Asili mia moja kutengwa kwa Utafiti. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asili mia moja kutengwa kwa Utafiti.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Feb 21, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametamka kwamba asili mia moja ya budget ya mwaka ujao itatengwa kwa ajili ya Utafiti. Ni kipiga hesabu za haraka haraka ni kwamba kama budget ya serikali mwaka ujao wa fedha itakuwa Trillion nne, basi utafiti watapata Billion40. Saa hivi wanapata pesa isiyozidi Mil.400 kwa mwaka! Na katika hizi ni fedha kidogo sana zinazo wafikia watafiti,tena for maintenance purposes only.Sio kufanya utafiti. Nampongeza sana Kikwete kwa maono haya, kama yatatekelezwa.

  Mara nyingi tumesema kwamba utafiti ndio moyo wa nchi,na nchi isiyofanya utafiti, imekufa.Hata hivyo katika kipindi cha kama miaka 20 hivi iliyopita, tulishuhudia developments ambazo zilikuwa hazipendezi hata kidogo. Tanzania sijui ilikumbwa na pepo gani ikadhani kwamba inaweza kufanya utafiti wake kwa kutumia hela za wafadhili, ambao kusema kweli ni matapeli tu.Hawa ajenda yao kubwa ni kuifanya Tanzania iwe tegemezi. Tanzania ina rasilimali nyingi na hakuna sababu yeyote kwa nini itegemee wafadhili kwa utafiti wake.

  Katika kipindi hicho cha miaka ishirini katika hali ya kushangaza kabisa, viongozi waandamizi wa serikali, ambao mpaka leo nimeshindwa kuelewa wanatoka sayari gani, ilifika mahali hata wakashawishi watafiti kwamba wao wenyewe waombe mashirika ya nje fedha ili waweza kufanya utafiti, literally making them beggers! Katika hali hii, unategemea nini, kama sio kuwafanya wataalam wako kuwa mamluki? Kwakweli tulidhalilika sana. Wengi bila kujua waliishia ku-save intersts za wafadhili, ambazo ni tofauti kabisa na interests za nchi yetu. Mambo ya ajabu yamefanywa na watafiti katika kipindi hicho cha ujima ili kuganga njaa! Na nchi imeingizwa mkenge katika kiwango cha kutisha sana. Mungu aepushie mbali. Hakuna asiyejua kwamba nia ya nchi za magharibu ni kutufanya tuwe omba omba milele. Anayedhani wazungu wana nia ya kweli ya kutuendeleza is scrap!

  Nirudie tena kwa dhati kabisa kumpongeza Kikwete, lakini naomba kutoa words of caution. Bado mafisadi wamejaa kila mahali, na upo mtandao wa Freemasons ambao nia yake ni kuharibu kila lililo jema kwa kuhamasisha maovu, ikiwa ni pamoja na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma. Siwaogopi ingawa najua wana nguvu nyingi za kishetani na kifedha. Kama tunataka tufanikiwe ni lazima tuutokomeze mtandao huu nchini. Vinginevyo tutakuwa na nia njema kabisa lakini hatutafika popote. Nakumbuka Mwalimu alipiga vita sana mtandao huu, na katika uongozi wake walijichimbia chini. Sasa bila aibu wameibuka na wanafanya kazi zao kwa uwazi kabisa. Wengi tunajua hata ofisi/hekalu lao lilipo sina haya ya kusema.

  Pia hatuna budi kuhakikisha kwamba fedha zitakazotengwa kwa ajili ya utafiti zinawafikia walengwa. Mfumo uliopo sasa una kasoro nyingi mno, na kama utaendelea matatizo yatakuwa yale yale.Napenda nitoe ushauri kidogo kama ifuatavyo:

  *Mfumo ulioko sasa hautoi nafasi kwa mtafiti kufanya budget ya kazi zake, badala yake hupewa chochote kilichopo! Na mara nyingi hakuna au ni kidogo sana, kwa hiyo hakuna utafiti. Nashauri kila mtafiti afanye budget ya miradi yake na kuitetea katika vikao husika.

  *Monitoring and evaluation,kama fedha kweli zitakuwepo, ifanyike vigorously ili kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

  *Ziwepo checks and balances ili kuhakikisha kwamba hakuna upendeleo wa aina yeyote katika ku-award projects.

  *Mazingira ya kufanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vitendea kazi kwa watafiti kwa ujumla yaboreshwe. Tusitegemee mtafiti kufanya kazi ya maana bila vifaa na kama ofisi yake na hata nyumbani kwake wakati wa mvua kunavuja, nyumba au ofisi haijapigwa rangi kwa miaka ishirini iliyopita, nyufa zimejaa tele, milango na madirisha vimebomoka nk. Hatuna budi kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vifaa husika kama tunataka kweli wawe productive in terms of utoaji wa appropriate technologies.

