Huyu alihusika sana kuiua NCCR Mageuzi! hivi yuko chama gani kwa sasa?
Ninachojaribu kutafakari juu ya Mahakama zetu ni pale zinapotoa hukumu za kuwabakisha wanachama kwenye vyama ili 'wasiathirike'.Unaweza kwenda mahakamani ukashitaki waliokuvua uanachama; na unaweza kushinda. Tatizo la kushinda mahakamani, katika siasa, ni kama kushindwa. Hii ni tofauti na kudai fedha. Unaweza kushinda na kujifariji kuwa umeonyesha jinsi ya kujipigania; lakini huwezi kushinda mahakamani na kurudi kufanya kazi za siasa na wale waliokuvua uanachama.
HATUA ya kufutiwa uanachama huwa haieleweki vizuri kwa watu wengi. Kuna mambo mengi ya kufanya pale unapofutiwa uanachama.
Unaweza kukaa kimya. Ukakubali kuondoka katika chama na hata ukaanzisha chama chako au kujiunga na chama kingine.
Unaweza kukaa kimya na ukaendelea kufanya mambo ambayo yanaweza hata kukisaidia chama ambamo umetimuliwa na hata vyama vingine. Ukapata umaarufu kufikia hatua ya waliokufuta uanachama kuanza kukuchumbia.
Unaweza kusahau shughuli zote za vyama vya siasa. Ukang'ang'ania eneo ulilosomea, ulilopenda, unalofahamu fika; na kujisimika kikamilifu. Hapa waweza kutumia uzoefu wako katika shughuli za siasa, kujenga mtazamo mpya juu ya mwenendo wa mambo katika jamii. Kama ni mwalimu, mchumi, mwanasheria, mwandishi wa habari, mfanyabiashara, mchuuzi/mjasiriamali au hata mkulima au mfugaji, waweza kutumia kile ulichochuma katika mienendo ya siasa, kutolea mifano ya kuleta mabadiliko katika jamii
Unaweza kwenda mahakamani – ukashitaki waliokuvua uanachama; na unaweza kushinda. Tatizo la kushinda mahakamani, katika siasa, ni kama kushindwa. Hii ni tofauti na kudai fedha. Unaweza kushinda na kujifariji kuwa umeonyesha jinsi ya kujipigania; lakini huwezi kushinda mahakamani na kurudi kufanya kazi za siasa na wale waliokuvua uanachama.
Unaweza kujiuzulu uanachama kabla hawajakufukuza; na bila kelele wala mikwaruzo. Hili nalo lina heshima yake hasa unapokuwa umeamua kuachana na malumbano na kukashifiana. Hatua hii inafanana kimya kinene na inaendana na eneo Na. 2 hapo juu, ambako unabaki katika jamii na sura yako ileile lakini ukiwa ‘ubongo rejea' kwa kila anayehitaji msaada wako.
Unaweza kuamua kujiua kisiasa, kijamii na kitaaluma; na wakati mwingine kiuchumi – kwa kujiingiza katika minyukano ya gharama kubwa – na wale unaowaita ‘wabaya' wako. Muda wako, fikra zako, rasilimali zako, hadhi na sura yako vinaweza kuteketea kwa mafao haba au bila mafao yoyote.
Unaweza kujiunga na wapinzani wakubwa wa chama chako ambamo umevuliwa uanachama. Ukatumika kwelikweli kukisema vibaya chama chako cha zamani. Ukapewa ujira mkubwa, ukabebwa juujuu na hata kuteuliwa kuwa mtu mkubwa katika siasa nchini mwako. Ukajiliwaza kwamba ‘afadhali nimewakomoa!'
Baada ya muda mfupi ukajizika mwenyewe. Mifano ya aina hii ni mingi Tanzania, hasa kwa wale waliochomoka/chomolewa kutoka upinzani na kuingia CCM wakitamba kuwa wana ‘siri' za upinzani wakati ni ama ulafi au njaa yao binafsi.
Uwanja ni mpana kwa wanasiasa wa kweli na wababaishaji; na kila uamuzi unaochukuliwa; kila mkondo unaochaguliwa una athari zake – mbaya au nzuri. Bali hakuna ramli. Ni kukaa na kufikiri, hasa kwa wale walioamua kwa dhati kwamba wanataka kutumikia siasa. Bali kwa wale ambao hawakujua tofauti kati ya siasa za vyama na uana-harakati, watateseka sana kabla hawajapata MSHAURI.
Katika mazingira ambamo siasa zinagusa maisha ya kila mtu kupitia mifumo – sera, sheria, kanuni, uamuzi mbalimbali – uwakilishi baraza la madiwani au bungeni, au uteuzi ikulu au kwingine kwenye madaraka; si njia pekee ya kufanya siasa. Hata wanaokana siasa ndio wanafanya siasa pevu ya kukana siasa bila mafanikio.
Makala hii imeandaliwa na Ndimara Tegambwage, ipo kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Jan 2014.
Asante kwa mfano mzuri na wa kueleweka. Na kwa vile lengo la chama ni wanachama kushirikiana ili kufikia malengo tarajiwa huku 'crushing' ya mawazo ikiwa within. Sasa nguvu ya Mahakama (sio sheria!!) inapokuwa kigezo cha uendeshwaji wa chama tafsiri yake inakuwaje!?Yuko sahihi kabisa. Ni kama maisha ya ndoa, mume anatoa talaka kwa mke kwa tuhuma kuwa mke huyo ni kahaba( na anatoa ushahidi) na mchawi nao ushahidi unatolewa. Kisha mke anaenda kanisani/ mahakamani kupinga ndoa kuvunjika na huko hukumu inatoka kuwa ndoa hiyo haiwezi kuvunjika kwa vile ilifungwa kanisani na ndoa ya kikristo haivunjiki hadi kifo hivyo jamaa amchukue tuu mkewe na waendelee kuishi.
