Asasi za kiraia zailalamikia CCM kauli zilizotolewa na UVCCM

Asasi za kiraia zailalamikia CCM kauli zilizotolewa na UVCCM

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa, ameeleza kusikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), akisema zinadhoofisha jitihada za Asasi za Kiraia katika kuchangia maendeleo ya taifa.

"Tumeona baadhi ya viongozi wa UVCCM wakizungumzia vibaya kazi za Asasi za Kiraia na NGOs, jambo ambalo linakatisha tamaa. Sisi tuna mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu. Kauli ya kiongozi mkubwa kusema kuwa Asasi za Kiraia zinaandaa magaidi ni jambo linaloweza kueleweka vibaya na jamii,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa ametoa kauli hiyo Aprili 30, 2025, katika Ukumbi wa Makao makuu ya CCM White House jijini Dodoma, wakati wa kikao na mashirika yasiyo ya kiserikali(NG'OS) na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg.

Rabia Abdalla Hamid. Kikao hicho kililenga kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili watoa huduma kutoka sekta ya utetezi wa haki za binadamu.Kauli hizo zinakuja kufuatia matamshi ya Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida, akiwa Bukombe mkoani Geita alidai kuwa ana taarifa za baadhi ya asasi na vyama vya siasa vinavyowapeleka vijana nje ya nchi kwa mafunzo yanayolenga kuandaa vurugu na machafuko.

“Ilani ya CCM inazitambua Asasi za Kiraia, NGOs, haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Kwa hiyo sisi hatufanyi kazi kinyume na maadili ya taifa wala chama. Tunapokuja kukumbusha utekelezaji wa ilani hiyo, tunafanya hivyo kwa nia njema,” ameongeza Olengurumwa.

Aidha, amelalamikia vikwazo wanavyokumbana navyo wanapojaribu kutoa huduma kwa wananchi, akisema bado kuna hiyana na kutokuelewa kwa baadhi ya viongozi kuhusu kazi ya utetezi wa haki za binadamu.

Kwa upande wake, Katibu wa NEC wa CCM anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, ameomba radhi kwa niaba ya chama kwa kauli zilizotolewa dhidi ya Asasi za Kiraia. Amesisitiza kuwa hiyo si tabia inayofundishwa ndani ya chama, na kutoa wito kwa viongozi wa UVCCM kuwa waangalifu na matamshi yao kwa jamii.

 
Back
Top Bottom