  *Mwisho nisisitize kwamba hata kama kungekuwa na fedha ya kufanyia kazi nyingi kiasi gani, na mazingingira mazuri kiasi gani,kama mishahara ya watafiti ni midogo kiasi kwamba hawawezi kutekeleza majukumu yao ya msingi katika familia zao, yote yatakuwa ni bure! Ni vema basi kuwepo kwa fedha ya kufanyia kazi na mazingira mazuri kuende sambamba na uboreshwaji wa maslahi yao.
   
  Last edited: Feb 21, 2009
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Nami nichukue nafasi hii kumpongeza JK...he should have taken steps mapema zaidi!

  Ulimaanisha 40 bilions au 400 Miliions hutolewa sasa?

  Nadhani serikali hutoa zaidi ya 50 billions ukiangalia upana wa utafiti kwa nchi...fikiria Utafiti wa COSTECH, TAFIRI, TRIDO, NIMR, Misitu, Kilimo n.k na pia Vyuo vikuu..serikali hulipia mishahara na running costs za maabara na other overheads!

  This is a credit kwa serikali..sema pesa za kufanya utafiti nyingi zinatoka kwa miradi toka nje..hili nakubaliana nalo kuwa pesa ya kufanya utafiti iongezwe!

  Ni ukweli kuwa ukilinganisha na nchi zingine zinazotuzunguka...haswa ukiangalia machapisho ya kisayansi Tz hatuko nyuma kiasi hicho!

  Hope this JK move itafanya Tz tufanye vema zaidi
   
 3. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwakweli hili jambo jema JK hongera,

  kazi kwao watafiti je wapo tayari kutumia kiasi hicho kwa ajili ya kufanya tafiti zenye faida kwa maendeleo ya taifa, kuendana na mazingira na hali halisi ya wananchi!

  isije ikawa hizi pesa zikaishia kujenga maghorofa ya project coordinators na kuwaacha wahangaikaji, wakusanyaji data, wakifanya kazi katika mazingira magumu ya kutokuwa na vifaa na pengine hata usafiri duni wakiambiwa bajeti ni ndogo!! wakati magari ya project yakitumika kuendea sokoni! na huku maabara zetu zikiwa hazina hata vitendea kazi! na taasisi zetu kukosa hata komputa!

  haya tunayaona katika taasisi zetu pesa za utafiti zinakuwa ni kwa ajili ya kuwanufaisha wakubwa ambao si watendaji wao hukaa ofisini na kupambana kuandika ripoti zisizokuwa na manufaa kwa taifa huku wakiwapigia kelele watu wa chini wawaletee taarifa bila ya kuwawezesha ipasavyo! FISADI wapo kila pahala, napo huku kwenye utafiti wamulikwe COSTECH, TAFIRI; NEMC; TAASISI ZA ELIMU YA JUU, NK

  kwa mfano, binafsi huwa najiuliza sana kuna kitengo cha tiba asilia pale Muhimbili kina fanya tafiti sana na kinapata pesa nyingi kwa ajili ya kuendeleza tafiti hizo, je tafiti zinafanyika itakiwavyo, nini matokeo yake na mnaufaa kwa umma, je hizo information huwa zinafanyiwa kazi ipasavyo! kwa mfano tafiti za dawa za ukimwi, kifafa etc,

  kuna taasisi kwakweli naziamini katika suala zima la utafiti na uwezeshaji vifaa etc, lakini taasisi nyingine niwasanii na pesa huishia kuinua maghorofa na kununua magari ya kifahari,
  Hope uwazi uliopo sasa kuwaanika mafisadi ingawa hatujaona wakihukumiwa unaweza kuwaogofya na hizo pesa kutumika kuleta mafanikio kwa taifa!!
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hivi ni kwa nini wengi hawachangii ktk mada za kisayansi..na Elimu?

  JF siasa zaidi ndo watu hupenda?
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Monitoring and Evaluation ktk utafiti vipi?

  Manake wazungu kibao tunao hapa na vibali vya utafiti..na sijui hata kuna mtu anafuatilia wanachokifanya!
   
 6. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hata mauzo ya vogue, cosmo and the like yanashinda time, news week, scientist and the like... trivia is more appealing especially to lazy/tired minds
   
 7. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  nadhani ni uamuzi mzuri baada ya kilio cha siku nyingi cha watafiti(ni Jk kweli kasema? bado siamini source pls!!), bado ni kidogo, lakini ni lazima tuwe na sehemu ya kuanzia, kwa sasa sio mbaya. Ni vyema pia tukaangalia matumizi ya fedha hizo yasije yakaingiliana na siasa, ni kama watu kutenga fedha ambazo wameshazitungia namna ya kuzifuata. Hakuna nchi yoyote iliyoendelea bila kuwa na utafiti wake unaojitegemea. Siku zote hawa mamluki hawaji kufanya utafiti wa kimaendeleo au endelevu, wanakuja na ajenda zao na ili kupata fedha zao ni lazima utafiti wako uendane na ajenda zao. Natumaini watafiti watajikita katika mambo muhimu ya kuweza kutatua matatizo yanayowakabili watanzania.
   