Lakini jee kuna ndoa tena hapo?
huyu ni msukule wa mbowe unategemea angeandika tofauti na alichokiandika?ningeshangaa.
Kazi nyingine ni tamko la Mzee Mkono (mpaka sasa hajakanusha).Good analysis, Zitto unakazi ya kututhibitishia Kuwa wewe siyo mbinafsi kama tunavyo kutazama sasa huku nje.
Huyu alihusika sana kuiua NCCR Mageuzi! hivi yuko chama gani kwa sasa?
Nilisema kuhusu Zitto kusahau kuhusu kuwa na uwezo wa kufanya kazi na viongozi alioshindana nao mahakamani.
Ninachojaribu kutafakari juu ya Mahakama zetu ni pale zinapotoa hukumu za kuwabakisha wanachama kwenye vyama ili 'wasiathirike'.
Mwanachama wa chama cha siasa kama mtu binafsi anayo haki ya 'kulindwa na Mahakama' but on the other way round iko hivi: Je vyama kama Taasisi nazo si zina haki ya kulindwa na Mahakama kwa mujibu wa Katiba zao na Katiba ya nchi kwa ujumla!?
Kwa maana hiyo, kweli inawezekana siku moja ikatokea Mahakama 'ikatoa hukumu' ya kumlazimisha mwanachama aliyeamua kuondoka/kukihama chama asiondoke ili isisababishe damage kwa chama na shughuli zake? (fikiria mara mbili kama hujanielewa tafadhali).
HATUA ya kufutiwa uanachama huwa haieleweki vizuri kwa watu wengi. Kuna mambo mengi ya kufanya pale unapofutiwa uanachama.
Unaweza kukaa kimya. Ukakubali kuondoka katika chama na hata ukaanzisha chama chako au kujiunga na chama kingine.
Unaweza kukaa kimya na ukaendelea kufanya mambo ambayo yanaweza hata kukisaidia chama ambamo umetimuliwa na hata vyama vingine. Ukapata umaarufu kufikia hatua ya waliokufuta uanachama kuanza kukuchumbia.
Unaweza kusahau shughuli zote za vyama vya siasa. Ukangangania eneo ulilosomea, ulilopenda, unalofahamu fika; na kujisimika kikamilifu. Hapa waweza kutumia uzoefu wako katika shughuli za siasa, kujenga mtazamo mpya juu ya mwenendo wa mambo katika jamii. Kama ni mwalimu, mchumi, mwanasheria, mwandishi wa habari, mfanyabiashara, mchuuzi/mjasiriamali au hata mkulima au mfugaji, waweza kutumia kile ulichochuma katika mienendo ya siasa, kutolea mifano ya kuleta mabadiliko katika jamii.
Unaweza kwenda mahakamani ukashitaki waliokuvua uanachama; na unaweza kushinda. Tatizo la kushinda mahakamani, katika siasa, ni kama kushindwa. Hii ni tofauti na kudai fedha. Unaweza kushinda na kujifariji kuwa umeonyesha jinsi ya kujipigania; lakini huwezi kushinda mahakamani na kurudi kufanya kazi za siasa na wale waliokuvua uanachama.
Unaweza kujiuzulu uanachama kabla hawajakufukuza; na bila kelele wala mikwaruzo. Hili nalo lina heshima yake hasa unapokuwa umeamua kuachana na malumbano na kukashifiana. Hatua hii inafanana kimya kinene na inaendana na eneo Na. 2 hapo juu, ambako unabaki katika jamii na sura yako ileile lakini ukiwa ubongo rejea kwa kila anayehitaji msaada wako.
Unaweza kuamua kujiua kisiasa, kijamii na kitaaluma; na wakati mwingine kiuchumi kwa kujiingiza katika minyukano ya gharama kubwa na wale unaowaita wabaya wako. Muda wako, fikra zako, rasilimali zako, hadhi na sura yako vinaweza kuteketea kwa mafao haba au bila mafao yoyote.
Unaweza kujiunga na wapinzani wakubwa wa chama chako ambamo umevuliwa uanachama. Ukatumika kwelikweli kukisema vibaya chama chako cha zamani. Ukapewa ujira mkubwa, ukabebwa juujuu na hata kuteuliwa kuwa mtu mkubwa katika siasa nchini mwako. Ukajiliwaza kwamba afadhali nimewakomoa!
Baada ya muda mfupi ukajizika mwenyewe. Mifano ya aina hii ni mingi Tanzania, hasa kwa wale waliochomoka/chomolewa kutoka upinzani na kuingia CCM wakitamba kuwa wana siri za upinzani wakati ni ama ulafi au njaa yao binafsi.
Uwanja ni mpana kwa wanasiasa wa kweli na wababaishaji; na kila uamuzi unaochukuliwa; kila mkondo unaochaguliwa una athari zake mbaya au nzuri. Bali hakuna ramli. Ni kukaa na kufikiri, hasa kwa wale walioamua kwa dhati kwamba wanataka kutumikia siasa. Bali kwa wale ambao hawakujua tofauti kati ya siasa za vyama na uana-harakati, watateseka sana kabla hawajapata MSHAURI.
Katika mazingira ambamo siasa zinagusa maisha ya kila mtu kupitia mifumo sera, sheria, kanuni, uamuzi mbalimbali uwakilishi baraza la madiwani au bungeni, au uteuzi ikulu au kwingine kwenye madaraka; si njia pekee ya kufanya siasa. Hata wanaokana siasa ndio wanafanya siasa pevu ya kukana siasa bila mafanikio.
Makala hii imeandaliwa na Ndimara Tegambwage, ipo kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Jan 2014.