Asante sana BAVICHA ninyi ndio vijana wa mfano kuigwa, mko tofauti sana

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Nimejaribu kufuatilia kwa kuzisoma mada nyingi sana humu hasa zinazohusu masuala ya kitaifa,siasa na uchumi! Kwakweli mmepevuka sana kiakili, niseme tu kwa moyo mkunjufu mnastahili pongezi.Nimeona ni kweli kabisa mmetoka kwenye siasa za uanaharakati na sasa mnajadili masuala na sio kujadili watu kwa mihemko. Kama ni mafunzo mnayopatiwa na viongozi wenu ni kweli wamethubutu.

Mnajadili masuala yenye tija kwa taifa tena mara nyingi mnadiriki hata kuweka uchambuzi wa takwimu na data zenye rejea, Kwakweli narudia tena kusema mmebadilika.Mashambulizi yenu kwenda CCM ni yenye akili na ukweli tena yasiyopotosha kama wao wanavyofanya.

Wakati ninyi mnajadili masuala wenzenu wa UVCCM wanajadili watu tena bila hata haya wala ushahidi wowote,mashambulizi butu yasiyopenya kwenye kundi la watu werevu.Mbaya za wanatukana na kudhalilisha bila kufahamu kua hizi siasa zilishapitwa na wakati.Wanashindwa kuelewa kua umma wa watanzania wa sasa unataka facts na sio blaa blaa.

Angalieni wenzenu wameshahau kua wao ndio jukumu lao kubwa kuishauri serikali yao kwenda katika mstari ulionyooka,pamoja na wao wenyewe kulakamika kua viongozi wao hawashauriki lakini kusiwafanye kuwasusia na kuanza kulalamika tu na kuandika majungu mitandaoni kutwa nzima badala yake wajaribu kwenda nao hivyo hivyo maana ndio waliowachagua.

Niwashauri tu BAVICHA ninyi ndio mnaobeba taswira za vijana wa taifa hili tofauti na wale wanaofikiri kukeshea kwenye mitandao na propaganda za kizamani ndio dili huku gurudumu zao likiendea kuzama.

Wao hawaelewi nini wafanye,ninyi mnajua nini cha kufanya niwatake kilaheri.
 
MAHANJU: Umesema kweli tupu. Lakini mimi sishangai vijana wa BAVICHA kuwa na hoja zenye mashiko. Inakuwa hivyo kwa sababu ya usomi hata kama sio wasomi sana lakini wengi wao ni wazuri kichwani. Kumbuka utafiti wa mwaka jana kwamba CCM inapendwa sana na watu wasio na elimu na upinzani unapendwa sana na watu wenye elimu. Na watu wengi wenye elimu wapo mijini na ndio maana upinzani unashinda sana maeneo ya miji. Miji kama Dar es salaam, Mbeya, Iringa, Kilimajaro, Arusha ni ya wasomi na yote inaongozwa na wapinzani. Angalia mikoa kama Singida na Dodoma ambayo ni ngome ya CCM hata kielimu iko nyuma sana!

Hebu tafakari kuwa mijini kuna umeme, lami, shule nzuri, hospitali nzuri, maji, n.k lakini hawaichagui CCM. Vijijini huduma zote hizo ni mbovu lakini wanaichagua CCM. Unafikiri ni kwa nini? Hawajielewi na elimu yao ni duni.
 
Back
Top Bottom