Arusha wimbo wa taifa wabadilishwa rasmi

massai

JF-Expert Member
May 2, 2011
653
137
jamani wanachadema mliopo Arusha tunaomba mtuhakikishie hili la wimbo wa taifa kubadilishwa.natumiwa sms kuwa badala ya kuimba MUNGu ibariki Tanzania wanaimba MUNGU ibariki CHADEMA.vipi jamani ni kweli haya ninayoambiwa??
 
Binafsi siipendi CCM na serikali yake na wala simpendi yeyote anayeipenda CCM lakini sifurahii hii namna wamebadili huu wimbo wa taifa.

Ni kama kufanya mzaha hivi kwa mambo muhimu sana (na kwakuwa mimi ni Mkatoliki, nawezasema kuwa ni sawa na Mkatoliki kuchezea matakatifu/sacraments au visacrament!
 
Binafsi sijasikia, ila kama ndivyo nawashauri viongozi wa chadema walizuie hilo. Mambo ya kisiasa yaendeshwe kwa namna ya kisiasa, tunapokuja kwenye utaifa tuheshimu na tujivunie utaifa wetu. Wimbo, bendera na vyote vinavotambulishe utaifa wetu tusivishushe thamani sababu siasa.
 
nimeuliza sababu ni nini huyo jamaa yeye ni mwenyeji wa Arusha anasema Tanzania ilikua ni ya mwalimu Julius kambarage Nyerere hii Tanzania ya sasahivi ni uoza mtupu.tafakari kwa makini hii kauli kwani enzi ya mwalimu hapakuwa na wizi,ufisadi,umasikini,uharibifu ,ukoloni na uuwaji kama ulikuwepo sasahivi,tafakari kwa makini ndugu yangu,leo hii serekali iliyokuwepo madarakani ni yakifamili,kama hujui ni yakifamilia kivipi jaribu kumuuliza mtu mwenye ufahamu mkubwa atakupa fullcoverage ya viongozi wenye ndugu zao serekalini kuanzia kwa rais mpaka madiwani wa sisiemu.hivyo wameamua kuibadili hiyo nyimbo ili CHADEMA watakapochukua dola 2015 waubadili katika hali yake yakawaida.kwahiyo tuweni wavumilivu mpaka mabadiliko yakweli yatakapotimia
 
Binafsi siipendi CCM na serikali yake na wala simpendi yeyote anayeipenda CCM lakini sifurahii hii namna wamebadili huu wimbo wa taifa.

Ni kama kufanya mzaha hivi kwa mambo muhimu sana (na kwakuwa mimi ni Mkatoliki, nawezasema kuwa ni sawa na Mkatoliki kuchezea matakatifu/sacraments au visacrament!

wimbo wa taifa lako haueleweki vizuri, unamuomba mungu aibariki afrika, kwa ufahamu wangu afrika ni jina mbadala wa ALKEBULAN = The land of the blacks. wazungu walichungulia wakaona wakiacha jina halisi kuendelea ingekuwa clear nowadays kuwa ALKEBULAN IS FOR BLACKS. changamka mkuu uelewe yourstory, siyo history.
 
After all hatuna wimbo wa taifa ....tuna watunzi kibao tunategemea kutungiwa na watu wa taifa jingine??
 
Hoja hii haina mashiko. Kama ni matatizo ya kiuongozi yanahusu chama tawala ccm. Wimbo wanaouletea dhihaka sii wa ccm ni wa taifa zima. Wimbo huu hauna uhusiano na utawala aidha mzuri au mbaya. Kama kuna hati miliki ya wimbo wa taifa basi inamilikiwa na taifa zima na sii chama fulani. Jamani wasanii wapo kibao wapeni tenda ya kuwatungia wimbo muupendao na sii kuuchafua huu wa taifa
 
Yes... Mungu ibariki CDM, ili iweze kutukomboa waTZ. Rehema za Mungu ziwe juu ya CDM, na awalaani ccm...
 
