Arusha: Madiwani wawili wa CHADEMA Prosper Msofe na Obeid Meng’oriki, wajiuzulu na kujiunga CCM

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Kutoka jijini Arusha AyoTV imezipata taarifa za diwani wa kata ya Daraja Mbili Arusha Prosper Msofe katika jimbo la Arusha Mjini amejiuzulu nafasi yake nakuhamia CCM kwa madai ya kumuunga mkono Raisi Magufuli.

Pamoja na mambo mengine Prosper Msofe amesema CHADEMA kimekuwa chama kinachoongozwa na Mbunge Lema katika mkoa wa Arusha na ameadai kuwa meya amekuwa akikataa kuambiwa ukweli.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia amekiri kupokea barua hiyo na zikiwemo barua za madiwani wengine wa CHADEMA kujiuzulu nafazi zao hizo kwa madai wa kuhamia CCM.

Chanzo: Millard Ayo

-------------
rusha.jpg

Madiwani wawili wa Chadema kutoka Arusha Mjini wamehamia CCM muda huu.

Diwani wa kata ya Daraja Mbili Ndg. Prosper Msofe na Diwani wa kata ya Terrat Ndg.Obeid Meng’oriki (Chadema) wamejiuzulu uanachama na udiwani leo hii na kutangaza kujiunga na ccm kwa kile walichoeleza kuwa wamefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Mh Rais Magufuli.

Diwani mmoja amesema; "Hakuna maisha magumu kisiasa kama kuishi kwenye Ukoo wa kambale ambao Baba, Mama na watoto wote wana Ndevu. Agenda hakuna, kila Mtu mropokaji na kulazimishana kufanya siasa za kuhujumu maendeleo kama njia ya kuijenga Chadema badala ya Nchi. Tukiendelea na siasa za namna hii, itafika wakati tutaambiwa tukabomoe Madaraja na kuiba pampu za miradi ya maji?

Tumekataa siasa hizi za kishetani na tunawaomba Watanzania wazikatae pia."
 
Anamuunga mkono rais kwenye nini! Maana rais yako mambo ya hovyo sana anayafanya kiasi ambacho hata shetani anamshangaa.

Chama kinachoua watu ili kisalie madarakani utaanzaje kukiunga mkono kama siyo ujinga!

Rais anayeishia kutweet tu kwenye mambo yanayoligawa taifa huku mambo malaini laini ya kutafutia kiki anafoka foka utafikiri kamezeshwa omo!
 
Hii hama hama ingetokea ccm kwenda cdm sasa hivi neno lingekuwa ukombozi umekaribia.CCM bado itabakia kuwa chama bora TZ kutokana na mifumo ya ndani na hazina ya wananchana.CDM uimara wake uko kwenye vurugu na ubinafsi wa viongozi
Mifumo bora ya kuwindana na smg aisee
 
Hahaaa!! Mwenyekiti wa cdm atapata tezi dume kwa hali hii, nyumbu bado wanaamini eti ukombozi unakuja yaani nchi uwape makanjanja halafu ufikiri umeikomboa, the ratio goes further till all nyumbus get awakened!!
 
Madiwani wawili wa Chadema kutoka Arusha Mjini wamehamia CCM muda huu.
arusha.jpg

Diwani wa kata ya Daraja Mbili Ndg. Prosper Msofe na Diwani wa kata ya Terrat Ndg.Obeid Meng’oriki (Chadema) wamejiuzulu uanachama na udiwani leo hii na kutangaza kujiunga na ccm kwa kile walichoeleza kuwa wamefanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Mh Rais Magufuli.

Diwani mmoja amesema; "Hakuna maisha magumu kisiasa kama kuishi kwenye Ukoo wa kambale ambao Baba, Mama na watoto wote wana Ndevu. Agenda hakuna, kila Mtu mropokaji na kulazimishana kufanya siasa za kuhujumu maendeleo kama njia ya kuijenga Chadema badala ya Nchi. Tukiendelea na siasa za namna hii, itafika wakati tutaambiwa tukabomoe Madaraja na kuiba pampu za miradi ya maji?
rusha.jpg

Tumekataa siasa hizi za kishetani na tunawaomba Watanzania wazikatae pia."
 
Diwani Obedi Moses wa Kata ya Terati na Prosper Msofe wa Kata ya Daraja mbili, Arusha wametangaza kujiuzulu nafasi zao leo na kujiunga na CCM
Ukimkuta mtu mlevi anajikojolea barabarani, ukaanza kumshangaa au hata kumshutumu, basi wewe una akili ya kilevi zaidi yake
 
figganigga
Hawana Huruma na Kodi zetu, Majimbo yao yabaki wazi mpaka 2020 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Hii hasara ingetumika kwenye shughuli zingine.
 
Back
Top Bottom