 8. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Tafadhali tupe source ya habari hii!!!
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Source Mkutano JK na Wakuu wa Wizara, COSTECH n.k karibuni,,je wazee huwa hamsomi hata magazeti?
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mzalendo original, ni jambo la kusikitisha sana kuwa hii ni tabia iliyokomaa katika jamii na hata idara mbali mbali za serikali.
  Scientific analysis inachukuliwa kama luxury that we cannot afford.Mambo yakienda ovyo kila mtu anapenda kulalama.
  Siasa ndio mchezo unaopendwa sana na kila mtu aliyepewa mdomo na Mungu.
  Mambo mengi yanaendeshwa hovyo kwa kukosa utafiti wa ki sayansi anu hata utafiti tu kwa ujumla ili kufafanua matatizo au mwenendo wa masuala ya kijamii.
  Jivyo basi bila kuwa na silaha ya utafiti hata solutions hazina maana kwani hazina information back up.
  Kwa kuongeza fungu la utafiti hii ni thumbs up kwa JK and co.
   
 11. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Tikerra umelonga, watafiti wapo lakini wapi watapata fedha za kufanyia tafiti zao imekuwa ni kazi. Kama mapendekezo yako namba 1-3 yakifanyiwa kazi tunaweza kuwakwamua watafiti, na tafiti zao zikalisaidia Taifa katika maendeleo. Nyingi ya hizi research institutions (TAWIRI, TAFORI, NIMR, NEMC, TPRI nk) fedha nyingi za utafiti kama walivyosema wachangiaji waliopita hutoka katika miradi inayofadhiliwa na watu wa nje. Kuhusu mishahara nina jamaa yangu yuko TPRI, aliwahi kuniambia kuanzia mwaka juzi mwezi wa saba, mishahara yote ya watafiti inapangwa na COSTECH, hivyo imeboreshwa kwa kiasi cha kuridhisha.

  Watafiti nao wanajitahidi kuandika proposal kutafuta fedha kupitia source mbalimbali. Lakini hili la serikali kutenga 1% ya budget kweli ni hatua nzuri sana. Sasa zitumike tu kwa maeneo yaliyopangwa, na isije ikawa asilimia kubwa zinatumika kwa mikutano, warsha nk badala ya kwanza kufanya tafiti zilizokusudiwa.
   
 12. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa hili JK anastahili pongezi. Kumekuwa na kilio cha muda mrefu kuyataka mataifa yanayoendelea na hasa ya Afrika kutenga budget yake kufikia 1% ielekezwe kwenye tafiti bila mafanikio. Naona hili huenda likafanikiwa kama JK alivyoahidi. Kwa muda mrefu pamoja na kuwa serikali imekuwa ikiwalipa mishahara watafiti wake lakini wamekuwa wakienda bila fedha za utafiti, kiasi kwamba walibaki kuwa kama misukule wa mashirika ya ulaya, ilifikia mahali watu wanafanya kazi ilimradi wapate tu fedha kwa kuwa hawana jinsi. Tafiti nyingi zilikuwa zinalenge tu kutimiza matakwa ya wafadhili na hakika sio kwa manufaa ya Watanzania, kwani kama wao nia yao ni kujifunza kwanza juu ya virusi vya ukimwi, kuambukiza watu wakaona jinsi wanavyopata na kuugua ugonjwa sio tatizo kama ilivyofanyika kule Libya (Lakini kwetu nadhani haiukutokea) japokuwa yalifanyika majaribio ya chanjo ambayo haikuidhinishwa na tume ya maadili ya tiba Tanzania huko Lugalo na kwingineko. Haya yote yanatokana na kukosekana kwa fedha na watu wachache wanalazimika kutumika wanatumika vibaya.

  Huu unaweza kuwa mwano mzuri wa taifa kuanza kujenga misingi yake baaada ya kipindi kirefu cha kuamini kuwa wazungu watalutea maendeleo.

  Ni ukweli usiofichika, ni vigumu Wazungu kukubali waafrika wakaendelea, unadhani nani angependa kukaa ulaya kama shida na maradhi ya afrika yangekwisha? Afika mtu unadunda siku 365 za mwaka, ulaya ni kipindi cha sijui kiangazi (summer kama sikukosea kama siku 120).

  Tuipende nchi yetu na tuwajibike kwa maendeleo yake. Tuchukie ufisadi na kila mtu asimame katika nafasi yake. Mtawala afanye kazi yake, mtafiti kazi yake, na mwanasiasa asimame kweli katika siasa kwa masilahi ya taifa na sio kwa maslahi ya mitandao na mengine yaliyoifikisha Tanzania hapa ilipo.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
Loading...