Kama ni kweli,jua kuna Pandikizi la sisiemu.La,sivyo nlishawahi ckia mtu anasema Mchwa ukitaka kufa huwa unaota MBAWA..
 
wimbo wa taifa lako haueleweki vizuri, unamuomba mungu aibariki afrika, kwa ufahamu wangu afrika ni jina mbadala wa ALKEBULAN = The land of the blacks. wazungu walichungulia wakaona wakiacha jina halisi kuendelea ingekuwa clear nowadays kuwa ALKEBULAN IS FOR BLACKS. changamka mkuu uelewe yourstory, siyo history.
Ongeza ufafanuzu mkuu hii ni habari mpya masikioni mwangu, please.
 
vipi jamani ni kweli haya ninayoambiwa??
Ni kweli, cheki mwenyewe hapo chini nyomi la wananchi linaimba wimbo wa Taifa kuanzia dakika ya 1:05 or thereabout. I mean, it's so hilarious it's treasonous.

Last edited by a moderator:
jamani wanachadema mliopo Arusha tunaomba mtuhakikishie hili la wimbo wa taifa kubadilishwa.natumiwa sms kuwa badala ya kuimba MUNGu ibariki Tanzania wanaimba MUNGU ibariki CHADEMA.vipi jamani ni kweli haya ninayoambiwa??
Hoja za kijinga hizi.
Sasa mtoa mada ulitaka wimbo upi? Mungu ibariki Chadema? Chadema si Tanzania na kama inapendwaArusha basi ujue Arusha si Tanzania yote.
Halafu Mods ile mada ya matukio ya kusikitisha huko Arusha juu ya Nasari kutamka kuwa CDM inataka Arusha ijitenge mbona mmeiondos?
Ujinga huu unaifanya hata JF kuingia mkenge.
Let them spill their own beans!
 
Wewe acha umagamba wako? Mimi naamini kuna siku kabla ya 2015 utabadilika.
 
Hoja hii haina mashiko. Kama ni matatizo ya kiuongozi yanahusu chama tawala ccm. Wimbo wanaouletea dhihaka sii wa ccm ni wa taifa zima. Wimbo huu hauna uhusiano na utawala aidha mzuri au mbaya. Kama kuna hati miliki ya wimbo wa taifa basi inamilikiwa na taifa zima na sii chama fulani. Jamani wasanii wapo kibao wapeni tenda ya kuwatungia wimbo muupendao na sii kuuchafua huu wa taifa
Usiwe na wasiwasi huo mwimbo unaoimbwa ni wa CDM sio mwimbo wa Taifa mwimbo wa taifa unataja Tanzania lakini huu wa kwetu Unataja CDM na lengo ni kumuomba mungu aibariki CDM kwa ajili ya Kuwakomboa Watanzania.
 
Hawajabadili, katika makusanyo ya watu huwezi kuzuia mtu moja mmoja asitende jambo au kupayuka kutokana na kila kinachomkwaza.

Katika thread yako ungesema chanzo halisi, yaani kutoka kwa kiongozi yoyote au msemaji wa CHADEMA ili tuchangie, hivi hivi ni fake tu.
 
jamani wanachadema mliopo Arusha tunaomba mtuhakikishie hili la wimbo wa taifa kubadilishwa.natumiwa sms kuwa badala ya kuimba MUNGu ibariki Tanzania wanaimba MUNGU ibariki CHADEMA.vipi jamani ni kweli haya ninayoambiwa??

Ukisikia utaahira ndio huu. Badala ya kuiombea nchi, wanawaombea wajanja ambao wanaweza kuwageuka wakati wowote. Watanzania wanatakiwa kuamka na kuachana kuifanya siasa kuwa kama Simba na Yanga. Siasa ni uhai wetu na tusiwashabikie watu kwa vile tu wanao uwezo wa kukusanya watu wengi au kelele zao ni kubwa kuliko wengine. Matendo yao yawe ni muhimu kwetu zaidi kuliko maneno yao. Baadhi ya vyama vya siasa ni bado ni NGO za wachache.
 
Sasa wafanyaje kama ccm inadhulumu, dola inawasapoti, serikali kilasiku habari mpya ya wizi. Kumbukeni kua ukanda unatokana na haya haya ya watu kukerwa alafu wanakosa pakutokea.
 
Back
Top Bottom