Asante Wenger umekumbuka kutuachia Aubameyang na Mkhitaryan

Dkileo

Member
May 23, 2017
51
46
Miaka 22 iliyopita profesa kutoka ufaransa aliwasisli London kuwa manager wa moja ya timu kubwa London..Ilikuwa september 1996 ambapo Arsenal ilimtangaza Wenger kuwa kocha wao na alianza kazi 1 october 1996 ..Nilikuwepo duniani japo sikuwa na uwezo wa kutambua yaliyokuwa yanaendelea..


Baada ya miaka 22 profesa ameamua kuachia nafasi yake kama kocha..Atakumbukwa Zaidi kwa kuihamisha Arsenal kutoka Highbury mpaka Emirates.. Ni moja kati ya mafanikio makubwa ya Wenger ambapo anaiacha Arsenal ikiwa salama pasipo madeni pamoja na uwanja mkubwa kabisa wenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 59000


Wenger amefanya mengi sana ndani ya Arsenal ..Lakini mashabiki wengi wanamkumbuka katika msimu wa 2003-2004 ambapo alicheza msimu mzima wa ligi kuu uingereza bila kupoteza mechi hata moja”The Invincible”..Katika msimu huo Wenger alikuwa na wachezaji imara sana…

Kulikuwa na watu kama James Lehman,Sol Campell,Ashley Cole,Martin Keown,Kolo Toure,Gilberto Silva, Freddie Ljungberg,Robert Pires,Patrick Vieira,Nwankwo Kanu,Denis Bergkamp na Thierry Hennry..Pia kulikuwa na vijana kama Fabregas,Fellipe Senderos na Gael Clichy..


Ukiangalia kikosi hicho unaweza kuona jinsi ambavyo Wenger alitengeneza timu imara sana iliyokuwa chini ya mikono salama ya Hennry na Bergkamp..Baada ya msimu wa huo msimu ulio fuata Arsenal ilichukua taji la FA cup ambapo fainali walicheza dhidi ya Man United..Wengi tutakumbuka fainali hii kama fainali ya Roy Keane na Patrick Vieira…

Tokea hapo Wenger aliweza kucheza misimu 9 bila taji lolote ndani na nje ya ligi kuu Uingereza..Msimu wa 2013-2014 Wenger aliweza kushinda taji la FA cup na kuweza kumaliza ukame wa misimu 9


Mwaka 2003-2004 mpaka 2017-20018 anatangaza kuondoka Wenger hajachukua taji la ligi kuu Uingereza..Ni takribani misimu 14 sasa…Na hapa ndipo mahali ambapo hata mashabiki wa Arsenal walishindwa kumvumilia huku bodi ya Arsenal ikiendelea kumuamini kwakua japo hakuwa na matokeo mazuri ndani ya uwanja lakini nje ya uwanja Arsenal ilikuwa imara sana kiuchumi..


katika kipindi hiki kigumu Arsene aliuza wachezaji wengi imara..Aliondoka Ashley cole kwenda Chelsea kwa utata.. Alexander Hleb kwenda barca pia Hennry nae alikwenda barca.. Kolo toure naye alikwenda Man city..

Pia vijana kama Fabregas,Adebayor na Clichy ambao walipewa nafasi kubwa na wenger waliondoka..Wakaja kina Samir Nasri nao wakaondoka..Bila kumsahau Robin Van Persie aliekwenda Man United.. Katika kipindi hiki hiki kigumu Wenger alikitumia kwa umakini ili kuweza kuwachukua wachezaji vijana na kuwakuza na kuwauza kwa bei nzuri ili kuweza kulipa deni la mkopo walilotumia kujenga uwanja wa Emirates..Na katika hilo alifanikiwa sana


Baadhi vijana wengine walio pewa nafasi na wenger japo hawakufikia azimio ni Niklas Bendtner,Denilson na Abou Diaby..Pia kuna vijana ambao wameendelea kuwepo mpaka leo ndani ya Arsenal Jack Wilshere,Aaron Ramsey na Laurent kocienly..Huku Theo Walcot,Chamberlain na Kieran Gibbs wakiondoka zao





Katika kipindi cha miaka ya karibuni ni kama Wenger aliona mwisho wa maisha yake ndani ya Arsenal..Nadhani hii ilitokana na shutuma nyingi kutoka kwa mashabiki..Na wenger aliamua kubadili mfumo na kuamua kutumia pesa


Mwezi September 2013 arsenal ilimsajili Ozil kutoka Real Madrid kwa £42.5 million….Msimu mmoja baadae mwezi July wenger alitoa £31.7 kumsajili Alexis Sanchez kuto Barca…Aliendelea kutuletea wachezaji kama Gabriel paulista,Shkodran Mustafi,Granit Xhaka,Welbeck nahata Lacazette..



Ila majira ya baridi msimu huu Wenger amelamba dume pamoja na kumpoteza mwanaume mmoja mpambanaji sana…Wenger alikubali kumpoteza Alexis Sanchez(kama alivyompoteza Van Persie) ambaye alikuwa ni kama roho ya Arsenal na yeye kupata mchezaji mmoja hatari sana Mkhitaryan



Wengi walimuona Mikhi kama mchezaji wa kawaida baada ya kutokuwa na msimu mzuri chini ya Mourinho lakini Mikhi ametuonyesha kwamba anafunga na kutoa assist katika kipindi hiki cha nusu ya mwisho ya msimu…



Kikubwa Zaidi ni usajili wa Aubameyang..Usajili huu ndio umeonesha tija Zaidi..Pierre amefunga magoli 10 EPL katika nusu msimu..Anaonekana ni hatari Zaidi huku yeye na Mikhi wakikumushia combination yao ya BVB

Kwa upande wangu wenger ameacha timu yenye wachezaji imara sana …Arsenal iko imara ila inakosa kikosi kipana tuu..Ukiangali kuna maeneo hayana mpinzani..Hector Bellerin hana mpinzani..Xhaka hana mpinzani..

Mwalimu atakaye kuja atahitaji kuongeza namba ya wachezaji waliokomaa kwenye kikosi ili kuleta ushindani kikosini…



Naiwazia Arsenal ya msimu ujao ya Mikhi+Ozil+Aubameyang bila kumsahau Lacazette



“thanks for the memories Arsene..always in our hearts”
 
msimu ujao lazima turudi kwe nafasi yetu ya nne huo ndo ubingwa wetu, lazima tufuzu champions league twende kushikana mikono na kina messi na ronaldo
 
Duh! Nyie wanaArsenal hebu acheni unafiki aisee, yani kutoka "wenger must leave" mpaka "always in our hearts" Sasa na kwa taarifa yenu kashahairisha kuondoka kasema alikuwa anawabeep tu .
 
Duh! Nyie wanaArsenal hebu acheni unafiki aisee, yani kutoka "wenger must leave" mpaka "always in our hearts" Sasa na kwa taarifa yenu kashahairisha kuondoka kasema alikuwa anawabeep tu .
nadhani akiahirisha kusepa kuna watu wengi wa Arsenal watakufa kwa pressure
 
msimu ujao lazima turudi kwe nafasi yetu ya nne huo ndo ubingwa wetu, lazima tufuzu champions league twende kushikana mikono na kina messi na ronaldo
mnashuka daraja amini nakuambia jiandae kwenda kucheza na bristol city na fulham
 
hakuna anaye faham mkuu..ngojea tuone kina ivan gazidis watakuja na jina gan

IMG_20180519_012253.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom