Arusha: Polisi yazuia mikutano ya Lema

Arusha: Polisi yazuia mikutano ya Lema

Nyingine tena!!! Hatimaye sasa jini linaanza kujichomoa lenyewe kutoka kwenye chupa! This time hata punguani anajua hii ni serikali ya namna gani!nashukuru leo mwigulu amezungumzia kuhusu miili ya watu inayookotwa Ikiwa kwenye viroba huku mingine ikiwa imefungwa mawe mazito!!! Amesema ni ya wahamiaji haramu!!!!!hongera kwa hilo! Huo ndiyo Uchapa kazi unaotakiwa na serikali! Wahamiaji Haramu ni janga! Japo hatujaambiwa walikuwa wanatoka wapi kuhamia wapi! Let's Go
 
Hawa jamaa wanahaha sasa wanaweza kukataza kabisa watu kuzungumza hata na jirani zao
 
Msipoangalia hiyo chuki mnayoijaza miyoni mwenu itawafanya kuchuma dhambi na hamtakuwa na furaha.
Lema kaombwa mikutano yake apange kuanzia tarehe tano. ...mmeshafanya nongwa. Shida mnayo na inawatafuna mifupa. Kila kitu mnakikuzwa kuzusha uongo. Mtaumia ninyi na roho zenu
 
Inawezekana mkulu anarudi kupiga another shoo na wale madiwani waliogoma kupanda stejini baada ya dau kuwa dogo (ni hisia tu).
Je hao viongozi wanafanya mikutano au mikutano italeta shida gani kwenye majukumu yao?
Inafikia kipindi watu wanahisi gov't imejichomea nyumba kuukuu iliwaweze kupiga shoo kama ile ya siku ya wajeda ilibuma … na hii vilevile ( in bwege voice)
Kwanini hao viongozi ndio wasiahirishe ziara zao kupisha mikutano ya wenyeji.
 
Msipoangalia hiyo chuki mnayoijaza miyoni mwenu itawafanya kuchuma dhambi na hamtakuwa na furaha.
Lema kaombwa mikutano yake apange kuanzia tarehe tano. ...mmeshafanya nongwa. Shida mnayo na inawatafuna mifupa. Kila kitu mnakikuzwa kuzusha uongo. Mtaumia ninyi na roho zenu
Kwanini hao wageni wasiambiwe kuahirisha ziara zao kupisha shughuli za wenyeji?
 
Yaani hata hii ya kufanya mikutano kwenye majimbo yao wananyimwa?

Chadema mkikaa kimya nyie ni wasengerema
Chadema waende UN pia waende The Hague wakashitaki Jeshi la polisi wasipofanya hivyo wataendelea kunyayasika.
 
Amezuiwa au imehairishwa?
tapatalk_1506230286614.jpeg

Wakiacha kubeba hilo begi ndo watalielewa swali lako !
 
View attachment 597651
Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.

Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa CHADEMA kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.

Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema jana Jumatano, imeeleza mikutano yake imesitishwa.

Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.

Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.

Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.

"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017 pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.

Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.

Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.

Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.

"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye mkutano," amesema.

Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.

Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.

Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na alitii agizo hilo.

Mwananchi
Tatizo polisi wetu wengi ni form IV failures na wanajaribu kujipendekeza kwa phd failure
 
Tarehe 5 October Mh Lema nenda kaongee na wanainchi wa Kimandolu kuhusu Diwani aliyejiuzuru,Kuhusu Ziara ya Rais na hata shambulio la Tundu Lissu wala hujazuiliwa ila mkutano umesogezwa mbele tu kupisha huo ugeni basi.

Be Patient Hon Lema.
 
Polisi yazuia mikutano ya Lema

Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.
Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa Chadema kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.
Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema jana Jumatano, imeeleza mikutano yake imesitishwa.
Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.
Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.
Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.
"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017 pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe 29/09/2017," inasomeka barua hiyo.
Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.
Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.
Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.
"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye mkutano," amesema.
Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.
Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.
Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na alitii agizo hilo.

DOWNLOAD APP YA CHADEMA NEWS KUPATA KILA UPDATES YA CHADEMA NA TAIFA KWA UJUMLA CLICKB HAPA Chadema News – Програми Android у Google Play
 
Attachments

  • lema+polis.jpg
    lema+polis.jpg
    96.4 KB · Views: 24
  • CHADEMA NEWS LOGO.jpg
    CHADEMA NEWS LOGO.jpg
    20.7 KB · Views: 17
Katika hili hakuna haja ya Lema kutunishiana misuli na Polisi
nadhani wameelezea vizuri tu
 
Back
Top Bottom