Asante speaker Ndugai japo kuwasemea watumishi wa umma

Asante speaker Ndugai japo kuwasemea watumishi wa umma

Tairi bovu

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
3,063
Reaction score
2,991
Pamekuwa na unyanyasani mkubwa kwa watumishi wa umma tangu awamu hii iingie madarakani. mtumishi amekuwa kama kikaragosi. Kwanza aliambiwa pasingekuwa na nyongeza ya mishahara wala kupandishwa madaraja hadi uhakiki uishe kakubali.

Baada ya uhakiki akambiwa hadi uzalishaji uongezeke akakubali.Tena uhakiki unaendelea tena hakuna nyongeza ya mshahara wala kupandishwa tena japo ni kwa mujibu wa sheria!? tunaambiwa Sheria kitu gani bwana tena mbele ya mandege, madaraja, umeme na mirel ya umeme?

Leo waziri yule anayehudumu TAMISEMI ameulizwa swali bungeni. Kama kuwafanya watumishi taahira wasio na kumbukumbu anawatupia lawama maafisa utumishi ati hawapeleki taarifa kwa wakati. Kwa bahati Ndugai amestuka kwamba majibu ya yule waziri ni ya kiubabaishaji! ama kwa kuwa anaogopa au hana kumbukumbu na alichokisema kasahau, kavimbiwa anabeua.

Nimkumbushe ndugu waziri taarifa za watumishi zipo kwenye mfumo Lawson.Huhitajiki tena kupeleka makaratasi ya taarifa za watumishi Dodoma au Ikulu zipo kwenye mfumo. Kuwatupia lawama ma HR ni kuudanganya umma na hao watumishi wenyewe!

Ikumbukwe kuwa motisha kwa watumishi ni sehemu muhimu ya huo uchumi wa viwanda. Mishahara ni suala la kisheria hulipwa kisheria wala sio hisani kama kugawa maburungutu ya noti kwenye misafara yetu hapana,gharama za maisha zinapanda kila siku nanyi mwajua.

Waziri yule ameambiwa wiki ijayo aje na majibu akajipange asipotoshe wala asijibu bora liende.

Asante bwana Ndugai kuwasemea watumishi japo wenyewe wamelala usingizi tena wa pono!
 
Anastahili pongezi kwa kile alichokifanya, ingawa kwa hulka na tamaduni zao usitarajie lolote la maana.

Tarajia jibu jingine la kisanii saniii then maisha yataendelea.
 
hao. wanaoitwa watumishi kama wapo. wanajua mimachoendlea kweli
 
Sisi hatuhitaji majibu mazuri, Tunahitaji Matokeo au utekelezaji wa madai ya watumishi. Majibu mazuri yatatusaidia nini watumishi, hata wasingetuambia wanafanya nini, lakini wakitupandisha madaraja na kutulipa stahiki zetu zote, kwa kipindi chote walicho tuahidi tuta washukuru.
 
Ni sinema inachezwa. Mwakani watumishi wa umma wataongezwa madaraja na mishahara na 2020 watasahau machungu yote nwataichagua ccm.
 
hao. wanaoitwa watumishi kama wapo. wanajua mimachoendlea kweli

Kwa hili nampongeza Mh. Spika angalau kwa kuonesha kuwa lipo tatizo. Watumishi wengi wa umma wanakabiliwa na tatizo la kutopanda madaraja. Sababu mojawapo ni uzembe wa baadhi ya maafisa utumishi na rushwa. Ukitaka kupanda cheo lazima utoe rushwa (pesa, mali ngono n.k) hata kama huna vigezo utaandikiwa nyaraka zote muhimu na sahihi zitafojiwa ili kuonesha unavyo vigezo halali vya kupanda cheo. Walioweza kutoa rushwa walipandishwa vyeo na wasioweza waliendelea kubaki katika madaraja yao. Uwezo mdogo (incompetency) wa baadhi ya maafisa utumishi katika kutatua changamoto za kiutumishi ni sababu nyingine. Baadhi ya issue ndogo ndogo zinashindwa kufanyiwa kazi kwa wakati. Ndio maana leo hatushangai kuona watumishi wengi walioajiriwa mwaka mmoja tena katika nafasi moja, kituo kimoja cha kazi lakini wakatofautiana viwango cha mshahara. Simaanishi wale ambao walipata uteuzi wa kushika nafasi za ukuu wa idara. Naongelea wale watumishi tu wa kawaida.

