Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Hali ya sintofahamu imetokea katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha Mount meru baada ya familia mbili kuchanganya miili ya marehemu familia ya Alpha Makundi ya Arusha ilipochukua mwili wa mtoto wa kike wa umri wa mwaka mmoja na miezi miwili wa familia ya Kamnde ya mkoani Kilimanjaro na kumzika Sokoni one jijini Arusha hali iliyo ilazimu familia ya Elimbise Kamnde kwenda kuufukua mwili wa mtoto wao na kwenda kuzika tena Moshi Kilimanjaro na familia Makundi kuanza upya taratibu wa maziko ya mwili wa mtoto wao wa kiume Valentino Makundi wa miezi tano.
Familia ya Elimbise Kamande ya mkoani Kilimanjaro ilitaka kuchukua mwili wa mtoto wao Brian mwenye jinsia ya kike na kupewa mwili wa mtoto wa kiume ndipo sakata lilipoanza na baadae wahudumu wa chumba hicho wakagundua kuwa wamechanganya miili kisha safari ya kwenda Sokoni one kufukua mwili ikawadia huku wazazi wakiwatupia lawama wahuduma wa chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospiali ya Mountmeru.
Baada ya taaruki kubwa kuwapata wakazi wa Sokoni one kwa kutoamini kilichotokea Mwenyekiti wa mtaa wa Lolovono akalazimika kuwatuliza wakazi hao huku mwangalizi wa mochuari Dk Lemweli Makando akizungumza kwa shariti la kutopigwa picha.
Chanzo: ITV