Arusha: Rais Magufuli anafanya uzinduzi wa safari za treni ya abiria

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Rais Magufuli anazindua safari za treni ya abiria Jijini Arusha baada ya huduma hiyo kusimama kwa zaidi ya miaka 30.





Abiria 50,579 wamesafiri na treni Dar- Moshi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania(TRC), Masanja Kadogosa amesema zaidi ya abiria 50,579 wamesafirishwa kupitia treni inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda Arusha kupitia Moshi na Tanga.

Pia, tani zaidi ya 26,000 za mbolea na saruji zimesafirishwa katika kipindi cha miezi 9 tangu treni hiyo ilipoanza safari kwenda Moshi kabla ya kufika Arusha.

Kadogosa amesema hayo katika uzinduzi rasmi wa treni ya abiria inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha kupitia Moshi na Tanga iliyokuwa imeacha kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

Amesema kabla ya uzinduzi huo, ulifanyika ukarabati uliogharamu zaidi ya Sh14 bilioni pesa zilizotolewa na Serikali huku kazi hiyo ikifanywa na wahandisi kutoka shirika la reli na kuajiri zaidi ya vijana 600.

“Kwa idadi ya hii ya abiria tuliowahudumia maana yake ni kuwa kuna Watanzania zaidi ya 5,000 wanaokuja Arusha, Moshi na Tanga wanategemea reli hii kwa sasa na tuna zaidi ya tani 2600 zinasafirishwa kila mwezi,” amesema.

“Nauli inayotumika katika treni ni ndogo na mtu anaweza kubaki na akiba tofauti na angetumia usafiri mwingine, kwa wafanyabiashara wadogo ina faida kwa sababu kabla hatujaanza tani moja ya mbolea walikuwa wanasafirisha kati ya Sh93,334 hadi Sh100,000 na sasa ni Sh46,000 tu kwa tani,”amesema Kadogosa.

“Maana yake ni neema kwa wakulima wa maeneo haya, kwa upande wa saruji walikuwa wanasafisha tani moja kwa Sh100,000 hadi Sh110,000 baada ya sisi kuja tani moja ni Sh68,000 unaweza kuona faida hii kubwa iliyoletwa na ujio wa reli,”amesema.

Amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo wamepanga kuwa na miundombinu baridi kwa ajili ya wakulima wa maua na mbogamboga

“Tunataka kujenga hapa ili waweze kuhifadhi na kwa upande wa Dar es Salaam itakuwa eneo la Kurasini na hi itasaidia sana wakulima wa Mbogamboga,” amesema Kadogosa.

Magufuli: Baada ya uchaguzi Serikali imejipanga kununua vichwa vya treni​

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema baada ya uchaguzi kukamilika Serikali imejipanga kununua vichwa vya treni 39 kwa njia kuu na vingine 18 vya treni sogeza sogeza.

Mbali na hilo pia imejipanga kununua mebehewa 800 ya kusafirishia mizigo na 37 abiria
Amesema hayo katika uzinduzi rasmi wa treni ya abiria inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha kupitia Moshi na Tanga iliyokuwa imeacha kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa mfano Afrika kwa mashirika yanayofanya biashara na kufanya kazi kwa kuhudumia wananchi wake ikiwemo wanyonge.

“Wito wangu kwenu (TRC) hakikisheni mnaendelea kuimarisha na kuboresha huduma zenu na gharama zenu zinakuwa chini na kupiga rushwa ili watanzania waweze kunufaika na usafiri huu,”

“Watanzania pia hususani wakazi wa mikoa ya kaskazini kutumia reli hii vizuri ili kuweza kunufaika nayo, serikali tayari imetekeleza wajibu wake sasa ni wajibu wa Watanzania wote kuweza kuilinda,”amesema.

Amesema kuna wakati aliwahi kusikia njama za watu wakitaka kuharibu reli hivyo aliwataka Watanzania kulinda miundombinu ya treni inatunzwa ili kuweza kuwasaidia.

“Ujio wa treni hii hapa Arusha, uchumi wake utapanda, watu watafanya biashara, hata mama lishe watapeleka vyakula vyao kwa viongozi wa treni na abiria wanaoteremka, wenye nyumba za kulala wageni watapata wateja kwa mpigo hivyo ujio wa treni hii ni suluhisho kwa ajili ya kujenga uchumi wa maeneo haya,” amesema Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Serikali kutokubali kubinafsisha vitu vya msingi katika nchi huku akitolea mfano wa ndege zilizobinafsishwa.

“Tulibinafsisha ndege zote zikaisha tumekuja kuanza upya, tukabinafsisha treni tumekuja kuanza upya, tulikuwa na meli zilizoachwa tangu enzi za baba wa Taifa hazipo, sasa hili liwe ni fundisho, mimi sitakuwa Rais wa Maisha ila natoa ujumbe wangu kwa wale watakaokuja baadaye kuwa hili liwe fundisho,’’

“Hata nchi zilizoendelea mashirika yao ya reli hawajabinafsisha ibaki kuwa ndani ya serikali ili huduma kwa wananchi wanyonge ndiyo itawafikia Wananchi kupitia hiyo treni na vinginevyo,” amesema Magufuli.

MARA YA MWISHO TRENI ILIENDA ARUSHA MWAKA 1986

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) amesema treni kwa mara ya mwisho ilifika Arusha mwaka 1986, akisema ni kama Mwl. Nyerere alipoondoka madarakani aliondoka na huduma ya reli

Ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa safari za treni, Dar, Tanga, Moshi na Arusha ambayo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli

Ukarabati wa reli hiyo umeghrimu Tsh Bilioni 14 ambazo zimetolewa na serikali. Huduma hiyo imeboresha usafirishaji wa mizigo na abiria wa njia ya Arusha kuelekea Dar

Pia amesema ukarabati wa reli hiyo umefanyika na wakandarasi wa TRC
 
CCM ni Mabingwa wa kutengeneza tatizo halafu kuna kulitatua kwa mbwembwe.

Hii Treni na Reli iliuwawa na CCM na Makada wake Leo wanaifufua na kuizindua.
 
Back
Top Bottom