Serikali nayo inahusika kutokana na uwepo wa baadhi ya Sheria, Kanuni na Taratibu kandamizi. Nitatoa mfano mmoja wa Waraka wa kubadilisha kada watumishi wa umma wa tarehe 01/12/2009. Huu ni mojawapo ya nyaraka kandamizi kwa watumishi wa umma. Waraka huu unaelekeza taratibu za kubadilisha kada kwa watumishi wa umma waliojiendeleza katika nafasi tofauti na zile walizokuwa wakizifanyia kazi. Waraka unaelekeza kwamba mtumishi anayehama kada moja kwenda nyingine lazima akaanze na mshahara wa kuanzia katika kada husika. Kwa maana nyingine ni kwamba, mtumishi aliyekuwa na mshahara mkubwa lazima ashuke na kuanza na mshahara wa mwajiriwa mpya. Sababu kubwa inayotolewa ni kwamba majukumu ambayo mtumishi anakwenda kuyatekeleza ni mapya na hivyo ni sawa na mwajiriwa mpya kwenye nafasi hiyo. Hilo siyo tatizo, naweza kukubaliana nalo. Tatizo linakuja kwa mtumishi ambaye anabadilisha kada siyo kwasababu amejiendeleza katika nafasi tofauti na ile aliyokuwa nayo awali bali ni kutokana na kutokuwepo kwa muundo wa kada yake ya utumishi lakini alikuwa akitekeleza majukumu ya nafasi hiyo kwa maelekezo ya Serikali. Nitatoa mfano mmojawapo wa watumishi waliokandamizwa na waraka huu.

Watumishi wanaoathirika zaidi katika hali hii ni maafisa Mazingira hususani katika ngazi za halmashauri. Ikumbukwe kuwa vyuo vikuu nchini Tanzania vilianza kuzalisha wataalamu wa Mazingira kuanzia miaka ya 2000. Hata hivyo, serikali ilianzisha ikama (scheme of service) ya maafisa mazingira tarehe 08/07/2011 takribani miaka 7 baada ya kutungwa kwa Sheria ya Taifa ya Uhifadhi wa Mazingira ya mwaka 2004. Sheria hii iliweka muundo wa usimamizi wa mazingira nchini ikiwemo; kuwa na wataalamu wa Mazingira katika ngazi zote za utawala. Hata hivyo, Serikali haikuweza kuanzisha ikama hiyo hadi mwaka 2011. Hivyo, wataalamu hawa iliwabidi kuajiriwa katika nafasi zingine zenye majukumu yanayofanana na taaluma yao. Wengi waliajiriwa kama maafisa misitu. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa changamoto za uharibifu wa mazingira nchini, pamoja na kutokuwepo kwa ikama hii kwa kipindi hicho, Serikali iliona umuhimu wa kuwa na wataalamu hawa katika mamlaka zake. Ndipo tarehe15/04/2008 ilipochukua maamuzi ya kuzitaka mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini kuajiri ama kuteua watumishi wenye sifa za kielimu ili kusimamia maswala ya uhifadhi wa mazingira katika maeneo yao.

Wengi walioteuliwa ni wale watumishi waliokuwa na Shahada ya Mazingira lakini waliokuwa wameajiriwa katika nafasi mbalimbali kama vile afisa misitu. Baada ya uteuzi huo, watumishi hao walianza kufanya shughuli za usimamizi wa mazingira kuanzia wakati huo. Tatizo linakuja hapa. Baada ya ikama ya maafisa mazingira kutolewa rasmi na Serikali mwaka 2011, baadhi ya watumishi hawa walianza kuomba watambuliwe kimfumo kuwa wao ni maafisa mazingira badala ya kuendelea kutambulika kwa kada zao za awali wakati hawatekelezi majukumu ya nafasi hizo. Kwa mfano, badala ya kumbukumbu za mtumishi X kuonesha ni afisa misitu basi zioneshe kuwa yeye ni Afisa Mazingira. Mabadiliko hayo pia yasiathiri kiwango chake chake cha mshahara kwasababu mtumishi huyu alishakuwa akitimiza majukumu ya afisa mazingira toka mwaka 2008 alivyoteuliwa kutokana na maagizo ya Serikali. Tatizo ndio linakuja hapo.

Waraka huu unaliweka hili kundi pamoja na makundi ya watumishi wanaobadilisha kada kutokana na kujiendeleza katika nyanja tofauti na zile walizokuwa wakizifanyia kazi. Kimsingi waraka huu haulihusu kabisa kundi hili la watumishi. Lakini maafisa utumishi wameendelea kuutumia waraka huu na kulazimisha watumishi hawa kushushwa viwango vyao vya mishahara kana kwamba nao wanabadilisha kutoka kada moja kwenda kada nyingine mpya. Hawa ni watumishi ambao waliteuliwa kwa agizo la Serikali kufanya shughuli za usimamizi wa mazingira kutokana na kutokuwepo kwa muundo wa kada hiyo kwa wakati huo. Sasa tujiulize kwanini watumishi hawa wanashushwa viwango vyao vya mshahara wanapoomba kurekebishwa kimfumo ili watambulike kama maafisa mazingira kwenye nyaraka za utumishi badala ya kuendelea kutambulika kwa nafasi zao za awali ambazo hawatekelezi tena majukumu yake?. Wengi wa watumsihi hawa wameitumikia Serikali ya Jamhuri ya Muungani kwa zaidi ya miaka 10 lakini sasa waraka huu umewalazimisha kushushwa kwa viwango vyao vya mshahara na sasa wanapokea mshahara wa mwajiriwa mpya (yaani Tshs 710,000).

