Arusha: Polisi yazuia mikutano ya Lema

Arusha: Polisi yazuia mikutano ya Lema

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
pic+lema.jpg

Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.

Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa CHADEMA kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.

Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema jana Jumatano, imeeleza mikutano yake imesitishwa.

Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.

Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.

Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.

"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017 pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.

Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.

Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.

Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.

"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye mkutano," amesema.

Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.

Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.

Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na alitii agizo hilo.

Mwananchi
 
Niko hapa sakina nakula nyama choma na amarula cream kwa furaha.
 
Hao viongozi wanakuja kuitisha mikutano ya hadhara?
 
Yaani hata hii ya kufanya mikutano kwenye majimbo yao wananyimwa?

Chadema mkikaa kimya nyie ni wasengerema
 
  • Thanks
Reactions: PNC
View attachment 597651
Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.

Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa CHADEMA kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.

Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema jana Jumatano, imeeleza mikutano yake imesitishwa.

Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.

Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.

Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.

"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017 pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.

Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.

Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.

Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.

"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye mkutano," amesema.

Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.

Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.

Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na alitii agizo hilo.

Mwananchi
Maelekezo kutoka juu,kweli police ni tawi la ccm
 
haisaidii kitu kwani hata ikizuiwa kwa siku anazotaka,atakaporuhusiwa kutakuwa nyomi ya kufa mtu ili mradi wananchi wana hamu ya kumsikiliza Nyerere wa Arusha
 
Nchi imeingiliwa kwa mlango wanyuma tena. CCM wanazidi kuibaka Tanzania
 
View attachment 597651

Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.

"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017 pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.

Mwananchi
Huyu OCD ana vyeti kweli?
 
Uoga, uoga, uoga kila mahali! Liliisha kuwa bayana kuwa wale wote waliokwenda Nairobi kumjulia Lissu hali washughulikiwe nje na ndani. Msigwa kashushwa jukwaani, Mbowe kanyang'anywa gari na huko Lema anazuiwa kukutana na wapigakura wake kupata mrejesho, kero na matatizo pamoja na changamoto za kufanikisha maendeleo. Tunaelekea wapi na kwa mwendo huu hatufiki. Hatakama angeshawishi kuraise fund ya ujenzi wa nyumba zao zilizojiwakia moto, wachangiaji watakuwa na moyo tena?
 
Tumechagua pombe iongoze nchi hapa ndipo watanzania tumejimix

Kiongozi muoga kuwahi kutokea duniani
 
Inawezekana mkulu anarudi kupiga another shoo na wale madiwani waliogoma kupanda stejini baada ya dau kuwa dogo (ni hisia tu).
Je hao viongozi wanafanya mikutano au mikutano italeta shida gani kwenye majukumu yao?
Inafikia kipindi watu wanahisi gov't imejichomea nyumba kuukuu iliwaweze kupiga shoo kama ile ya siku ya wajeda ilibuma … na hii vilevile ( in bwege voice)
 
Back
Top Bottom