rusha ni mji uliojaa wazungu kila Kona utafikiri tupo South Africa 🌍 na tushazoea kufanya biashara au mazungumzo ya hapa na pale na hawa wadoshi wakiwa hapa jijini.
Na wazungu wengi wao wamewekeza sana hapa. Asilimia kubwa sana ya wana Arusha pato Lao kubwa achia mbali madini la pili ni utalii.
Lakini kwa sasa hali ni tofauti kabisa urafikiri tupo singida au wap sijui hatuoni wazungu kabisa kabisa hata Ile migahawa wazungu hukaa hamna mtu mweupe hata kidogo.
Hotel, migahawa, na kule vinyagago na sehemu zote wazungu wanapopendelea kutembea au kukaa hamna kabisa watu weupe.
Makampuni mengi, migahawa, maduka na hata masoko wengi tunategemea utalii, sahiv kila mtu analia.