Hivyo, Mheshimiwa Spika huu waraka hauna budi kuangaliwa upya. Na hili kundi la maafisa Mazingira walioathirika kutokana na waraka huu waangaliwe. Hii siyo sawa, ni uonevu na inakatisha tamaa.
 
Ndungai hongera sana kwa kuwasemea Watumishi usiwe kama wakina Mkuchika kila siku wanasema uhakiki haujaisha lengo in kujificha kwenye Kichaka cha Uhakiki ili wasiwaongeze watumishi mishahara na Kupanda Vyeo. Serikali hihi hi ilifanya Uhakiki zaidi ya Mwaka mmoja na kutoa majibu Leo hii wanasema bado kuna watumishi Feki eti wanataka kufanya Uhakiki Upya mmmmhhh hamuoni aibuuuu? Kwa ufupi tangu serikali hii iingie Madarakani hakuna Mtumishi aliyepanda Cheo, hao watumishi 59,000 waliopanda vyeo walikuwa ni bajeti ya Mzee Kikwete iliyoandaliwa desemba 2014 kwa ajili ya kuwapandisha watumishi mwaka 2015/2016. Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya watumishi wanaotakiwa kupanda vyeo hata takwimu alizotoa Naibu Waziri Wa TAMISEMI bungeni Leo zilikuwa za Uongo kwani Watumishi waliopandishwa Vyeo 2012/2013 mpaka Leo hawajapandishwa Vyeo. 2012/2013, 2013/2014, 2014/2015, 2015/2017, 2016/2017 na sasa tunaenda 2017/2018 hawa wote wanasifa za kupanda Vyeo kwa mujibu Wa Kanuni za Utumishi Wa Umma. Kwa ufupi ndo hivyo na ili kuthibitisha Wizara ya Utumishi iingie kwenye Mfumo Wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara (Lawson) itajionea yenyewe idadi kubwa ya watumishi ambao hawajapanda vyeo tangu mwaka 2012.
 
Hawahitaji kura ya mtu ili wakae hapo walipo
Kura ni formality tu lakini anayetangaza matokeo kwao ndiye wa muhimu zaidi!
labda hivyo ndo maana juzi chakubanga kawaita wasanii na kuiruka kauli ya dr bushiru,wakapewa wali na kuku so 2020 kina mama watakata mauno ya kwangwaruuu kama kawa mikutano ijae huku polisi wanaingia na masanduko ya kura tena mawakala wa chadema wakiwa wamefukuzwa vituoni
 
pamekuwa na unyanyasani mkubwa kwa watumishi wa umma tangu awamu hii iingie madarakani. mtumishi amekuwa kama kikaragosi. kwanza aliambiwa pasingekuwa na nyongeza ya mishahara wala kupandishwa madaraja hadi uhakiki uishe . akakubali.
baada ya uhakiki akambiwa hadi uzalishaji uongezeke . akakubali.
tena uhakik unaendlea tena hakuna nyongeza ya mshahara wala kupandishwa tena .japo ni kwa mujibu wa sheria!? twambiwa sheria kitu gani bwana tena mbele ya mandege, madaraja, umeme na mirel ya umeme?
leo wazir yule anayehudumu TAMISEMI ameulizwa swali bungeni . kama kuwafanya watumishi taahira waso na kumbukumbu anawatupia lawama maafisa utumishi ati hawapeleki taarifa kwa wakati. kwa bahati ndugai amestuka kwamba majibu ya yule wazir ni ya kiubabaishaji! amma kwa kuwa anaogopa au hana kumbukumbu na alichokisema. kasahau, kavimbiwa anabeua.N
nimkumbushe ndugu wazir taarifa za watumishi zipo kwenye mfumo Lawson. huhitajik tena kupeleka makaratasi ya taarifa za watumishi dodoma au ikulu zipo kwenye mfumo. kuwwtupia lawama ma HR ni kuudanganya umma na hao watumishi wenyewe!
ikumbukwe kuww motisha kwa watumishi ni sehemu muhimu ya huo uchumi wa viwanda .
mishahara ni suala la kisheria hulipwa kisheria wala sio hisani kama kugawa maburungutu ya noti kwenye misafara yetu hapana
gharama za maisha zinapanda kila siku nanyi mwajua.
Wazir yule ameambiww wik ijayo aje na majibu akajipange . asipotoshe wala asijibu bora liende.
Asante bwana ndugai kuwasemea watumishi japo wenyewe wamelala usingizi tena wa pono!

ANA RANGI MBILI, KESHO MTAMLAUMU TENA
 
Write your reply...Tatizo bunge .wasaidie watumishi wa umma.TUCTA iko kimyaa mno huku wakikata mishahara.
 
Write your reply...Tatizo bunge .wasaidie watumishi wa umma.TUCTA iko kimyaa mno huku wakikata mishahara.

Wapo tu kama alama. Hatuoni mchango wao wa maana kwa watumishi
 
Back
Top Bottom