VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Nipo Arusha kwasasa kwa shughuli binafsi. Nitakwenda pia Manyara. Lakini, mwanasiasa haachi siasa. Nimejikuta nimefuatilia kilichojiri na kinachoonekana hapa Arusha kisiasa. Ninashuhudia CCM dhaifu kuliko mkoa wowote wa Tanzania Bara (kwakuwa Pemba inazidi). Nashuhudia CCM ikijifichaficha kufanya siasa na CHADEMA wakitamba watakavyo.
Nashuhudia kila kona,kila nyumba CCM ikibezwa na kumezwa. Kila kona, kila nyumba CCM inasemwa vibaya bila haya kwa kila mwanakaya. CCM ni kama haipo Arusha. CCM inanyanyasika vya kutosha na kutisha hapa Arusha. Nikawakumbuka wakuu mmaranguoriginal na sirluta. Jinsi wanavyojitahidi kufa na tai zao shingoni.
Kutokana na niyaonayo, nampongeza Bwana Mollel aliyekuwa mgombea wa CCM yetu hapa Arusha. Kwa kupata kura zaidi ya thelathini elfu. Bwana Mollel almaarufu kama MONABAN amekibeba vya kutosha chama chetu. Amekipunguzia aibu ya kupata kura kiduchu hapa Arusha.
Hakuna propaganda itakayoiponya CCM Arusha zaidi ya kuhuishwa. CCM Arusha wana kazi ya kufanya. Mkuu MUSSA ALLAN, tafadhali rudi kundini tukirejeshe chama chetu kwenye mstari hapa Arusha. CCM haistahili kupata manyanyaso ya aina hii. Ingawa Lema anakubalika, lakini nasi yatupasa kutikisa.
Kuna kazi kubwa ya kufanyika!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Last edited by a moderator: