maarufu sana ambazo ni Babinza, Bachama, Bakwaya, Baasi nulu Bashi, Bahunda, Baseka nulu Basega, Babungu, Bakamba, Bayemba, Balong'we, Basamba, Balega, Bakamba nk. Ndiyo maana Banantuzu wengi Wana majina ya ukoo ya wanawake kama vile Minza, Nchama, Nkwaya, Ng'wasi, Ng'hunda, Nseka, Mungu, Nkamba, Nyemba, Long'we, Nega nk.

ASILI NA CHIMBUKO LA BANANTUZU.
BANANTUZU ni Chimbuko la Mwingiliano wa kabila la Wasukuma na Makabila kutoka jirani na Usukuma kama vile Wataturu, Wanyamwezi,Wamasai, Washashi, Wazinza, Wanyiramba, Watindiga na Wadzabe au Wasandawe, Wanyaturu. nk. Wasukuma -Banantuzu Wana Mwingiliano na Wasukuma wa Mwanza na Shinyanga na ndiyo maana baadhi ya Koo zilizopo Bariadi Zina asili ya kutoka Mwanza kama vile Bakwimba (Nkwimba), Bagolo(Ngolo), Bakela (Nkela), Batimba (Ntimba) na Basiya(Nsiya) na Bakamba (Nkamba) kutoka Shinyanga.

Wasukuma -Banantuzu Wamekuwa na Mahusiano ya Karibu sana na Makabila ya kutokea Mashariki ya Usukuma kama vile Wamasai, Wataturu, Wanyiramba, Wanyaturu na Wadzabe nk. Ushahidi huu unaonekana katika maswala ya kiimani hasa pale makuani wa jadi wa napokuwa wanaagua huwa wanataja majina ya Wakurugenzi wa Wataturu na Wamasai lakini pia Wasukuma huwa Wanaomba upande wa Mashariki wakiwataja Bahanya au Bakula Batale bha Balatulu na Bamasayu. Vile vile uganga wa Umanga ambao ndiyo uganga maarufu Usukumani hasa Bariadi una asili au ulienezwa Usukumani na Balatulu Kwa Wasukuma kuzaliwa kidawa na Walatulu.

Lakini pia Wataturu Wanahistoria ya kuishi Usukumani miaka mingi iliyopita hasa maeneo ya Kanadi, ambapo pia kulikuwa na Mganga maarufu aliyefahamika Kwa jina la SITA na Mpwa wake NINDWA au Nyindwa. Inaaminika kuwa Ng'alang'ayi na Sinana ni moja ya Wataturu wa mwanzo kuishi Usukuma ya Mashariki.

Lakini pia ukiwa Wilaya ya Itilima Kuna eneo Linaitwa Gambasingu ambalo linahusishwa na kuishi Kwa Wataturu maeneo hayo. Wataturu waliozamia Usukumani Walifanya baadhi Yao kuoleana na Wasukuma na ndiyo maana ukiwa Bariadi Kuna Wasukuma wana maumbile ya kitaturu na kimasai kabisa.

Lakini pia Kuna tambiko la KANUDA linalohusishwa na Wamasai nafikiri Wasukuma wa Bariadi Wanafahamu namna Tambiko Hilo linavyofanyika, na Wasukuma wengi wa Bariadi Wana majina ya KANUDA.

pia Wana majina ya kitaturu kama vile, Singu, Magina, Sugilo, Lagu, Gamawishi, Wishi au Weshi nk. Hii inaonesha wazi kuwa Kuna mahusiano ya Karibu kati ya Wasukuma na Wataturu na Wamasai.

Wasukuma -Banantuzu ni moja ya Wasukuma maarufu walioshiriki katika kufuata biashara ya chumvi ya Nyaraja Mkoani manyara ambapo huko walikutana na Makabila ya kutoka Singida kama vile Wanyiramba na Wanyisanzu pia Wanyaturu na kuanzisha mahusiano ya kuoleana, ambapo Wasukuma walipendezwa na wanawake weupe kutokea Kwa Makabila hayo.

dhahiri kuwa asili ya Wasukuma wa ukoo wa Babungu ni makabila ya Wabungu na Wanyiramba.
NB; Msukuma kwa mwanamke mweupe humwambii kitu ,sura sio shida zao wao ni weupe tu basi 😁
Source; Bujora sukuma historical site
kuna baadh ya v2 umeweka sawa lakin kuna v2 sizan kama uko sawa any way mawazo yako
 
si kweli kjana wasukuma wana roho nzuri japo huenda ulikosewa na mmoja ko unawaon ote wako vile na siku zote mtu aliye kosewa humuona yoyote apitae mbele yake pia nae ni mkosaji 2
Ni kweli kuna jamii za kisukuma ziko poa sana wana roho nzuri.

Ila kwa wanyantuzu nakukatalia.

Hao wana uchoyo roho mbaya na uchawi wa kufa mtu.

Wachache sana kwenye jamii za kinyantuzu ndo wako poa.
 
kwa uchawi hapo sawa maaa hdi wazir alisema mkandarasi kashindwa kufanya kaz coz ikifika usiku mabomba huwa yanapaaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom