mkuu itafsiri article yote kwa manufaa ya jukwaa nashukuru
Mkuu sina utaalamu wa kutafsiri...
Ila kwa ufupi ni kuwa huyu mwandishi ni binti ambaye ni wa umri sawa na Ange..
Anaishi US ambako alienda akiwa mdogo akitokea kwenye kambi ya wakimbizi (na ametoa picha yake ya utotoni ambayo wanaomlea kwa sasa walimpiga nadhani anaishi na wazungu...hiyo picha ya mtoto ameshika tama ni yake akiwa mdogo)
Sasa juzi kati kakutana na Ange...Ange nae inaonekana amesomea US (unajua tena viongozi wetu...watoto wao lazima wapate quality education..lol)
Ananchoandika anasema alitamani amfate Ange pale gym walipokutana aanze kuongea nae kama mshikaji maana wanalingana na wote ni wanyarwanda...
Ndio anasema alichotaka kumwambia akashindwa lakini ameamua kumwandikia ndio hiki alichoandika na ku post kwenye mtandao kwani anasema ana uhakika Ange atasoma tu huu waraka
Anamwambia Ange kwa kuwa yeye ni kipenzi cha PK na ana influence kuliko mama yake...na anajua fika kuwa baba yake hana wa kumshauri kwa kuwa wote waliomzunguka wanamuogopa....basi yeye Ange amshawishi baba yake atafute amani ya ukweli ya Rwanda...aende South Africa akajifunze wenzake walifanya nini...
Anasema ana uhakika baba yake atamsikiliza sababu ni mtoto kipenzi...anasema baba yake hata akichukia...lakini atamsikiliza tu kuliko mtu mwingine kwa kuwa ni mtoto kipenzi...akiona kakasirika sana asubiri timing nyingine arudie kumwambia mpaka amsikilize...
Na anasema kabisa si yeye wala Ange wala vijana wa rika lao wana kosa lolote kuhusu mauaji ya 1994; ila wanaishi kama wakosaji sababu hakuna amani ya kweli Rwanda...
Ameandika kwa ufundi mkubwa siwezi kumuiga...
Ila nimemu admire mwandishi na kukubali kuwa Ange anaweza leta mabadiliko ya amani akitaka kufanya hivyo...daddy's daughter...
Lakini pia anamwambia Ange bila amani ya kweli future ya baba na kaka yake na watusti na wahutu wengine iko mashakani kwani huko Rwanda ni kuna bomu linasubiri kulipuka....
Nilichopenda kuhusu hii article huyu mwandishi haongelei kisasi wala sijui PK apelekwe ICC...anataka wasameheane.; maisha yasonge kama South..sasa kweli ameandika kitu kibaya kipi? Maana anamuombea heri hata PK