Elections 2015 Asante Edward Ngoyai Lowassa

Mangisandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,652
2,272
Mheshimiwa Eduward Ngoyai Lowasa, nikiwa kijana wa Kitanzania, napenda kutambua Mchango wako mkubwa katika kuelekea mabadiliko Tanzania. Lengo lako na wengi tunaopenda mabadiliko ya kweli ilikua: IKULU.

Tulitaka ukasimamie mchakato wa mabadiliko kwa dhati, ukiwa kamanda namba moja. Kuonesha Imani yetu kwako tulikupa kura nyingi zaidi ya kura alizowahi kupata mgombea wa upinzani nchini Tanzania, na labda kuna kura zako nyingi zimepotea au kupotezwa!

Maamuzi uliyo fanya ni Yale ambayo Watanzania wengi wanaogopa kufanya, sababu kubwa ikiwa ile "fear of unknown" aliyo sema Sumaye. Kung'oka kwako CCM ni sauti ya kudumu ya kuhamasisha watu kukataa mfumo kandamizi, wenye dhuluma na msingi wake ukiwa maamuzi ya wachache.

Historia itakukumbuka kwa Ujasiri wa kukataa dhuluma na kuwa tayari kudai mabadiliko, hata nje ya mfumo, ambao wengine kwa kudanganywa, kwa uoga au kwa ujinga, wanauabudu! Matokeo hayaoneshi kukidhi matarajio yetu, lakini misingi imewekwa na ujumbe umefika!

ENL, umeweka tofali lako katika kuelekea MABADILIKO. Asante sana kwa kudhubutu, Mungu akubariki.
 
Pamoja sana enl mungu akupe maisha marefu ili uje ushuhudiye mabadiliko ulioyaanzisha miaka mitano ijayo.ameni
 
Umeandika vyema mkuu, hizo alizopata Lowasa, ni asilimia ambazo hajawahi kupata mgombea yeyote wa upinzani, ni kwa mara ya kwanza nchini, CCM hawawezi kuthubutu kusema wameshinda kwa kishindo, wanajua kuwa wameshinda kwa gilba, Hongera Edward Ngoyai Lowasa, Wewe ni jiwe walilolikataa CCM, likafanywa kuwa jiwe kuu la UKAWA!
 
Mbowe hawezi kuisoma namba. Ana biashara zake plus mshahara wa ubunge. Lowassa pia ana hela zake. Mbatia mhandisi pia mbunge. Tundu Lissu advocate. Ana hela zake. Kushangilia eti UKAWA watakoma ni ujinga. Atakayeisoma namba ni yule ambaye akija hospitali ukamwambia hela ya kumuona daktari ni 6000 anapanic anaanza kuwalaum madaktari. Anaeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini, bima ya afya hana, hata hela ya kumshonea mwanae uniform hana. Anaeisoma namba ni yule ambaye hawez kuafford milo mitatu iliyo kamili kwa siku. Ni upuuzi kwa mtanzania wa manzese (asiyeweza kulipa ada ya shule ya 40k kwa mwaka) kusema Duni ataisoma namba wakati ana taaluma yake na pesa zake. Unaeisoma namba ni wewe ambaye tokea umemaliza chuo ni miaka mitatu huna kazi (halaf kwa upumbavu unashabikia hapa kazi tu). PUMBAVU SANA. Unaeisoma namba ni wewe ambaye mtoto wako akiumwa mafua tu huwez kuafford dawa. Asilimia kubwa ya waliomchagua pombe ni ile 30% ya watanzania wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (kipato cha siku kuwa chini ya dola za kimarekani 1.9.. sawa na sh 4000 hiv). Hawa ndo wanaisoma namba, miaka 54 ya uhuru bado wanaishi gizani, bado hawawez kupata maji safi na salama... Halaf walivyo wapumbavu wanashabikia hapa kazi tu.. Kweli ni kazi.. Maana kushindia mlo mmoja kwa siku so mchezo, ni kazi kweli. Kumnywesha mwanao mwarobain kwa sabab huwez kumudu bei za madawa, so mchezo ni kazi haswa haswa.
Kama watanzania wenyewe ndo hawa ambao hawajitambui, WE HAVE A LONG WAY TO GO.
 
hii tu haitoshi tunapongezana ujinga wakati majimbo zaidi ya 200 kati ya 266 yamechukuliwa na CCM !sasa hapa tumepiga hatua gani?kuelekea kura za ndioooo?au vp?edward lowassa wakati wake ni sasa mpaka lini HAKI itapindishwa nchi hii?to what end?mtakuja kuchekwa na wajukuu zenu nyie!
 
