Arusha iachwe ichague!

Arusha iachwe ichague!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kuna habari za kila aina ya hila zinazolenga ima kuvuruga au kukwamisha Uchaguzi wa Arusha (uchaguzi wa Madiwani wa Kata nne) uliopangwa kufanyika tarehe 14/7/2013. Habari hizi,pamoja na kwamba zaweza kupuuzwa,lakini zizingatiwe.

Watu wa Arusha wameshasikiliza kampeni na sera za wagombea wa kata zote nne. Wamewaelewa. Wapigakura wako tayari.Tayari kupiga kura hapo tarehe 14/7/2013. Tayari kuchagua viongozi wawatakao. Tayari kuchagua wanamaendeleo. Arusha si Tanzania nzima.Kushinda au kushindwa Arusha si kushinda au kushindwa Tanzania nzima.

Nitoe rai kwa wadau wote wa uchaguzi huu kuwa wana-Arusha wanataka kuchagua na kupata viongozi wao. Mvurugaji yeyote wa uchaguzi huu kwa mara nyingine hatakuwa na nafasi. Arusha pakichafuliwa,patachafuka kweli. Vyama vyote vya siasa vikae tayari kukubali kuchaguliwa au kukataliwa. Vikilazimisha ushindi,vitajilaumu sana.

Na ni vyema,mwanzilishi wa vurugu(kama ikitokea)adhibitiwe ipasavyo. Kama si na vyombo vya dola basi na umma.Arusha,chagua sasa.Chagua maendeleo ya Arusha. Wapenda siasa safi tutailinda demokrasia ya Tanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Mkuu tatizo ni matumizi mabaya ya nafasi ya Mkuu wa Mkoa. Ebu mdhibitini mtu wenu; mnakuwaje na jitu Pinda Pinda kwenye mkoa wa walio na uelewa mkubwa? Maswala kuwa biashara zinaharibika kwa Arusha kuongozwa na Chadema mjiulize ni biashara za nani? Kwa sisi wana Arusha hizo biashara zikifa zote leo hatutakosa kula kuvaa maana tuna elimu ya kutosha ya kujitegemea, pia aina ya maisha yetu haihusiani kabisa na mtazamo wa CCM; ni huru. CCM wafanye wafanyalo tutachagua kwa hoja na imani kwa mgombea si kulazimishwa na kushinikizwa kwa sababu HATUNA CHA KUPOTEZA kwa kuikataa CCM.
 
Arusha hatuitaki ccm hilo ndio la muhimu kwetu....
 
Kuna habari za kila aina ya hila zinazolenga ima kuvuruga au kukwamisha Uchaguzi wa Arusha (uchaguzi wa Madiwani wa Kata nne) uliopangwa kufanyika tarehe 14/7/2013. Habari hizi,pamoja na kwamba zaweza kupuuzwa,lakini zizingatiwe.

Watu wa Arusha wameshasikiliza kampeni na sera za wagombea wa kata zote nne. Wamewaelewa. Wapigakura wako tayari.Tayari kupiga kura hapo tarehe 14/7/2013. Tayari kuchagua viongozi wawatakao. Tayari kuchagua wanamaendeleo. Arusha si Tanzania nzima.Kushinda au kushindwa Arusha si kushinda au kushindwa Tanzania nzima.

Nitoe rai kwa wadau wote wa uchaguzi huu kuwa wana-Arusha wanataka kuchagua na kupata viongozi wao. Mvurugaji yeyote wa uchaguzi huu kwa mara nyingine hatakuwa na nafasi. Arusha pakichafuliwa,patachafuka kweli. Vyama vyote vya siasa vikae tayari kukubali kuchaguliwa au kukataliwa. Vikilazimisha ushindi,vitajilaumu sana.

Na ni vyema,mwanzilishi wa vurugu(kama ikitokea)adhibitiwe ipasavyo. Kama si na vyombo vya dola basi na umma.Arusha,chagua sasa.Chagua maendeleo ya Arusha. Wapenda siasa safi tutailinda demokrasia ya Tanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

Arusha bila Ccm inawezekana
 
Wanaarusha musikubali hila za Kikwete na genge lake la mumiani anatangaza kwa kujivuna kabisa kupitia mwigulu anasema mulie musilie mutashindwa tuu manake nini kwa kwakweli kuna hatari kubwa panahitajika kumbomoa mkuu wa mkoa kwanza kiakili
 
Msmamo wa watu wa Arusha unajulikana.Utaoneshwa tarehe yoyote ya uchaguzi
 
Magesa Mulongo ni janga kwa Wana Arusha kilichopo ni kuandamana kumkataa, hata kama President hatamtoa immediately anaweza kufanya mabadiliko ya Wakuu wa mikoa ili kumg'oa maana mshikaji hanagamuamana yule...

Baada ya uchaguzi Plan iwe ni kumuondoa Magesa Mulongo kwa nguvu ya Umma,,,haiwezekani Mtu umeletwa tu then unataka kuwaondoa watu waliochaguliwa na wananchi kwa maslahi binafsi,,,,wana Arusha kwa umoja wenu semeni NO kwa Magesa Mulongo,,,anawaharibia jiji, anakwamisha maendeleo huyo

Mimi naanza MAGESSA MULONGO NOOOOOO,,,,wengine wafuatie
 
Back
Top Bottom