Hilipendo
Senior Member
- Sep 13, 2011
- 188
- 97
Kazi mojawapo kwenye job descriptions alizopewa Kinana ambazo ni kupata viongozi kutoka CHADEMA, imeshamshinda.
Tena yeye mwenyewe Kwa kujua au kutojua, anakiri kushindwa hayo majukumu aliyopewa na maCCM wenzake.
Kwa watu wanaofuatilia ziara za Kinana mikoani akijaribu kuinasua CCM chumba cha ICU, watakuwa wamebaini aibu aliyoipata juzi huko Ngorongoro ambapo aliingizwa mkenge na wenzake.
Wakamwekea watu wawili. Akaambiwa kuwa eti ni viongozi wakubwa au vigogo huko CHADEMA. Loh! Naye kama ilivyo kawaida ya CCM akaingia kichwa kichwa na kuwapokea jukwaani eti anapokea viongozi wa CHADEMA.
Alas! Kumbe Mzee mzima na ujeshi wake amelambishwa galasa na viongozi wake.
Kumbe hao wote alioambiwa kwamba ni vigogo wa CHADEMA kumbe wako CCM kitambo hadi mmoja amegombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na akabahatika kushinda nafasi Kwenye serikali za mitaa...
Leo pia kaharibikiwa huko Longido.
Si tu kwamba amelamba galasa tena Kwa mara nyingine, bali safari hii kampokea mtu aliyekuwa mlinzi wa ofisi akiambiwa ni kiongozi mkubwa wa CHADEMA, kigogo wa Wilaya ya Longido.
Tutoe wito kwa CCM; kwanza hiyo job description waliyompatia Kinana ya kuendelea kufanya siasa za ghiliba za kununua au kulaghai viongozi wa CHADEMA imeshamshinda.
Kama walimpatia target za ku-meet wajiandae kumwonesha njia aliyoelekezwa Mangula, Makamba na Mkama.
Katika hali ya umahututi wa kisiasa ambayo CCM imefikia, si Kikwete, Kinana wala kijana wao asiyejua hadhi ya mdomo wake, wanaweza kuinua chama hicho.
Tunashukuru ziara za Kinana zinashuhudia namna CHADEMA ilivyojikita akilini na mioyoni mwa watu. Hawakununuliwa wale. Hawajaghilibiwa. Ni Hoja za kisiasa zinazozungumzia maendeleo yao na mstakabali wa maisha yao na taifa hili.
Wakati Kinana katika kukimbizana na target alizopewa na aliyemtuma za kununua viongozi wa CHADEMA eti kama njia ya kushusha morali wa mapambano ya wanyonge dhidi ya mfumo na utawala mbovu, CHADEMA inaendelea kusimika mizizi si kwa wale wenye vyama tu, bali ikilenga constituent kubwa ya Watanzania ambao hawakuwahi kuwa CCM wala chama kingine cha siasa na sasa wanatambua kuwa SIASA si porojo (kama za CCM) bali ni maisha yao. Ndiyo maana waliweza kuthubutu kuamka usiku wa manane kwenda kujipanga kujiandikisha ili kupiga kura ya MABADILIKO uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Source: Makene.