S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 88
NAifahamu Arusha Modern iko Arusha maeneo ya kisongo ni nje ya mji kabisa, ni shule nzuri ina maadili ya dini full maombi hiulo kila mtu analijua, kwa upande wa masomo wanafanya vizuri japo si maksi za kutisha sana lakini hamna aneyfail, ni boarding na watotot wanafundishwa kazi kama ni mdogo wa kike anapewa dada yake wa madarasa ya juu atakayemfundisha kazi ndogondogo mpaka azoee,
Na mazingira si ya kimjini sana ambayo yanampa mtoto vishawishi ni shule ya wahindi.
Na pia kuna st. Patrick Trust Academy ni shule nzuri sana inaanzi baby class mpaka chuo pale mtot akienda hata kama kichwa chake si kizuri lazima atapasua tu jaribu hizo nikiendele kukumbuka nitakuambia, halafu ungesema mtot wa jisnia gani na anasoma darasa la ngapi au secondary ndo ingekuwa nzuri zaidi
Ahsante Joyceline,
Mtoto wa kiume, natafuta shule aingie Form 1.
1. Yes Agape mwaka jana ilikuwa among the best 10 kwa matokea ya form IV Tz! Nadhani likuwa ya sita!
Kimaadili ni shule ya Lutheran: na ipo nje ya mji Mamba-Mkolowony, sii mbali toka Marangu na hakuna vishawishi!
sema inakuwa kazi sana kupata nafasi ni bora basi uanze maandalizi mapema!
2. Kwa wenye watoto wakike kuna St. Anuarite ipo karibu na Kawawa Rd, Moshi it was also among the best 10 Tz mwaka jana! Ni ya bweni chini wa RC! wako so strong haswa ktk Sayansi!
kumbe ni mkubwa kiasi, kama ingekuwa umependelea mkoa mwingine ningekucctizia sana AGAPE SEMINARY kilimanjaro, ni nzuri sana sana.
ningekushauri kati ya st Patrick,Green valley, st Costantine na st Jude., Joyceline Arusha modern haufiki kisongo, pale bado ni sakina.
Wa boarding wote wanakaa Kisongo, sakina ni madarasa tu kulala na kila kiru ni Kisongo
Agape ni nzuri sana ila kupata ni tatizo inabidi ujiandae,
na pia kuna st. Dorcas iko hai maeneo ya boma Ng'ombe ni nzuri sana inafundisha vizuri na pia ina maadili, mdogo wangu anasoma hapo alikuwa mtupu kichwani lakini sasa ni bonge la kichwa.
mzazi ukienda kumuona mtoto wako unaombewa kwanza usije ukamuambukiza maroho na matabia uliyotoka nayo nyumbani ila kama mtoto ni mchoyo hataweza maana kila kinacholetwa anakula na wenzake( joke)
Kuna shule moja ya wavulana maeneo ya same ndo imeto form four ya kwanza mwaka jana lakini wamejitahidi sana inamilikiwa na kanisa katoliki iko kama seminari jaribu kuulizia na hiyo au nenda pale msimbazi centre unapewa orodha ya shule za kanisa na perfomance zake bado hujachelewa.
kuna mukidoma pia iko nje ya mji (Usa River) ni shule nzuri.
Mukidoma ilikuwa nzuri ila sasa wana matatizo kidogo. Na zipo mukidoma mbili,ambapo mojawapo ilikuwa au bado ipo ndani ya eneo la NAIC na ilitakiwa kuondoka kuhamia eneo lingine. Pia siku hizi inaperform below standard na service zake haziendani na gharama ya shule,ilifungikwa kama siyo kupewa warning.
Ilikuwa ya dini ya kisabato ila hawabagui dini yoyote sema unafuata mwenendo wao yaani kukubaliana na sheria zao. Hope Mama Masanja(mmiliki wa mukidoma) atarekebisha na kurudi kwenye standard ilivyokuwa.
Kuna shule nyingine inaitwa taps/tass, ila kwa sasa sijui hali yake kwasasa kitaaluma. inaanzia kindergaten-form 4.Ipo usa-river/momela.
St.Constantine kwa arusha ni nzuri pia,tembelea www.scisarusha.org
Ukifikiria jirani na arusha jaribu cheki na St.Margoreth ipo moshi nzuri ni ya masista
Hata hii ila haipo arusha ni Stanley ipo tuangoma-temeke ni mpya kidogo,boarding.
Pia kwa dar, Feza boys inafanya vizuri tena boarding ipo.