As a man, I have no room for tears

As a man, I have no room for tears

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
590
Reaction score
706
Alloyce Quote-1.png


"Kijana wa kiume, ni muhimu kutambua kwamba dunia haipo upande wako siku zote. Hii ni kwa sababu tangu enzi za mababu, wanaume tumehesabiwa kuwa na uwezo wa kutatua changamoto, hata ziwe kubwa kiasi gani. Tuna nafasi ya kupambana na adui yeyote, kwa ujasiri na hekima.

Uanaume si kulia ovyo, kulalamika, kutukana, kuwa na tabia za umbea, au kuishi maisha ya ‘ndiyo mzee’. Uanaume si kuogopa kuacha kazi isiyo na tija, au kuishi bila msimamo. Maisha yetu ni ya kubeba familia na taifa mabegani, si ya kukimbia majukumu.

Uanaume si jinsia pekee, ni matendo. Ni uthubutu, ni ukakamavu, ni heshima ya ndani isiyoyumba. Huwezi kuita nafsi yako mwanaume kama kila changamoto inakutoa machozi. Uanaume ni kuvumilia, ni kushinda, ni kuendelea kusimama hata pale ulimwengu unapokuangusha." — Alloyce, P.R.
 
Back
Top Bottom