Arusha: Hatutakubali uvujaji na upotevu wa mapato

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
287
1,000
Na Mwandishi Wetu

Wakati Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza iwapo Tanzania tutaziba mianya ya ukwepaji kodi, tutakusanya kodi kwa uaminifu na kuvuna utajiri wa rasilimali na maliasili tulizonazo kwa manufaa ya Taifa nchi yetu haina sababu ya kuwa ombaomba badala yake tutafanya mambo makubwa ikiwemo kuwa 'DONOR COUNTRY' yaani nchi inayoweza kutoa msaada kwa mataifa yenye uhitaji.

Msisitizo huu wa ukusanyaji wa mapato ameutoa pia kwa wakurugenzi wa halmashauri za miji, manispaa na majiji ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kifedha katika kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 pamoja na ahadi za Mhe Rais alizozitoa kwa wananchi wa maeneo yao wakati wa uchaguzi mkuu 2015.

Jiji la Arusha limeamua kutekeleza kwa vitendo maelekezo hayo ya Mhe Rais Dkt Magufuli kwa kusimamia kwa ufanisi miongozo na maagizo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia vikao vya baraza la madiwani katika ukusanyaji wa mapato ili kuijengea uwezo halmashauri yao katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dkt Maulid Suleiman Madeni amesema baada ya kufika ofisini alijipa muda wa kusoma mazingira na kujifunza mambo mengi juu ya jiji hilo ambapo alibaini fedha nyingi kupitia vyanzo vya mapato vya jiji hilo zinapotelea mifukoni mwa watu wachache. Anasisitiza akaamua kufanya mabadiliko madogo katika masoko kwa kuwabadilisha wakuu wa soko na kuleta sura na damu mpya.

"Matokeo yake ni kuwa mfano soko la Kilombero
mkuu wa soko aliyekuwepo alikuwa akikusanya kati ya shilingi 170,000-200,000 kwa siku sasa mkuu mpya wa soko kwa usimamizi madhubuti katika siku zake tatu za kazi hiyo amekusanya shilingi 1,345,500, 1,750,000 na 2,465,000" Amesema Dkt Maulid

Aliendelea kusisitiza lengo lake na watumishi wenzake wa jiji ni kuhakikisha wanaikidhi bajeti yao ya maendeleo kwa zaidi ya asilimia mia moja kwani kwa mwaka wa fedha 2018/19 bajeti yao ni bilioni 15 kwani kwa ushirikiano na mipango yao wanauhakika wanaweza kukusanya bilioni 16 au 17.

"Ili kuwaondolea kero wananchi wetu ambao wengi wao ni wanyonge ni lazima tukusanye vizuri mapato. Kwa kufanya hivyo watapata huduma bora na hata ile mikopo ya kina Mama na vijana nayo itatoka kwa kiwango kizuri zaidi na kuwafikia wengi." alisema Dkt Maulid

Dkt Maulid amemalizia kwa kuwataka watumishi wenzake kuendelea kuwajibika kwa nidhamu, uadilifu na uzalendo ili kulipa heshima jiji hilo. Pamoja na kuwa anawatembelea wananchi mara kwa mara katika maeneo yao ya biashara Dkt Maulid amewaomba wananchi wa jiji hilo la Arusha wasisite kufika ofisini kwake muda wowote wanapokutana na changamoto kwani hiyo ni ofisi yao na yeye ameletwa Arusha na Mhe Rais Dkt Magufuli kuja kuwatumikia hivyo milango ipo wazi muda wowote.

Arusha tupo kazini.
IMG_20190304_082250_612.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,348
2,000

Arusha tupo kazini. View attachment 1037359

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa mbona anauza nyago sana anataka ukuu wa mkoa nini?!!

Mrisho anatosha bhana!
 
Shapu

JF-Expert Member
Jan 17, 2008
2,090
2,000
Kuna barua niliona kaandika kwamba ile ada ya vitambulisho ya elfu 20 haihusiani na ushuru ndani ama katika mazingira ya soko ya shilingi mia tano. Sasa ikapelekea yule mtumishi kupata vizingiti kwa wale akina mama ndipo akaamua kuchukua video clip. Sasa alipoona kwamba video imeeda viral aka suggest yule mtumishi aende shule. Then jana tunaona ameenda kuomba msamaha wale akina mama. Ukiliangalia hili swala kwa makini tatizo ni huyu Mkurugenzi na alikiuka maagizo ya Raisi kupitia ile barua yake sasa anajaribu kujisafisha. Nashangaa kwa nini woga mkubwa hivi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom