ARUSHA: Ewura yatangaza kushuka Kwa Bei ya mafuta ya Dizeli

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
ARUSHA


Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (Ewura)imetangaza kupungua Kwa Bei ya mafuta ya Dizeli Kwa kiasi cha Sh 18 kwa Lita Moja mwezi huu.


Wakati Bei ya Dizeli ikipungua ,Bei ya mafuta ya petrol itaendelea kubaki pale pale .


Akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha, mkurugenzi mkuu Ewura , Mhandisi Godfrey Chibulunje alisema mabadiliko hayo ni Kwa mafuta yaliyopokelewa Kwa bandari ya dar es salaam pekee na Bei hiyo utaanza kutumika hapo kesho Novemba 3 mwaka huu.


Mhandisi Chibulunje alifafanua kuwa tangu mwezi wa Tisa mwaka huu,Ewura ilisimamisha Bei na kuendelea kutumika Bei za mwezi Agost na Serikali iliendelea kuangalia namna ya kupunguza tozo mbalimbali ili kuleta unafuu Kwa wananchi.


Alisema Oktoba 5 mwaka huu Rais Samia Suluhu alielekeza tozo mbalimbali zipunguzwe ambapo kiasi cha sh,bilioni 102 Kwa mwaka kimeondolewa


Mhandisi Chibulunje alisema kuwa pamoja nanjuhudi mbalimbali za serikali lakini Bei ya mafuta katika soko la dunia imeendelea kupanda ambapo Mei mwaka Jana Bei ya pipa Moja ya mafuta ghafi ilikuwa Dola 32 ,lakini hadi kufikia Oktoba mwaka 2021 Bei ya pipa imefika Dola za kimarekani 86.


Alisema Kutokana na juhudi za serikali kuondoa tozo mbalimbali Bei ya Dizeli imeshuka Kwa sh, 18 kwa bandari ya Dar es salaam ambapo Bei iliyokuwa ikitumia mwezi uliopita ilikuwa ni sh, 2261 lakini Kwa mwezi huu Novemba Bei imeshuka na kufikia kiasi cha sh, 2243.


"Bei zingine zitabaki vilevile sh,2439 Kwa Lita Moja ya mafuta ya petrol na kama Serikali isingeingilia Kati Bei ya petrol Kwa mwezi huu Novemba ilitakiwa iwe sh, 2492"alisema



Alisema Kwa mwezi Novemba Bei ya Mafuta ya Petrol itaendelea kubaki sh, 2439 ,ila bei ya mafuta ya Taa Kwa bandari ya Dar es salaam itaendelea kuwa sh, 2188 kwa lita.


Alisema kwa bandari ya Tanga na Mtwara Bei za mafuta zitabaki kuuzwa Kwa Bei ile ile ya mwezi uliopita.


Ends...






IMG_20211102_141419_839.jpg
 
18 x 10ltrs =180 tax au bodaboda.
18 x 70ltrs =1260 daladala nk.
Punguzo la bei kutoka sasa.

Okay.

 
Mbona imepanda ukilinganisha na mwezi uliopita ...au wana maana gani
 
Back
Top Bottom