Kuna thread iliwahi kuwekwa hapa namna ya kujua kama mpenzi wako anakucheat,
Nilifuatilia namna ilivyochangiwa na watu wengi walitoa michango yao kwa namna wanavyofahamu,
uamuzi niliochukua ni kufanyia kazi yale niliyoyapata cz na mimi nilikuwa mmojawapo wa wanaohic kama wanadanganywa katika mapenzi,nilihic hivo baada ya kuona mpenz wangu amebadilika kwa kila kitu,hakuna anachonisikiliza sikupata jibu,kuna siku niliamua kumwita sehem na kujaribu kumweka sawa y ananifanyia hivo,hakuna alichojibu zaidi ya kusema atajirekebisha,cha ajabu nkaona kama anazidi sasa,nilichofanya nilimwita tena nkaziomba sim zake zote mbili,hapo ukawa ugomvi mkubwa sana kwann nakagua simu zake
Nilifanikiwa kunyang'aanya sim moja nkaangalia text,nilichokikuta Mungu anajua nilipomwuliza akadai ni zafiki zake tu wa kawaida,niliingiza namba zangu za simu kwenye cm yake nkajipigia nkaona amenisave jina la kike,utetezi wake haukuniridhisha,niliamua kuvunja simu zote mbili kwa hasira
Kesho yake asubuhi niliamua kununua sim nkadownload ile kitu mspy,nikampelekea na kumwomba msamaha kwa yaliyotokea nkanyamaza,
Nikaendelea kumchunguza kama kuna mtu ana mahusiano nae,kweli nilianza kuona yale mawasiliano,nikayakusanya kama yalivo,baada ya siku nne niliamua kumwambia ukweli wote na kumwonesha text zote na sim alizopigiwa,hakuweza kuamini kitendo kile lakini ndo ulikuwa ukweli wenyewe,hakuweza kukataa tena alikiri kuwa ni kweli ana mahusiano na huyo kijana mwingne,
Uamuzi wangu niliochukua nilimwambia sihitaji tena mahusiano kati yangu na yeye,
Alilia sana na kuomba msamaha lakin kiukweli moyo wangu umeshamtoa kabisa tena simhitaji,
Kpaka hivi sasa anajitahidi kuomba msamaha na kuahidi kwamba hata niumiza tena,lakin hofu yangu naona atarudia tu na sitaki kupata presha tena za namna hii
Shukrani sana kwa aliytoa ile thread kweli jf ni kila kitu.
Asanteni