NTIGAHELA
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 362
- 254
TUNAWEZAJE KUIONDOA CCM KWA KUDHIHAKI KAZI ZA WANANCHI?
Ndio Bodaboda ni kazi Kama zilivyo kazi zingine halali.
Pikipiki ni usafiri wa umma Kama yalivyo Magari, Ndege na vyombo vingine vya usafiri Kuna wanaotumia kama chombo binafsi Cha usafiri lakini wasionavyo wanachukua kwa malipo ya route au muda.
Changamoto wanazokutana nazo maafisa Bodaboda haifanyi KAZI YA BODABODA KUWA KAZI YA LAANA.
Hakuna kazi isiyo na changamoto, hata kazi ya siasa inachangamoto ambazo Kuna watu hawatamani wao Wala watoto wao kuingia kwenye siasa.
Kama ni ajali hata mafunzi ujenzi wanapata ajali wakiwa kazini, madereva wa magari ya abiria na binafsi yakiwemo ya wanasiasa yanapata ajali na kusababisha vilema na vifo kwa madereva na abiria.
Hoja ya kwamba hakuna watoto wa vigogo kwenye kazi ya bodaboda Basi hivyo ni kazi ya laana ni mfu sana. Ukienda pale msamvu Kuna wapiga debe, ukienda kule mabondeni Kuna watu wanaopoa mchanga, wapo Machinga na mama lishe kote huko hakuna watoto wa viongozi... Je nazo hizo ni kazi za laana? Kumbuka hao wachimba mchanga, Machinga, mama ntilie nk. Hawapo tu Tanzania, hata nchi nyingine wapo.
Hatuwezi wote tukawa viongozi, hatuwezi wote tukawa wabunge, hatuwezi wote tukawa wafanyabiashara wakubwa, hatuwezi wote tukawa maaskofu.
Ndio maana lazima tutafute njia za kujikwamua kimaisha, na kazi zetu ziheshimiwe.
Wengine hatuwezi kazi za wizi wa Magari na utapeli Wala hatuwezi kutengeneza michongo ya ukimbizi ili tukalelewe na wanaume wenzetu ughaibuni.
Vijana zipendeni kazi zenu, changamoto tuendelee kukabiliana nazo na mahala pa kupaza sauti zetu tupaze, tusikatishwe tamaa na wanaobeza kazi zinazotufanya tulee familia zetu.
Kwanza huyu jamaa amerudi Tanzania Tanzania kwa hisani ya mama Samia baada ya kufutiwa kesi na kulipiwa madeni ndio maana anakosa sera/hoja anaishia kutukana bodaboda na vicoba.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Mwambieni LEMA kazi za laana ni wizi wa Magari na kukimbia Madeni unayodaiwa.