Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,612
- 40,158
ARUSHA : RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kipindi cha mwaka mmoja katika mkutano wa 25 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wa jumuiya hiyo.
Akikabidhi uenyekiti huo, Rais wa Kenya, William Ruto, amesema Museveni atachukua nafasi hiyo baada ya yeye kumaliza muda wake wa kuliongoza baraza hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Baada ya kutangazwa, Rais Museveni amemshukuru Rais Ruto kwa kuiongoza jumuiya hiyo katika kipindi cha mwaka uliopita na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili kuimarisha maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani ya jumuiya hiyo.
Aidha ametoa shukrani kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa mapokezi mazuri waliyopata wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Arusha.
#HabariLeoUpdates