Asante sana Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Utaendelea kuwa Rais wangu mpaka Maisha yako yote ya dunia hii. Ni haki yako umeporwa ila Mungu yupo.
 
Ushindi wa Magufuli una ukakasi hata wananchi wamebaki kimya utadhani hakuna kilichotokea.

Kumbuka: CCM ni ileile.
 
Haki ya mtu huwa haipotei, inaweza kuchelewa ndio lakini haipotei kamwe. Those who wait upon the LORD shall not grow weary, they will always renew their strength. Isaiah 40:31
 
hii tu haitoshi tunapongezana ujinga wakati majimbo zaidi ya 200 kati ya 266 yamechukuliwa na CCM !sasa hapa tumepiga hatua gani?kuelekea kura za ndioooo?au vp?edward lowassa wakati wake ni sasa mpaka lini HAKI itapindishwa nchi hii?to what end?mtakuja kuchekwa na wajukuu zenu nyie!
ENL amefanya kazi kubwa ndugu yangu, lakini kazi bado sana, mapambano yanaendelea!
 
Haki ya mtu huwa haipotei, inaweza kuchelewa ndio lakini haipotei kamwe. Those who wait upon the LORD shall not grow weary, they will always renew their strength. Isaiah 40:31
Kumtegemea Mungu ni jambo jema, Kama mlima Sayuni hutatikisika!
 
hii tu haitoshi tunapongezana ujinga wakati majimbo zaidi ya 200 kati ya 266 yamechukuliwa na CCM !sasa hapa tumepiga hatua gani?kuelekea kura za ndioooo?au vp?edward lowassa wakati wake ni sasa mpaka lini HAKI itapindishwa nchi hii?to what end?mtakuja kuchekwa na wajukuu zenu nyie!

Wewe upo kundi gani? Unataka nini kifanyike? Mchango wako ni nini?
 
UKAWA wabunge 59 kisha mnadai dola, mbona maajabu ya dunia haya!
Kuna viashiria vya haki haikutendeka hata kwenye hizo nafasi za ubunge! Lakini Hapa tunampongeza ENL kwa mchango wake katika harakati za mabadiliko nchini Tanzania.
 
Mbowe hawezi kuisoma namba. Ana biashara zake plus mshahara wa ubunge. Lowassa pia ana hela zake. Mbatia mhandisi pia mbunge. Tundu Lissu advocate. Ana hela zake. Kushangilia eti UKAWA watakoma ni ujinga. Atakayeisoma namba ni yule ambaye akija hospitali ukamwambia hela ya kumuona daktari ni 6000 anapanic anaanza kuwalaum madaktari. Anaeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini, bima ya afya hana, hata hela ya kumshonea mwanae uniform hana. Anaeisoma namba ni yule ambaye hawez kuafford milo mitatu iliyo kamili kwa siku. Ni upuuzi kwa mtanzania wa manzese (asiyeweza kulipa ada ya shule ya 40k kwa mwaka) kusema Duni ataisoma namba wakati ana taaluma yake na pesa zake. Unaeisoma namba ni wewe ambaye tokea umemaliza chuo ni miaka mitatu huna kazi (halaf kwa upumbavu unashabikia hapa kazi tu). PUMBAVU SANA. Unaeisoma namba ni wewe ambaye mtoto wako akiumwa mafua tu huwez kuafford dawa. Asilimia kubwa ya waliomchagua pombe ni ile 30% ya watanzania wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (kipato cha siku kuwa chini ya dola za kimarekani 1.9.. sawa na sh 4000 hiv). Hawa ndo wanaisoma namba, miaka 54 ya uhuru bado wanaishi gizani, bado hawawez kupata maji safi na salama... Halaf walivyo wapumbavu wanashabikia hapa kazi tu.. Kweli ni kazi.. Maana kushindia mlo mmoja kwa siku so mchezo, ni kazi kweli. Kumnywesha mwanao mwarobain kwa sabab huwez kumudu bei za madawa, so mchezo ni kazi haswa haswa.
Kama watanzania wenyewe ndo hawa ambao hawajitambui, WE HAVE A LONG WAY TO GO.
Mkuu Najua kufikia sasa utakua umebadikisha maoni kuhusu usomaji wa namba!
 
Back
Top Bottom