Vijana wanasiasa wajifunze kwa nguri wa siasa Lowassa

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
VIJANA WANASIASA WAJIFUNZE KWA NGURI WA SIASA LOWASA

Kizazi cha kina lowasa na wenzake kama kina JK,Kinana, Mangula etc ni kizazi kilicho anza siasa enzi za Nyerere wakati huo ilikua muhimu kwenda jeshini, kusoma chou cha siasa kivukoni, kushika madaraka ya serikali toka ngazi za chini ndipo uaminiwe kuwa mwanasiasa hata ukapewa ubunge.

Enzi hizo utumishi na Maisha ya siasa yalikua muhimu sana kuliko fedha za haraka haraka.

Lowassa siku anaondoka CCM hakutoa siri yeyote wala kumtukana mwana ccm hata CCM yenyewe. Hata wakati ambapo alikua amepishana na JK, alikua positive san ana JK na alikua makini san ana kila alicho kua anakiongea.

Huyu huyu lowasa siku ana ondoka CHADEMA chadema hakusema jambo lolote kuhusu chadema , walipo mpa muda aongee aliwambia tuu , narudi nyumbani, wakajaribu kumdodosa aseme neno alikataa katu, akasema yeye analo jua amerudi nyumbani. Na tangia hapo hajawahi kusema lolote kuhusu chadema na sidhani kama itakuja kutokea akasema mambo ya hovyo kuhusu chadema.

Katika Maisha hakuna adui wa kudumu wala Rafiki wa kudumu. Wanasiasa wazoefu wanalijua , wanasiasa wanajua juu maana ya Maisha ya siasa.

Hili pia linakosewa san ana vijana waajiriwa, utakuta kijana anapata kazi sehemu nyingine basi ataiponda kampuni anayo ondoka na mabosi wake utadhani alikua anawafanyia bure kumbe amelipwa hadi fedha ya kuondokea.

Watu wanao jua Maisha hata siku moja hawezi kumsema bosi wake hata awe mwovu kiasi gani, na hawezi kuisema kampuni anayo ondoka hata kama hakupata kile anapata kwa sababu anajua dunia ni mduara, unaye mkimbia kesho anaweza kuwa bosi wako tena.

Hivyo nawashauri wana siasa vijana hasa waliopo vyama vya upinzani, hata CCM. Ukikosa fursa tulia, kama umeona firsa sehemu nyingine usijiharibie Maisha yako ya baadae kwa kuongea mambo ambayo wazoefu wa siasa hawawezi kuyaongea.

Ukiona mwanaume anakusimulia mambo mabaya ya demu wake , basi ujue ana utoto mwingi na hatakuja pata demu mzuri wa kuoa. Mwanaume wa kweli demu akimpiga kibuti , ukiwmuliza anampa sifa kem kem, hata kama yeye ndio kampiga kibuti bado atampa sifa kemkem.

Vijana waliondoka Chadema na kuropoka mambo ya ovyo, tambueni hakuna chama ambacho kitawavumilia waropokaji na watu wachanga wa aina hii. Hawa vijana wamejipaka rangi ya utambulisho kwamba ni wasaliti na sii wa kuwaamini. Mwisho wao wa Maisha ya siasa si Zaidi ya miaka 5.

Ushauri, Vijana mtafuteni Lowasa awafundishe juu ya siasa.
 
Back
Top Bottom