KIBURUDISHO
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 1,002
- 278
Nimeianza safari mapema leo asubuhi nikiwa njia moja kwendda kulitumikia Taifa langu baada ya kuhamishwa kituo changu cha kazi kutoka Wilaya ya Serengeti kwenda Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita niko ndani ya lori ndogo aina ya Canter ikiwa na vyombo vyangu nimefika Mwanza nikafanya mahitaji baadae njia. moja kwenda kivukoni nimetumia kivuko cha Kigongoni-Busisi.Duh saa saba mchana nilikuwa tayari kwenye foleni ya kuvushwa ila sasa tokea saa saba mchana hadi hivi sasa saa mbili kamili usiku ndio niko ndani ya pantoni navuka kwenda ng'ambo ya pili nawauliza wenyeji wananiambia mbele yangu nasubiliwa na masaa matatu ya kukimbia kwenye lami ya kwenda kwao na Mh Magufuli.Ninachompongeza Mh ni jinsi gani alivyoboresha suala la tiketi za kielectroniki tofauti na awali unaambiwa watumishi wa Temesa walikuwa na kaescrow kao hapo.Bado nipo katikati ya maji ikiwa ni mara yangu ya kwanza kabisa kusafiri na chombo kinachotumia maji kama sehemu ya barabara yake.WanaJf wa Chato naombeni mnipokee jamani.
ila chato pamechoka mkuu mahali pazuri ni ofisi za hamshauri tu kwingine ni uchuro, mugumu serengeti ni new york kwa chato
Tobaaa mugumu na serengeti ni new york kwa chato uwiii,nilikuwa mgumu mwaka 2004/2005 kipindi hicho hakukuwa na umeme sasa hivi nasikia kuna umeme kweli siku hazigandi,kuna baa moja inaitwa tanzanite hapo mugumu sijui bado ipo tulikuwa tunajidai hapo maana kulikuwa na generator na kulikuwa na nyama choma safii aisee nimiukumbuka sana mugumu,rubanda,ndabaka gate bunda.
KIBURUDISHO nime kuinbox,
Pole mkuu kwa safari ila safari bado ni ndefu. Usishangae ukifika Geita mida ya usiku ukazuiwa kuendelea na safari na polisi eti kuna msitu hapo mbele kidogo unaitwa Samina huwa kuna majambazi! sijui kama polisi wameacha mchezo huo,tuliwahi kuzuiwa hapo siku moja mida ya saa moja. Nilishangaa sana polisi anakuambia haturuhusu kwa sababu kuna majambazi huko mbele,sasa kazi ya polisi ni nini? Ta Kamugisha msitu wa Samina siku hizi ni salama?
Tobaaa mugumu na serengeti ni new york kwa chato uwiii,nilikuwa mgumu mwaka 2004/2005 kipindi hicho hakukuwa na umeme sasa hivi nasikia kuna umeme kweli siku hazigandi,kuna baa moja inaitwa tanzanite hapo mugumu sijui bado ipo tulikuwa tunajidai hapo maana kulikuwa na generator na kulikuwa na nyama choma safii aisee nimiukumbuka sana mugumu,rubanda,ndabaka gate bunda.
Ahahaaaaaa acha kunikumbusha tena huko nitapamiss sana uko kampuni gani wewe ya utalii?
KIBURUDISHO nime kuinbox,