Arusha City: My perspective...

Arusha City: My perspective...

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
906
JICHO LANGU LA UCHAMBUZI, NILIPO KUWA JIJINI ARUSHA. (THE GENEVA OF AFRICA)

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Tuesday -18/6/2019.
Karatu DC, Manyara - Tanzania.

Jiji la Arusha ni sehemu yote ya wilaya ya Arusha ndani ya mkoa wa Arusha, Eneo la jiji hilo lilianzishwa rasmi tarehe 1, Julai 2005 kupitia tangazo maalumu la rais Benjamin Mkapa.

Mji wa Arusha ambao leo ndio sehemu ya jiji la Arusha ilianzishwa kama mji mwaka 1948 (Incorporated Town) chini ya utawala wa ukoloni wa Kingereza. Jiji hili ni maarufu sana kwa utalii na shughuli za kidplomasia, hasa jiji hili hufahamika kama "Geneva of Africa" (yani Geneva ya Afrika).

Kutoka mkoa wa Kilimanjaro yani Moshi mjini mpaka jiji la Arusha ni Km 80.1 ambayo huchukua saa 2 kwa usafiri wa basi na 2:30 kwa usafiri wa Costa, Ikiwa utaingia Arusha kwa usafiri wa ndege itakuchukua nusu saa tu (dk30) kutoka Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambao umbali wake kutoka uwanja huo mpaka jijini Arusha ni 55 Km.

Tarehe 9/6/2019 nilianza ziara yangu ya utembezi katika jiji la Arusha, ziara yangu hii ilifatia baada ya kukamilisha ziara binafsi ya mji wa Namanga kutokea Kenya.

nilipokuwa Arusha nilipata wasaa wa kujifunza mengi sana, pamoja na kupata fursa ya kuwatembelea baadhi ya rafiki zangu ambao tulisoma wote chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa sasa wengi wapo Arusha kishughuli, moja ya rafiki yangu ambae tulikutana na kuzungumza mengi kwa upana pamoja na kupeana fursa mbali mbali ni Wakili (advocate) Gadi Silasi ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa kampuni ya mawakili ya Grobal advocate company iliyopo mtaa wa Kaloleni umbali wa Km 1.8 kutoka kati kati ya jiji la Arusha.

Nje ya hilo nilipata fursa ya kujifunza mambo kadhaa juu ya jiji la Arusha, jiji ambalo ndio jiji la 3 kwa ukubwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha jiji hilo lina idadi ya wakazi wa Wilaya ya Arusha Mjini (Jiji la Arusha) kuwa inafikia 416,442, idadi ambayo huifanya kuwa jiji la pili kwa idadi ya watu wengi nyuma ya Dar es salaam.

Jiji hili limezungukwa na baadhi ya maandhari mazuri sana ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama, jiji lipo kando ya Mlima Meru kwenye upande wa mashariki mwa Bonde la Ufa, lakini kubwa zaidi kuna mbuga ya wanyama ya Arusha (Arusha national park) katika upande wa kaskazini mashariki, Ikumbukwe kuwa jiji la Arusha ndio jiji pekee Tanzania ambalo mbuga ya wanyama ipo mjini na jiji la pili Afrika kuwa na mbuga ya wanyama katikati ya jiji nyuma ya jiji la Nairobi nchini Kenya.

Hali ya hewa ya jiji hili ni nzuri sana. Mbuga zingine za wanyama za Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo karibu kuzunguka jiji hilo, hivyo kuifanya Arusha kuwa kitovu cha utalii na eneo muhimu katika soko la utalii nchini.

Lakini pia jambo moja la kufurahisha katika nyanja za kidplomasia katika jiji hili la Arusha ni kwamba jiji hili ndio makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu na Mahakama ya Afrika Mashariki huku kuanzia mwaka 1994 mjı huu ulifanywa kuwa makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR).

Pia jiji la Arusha lipo katika mwinuko wa mita 1400 kusini mwa Mlima Meru, jambo ambalo hufanya hali ya hewa ya jiji hili kuwa yenye ubaridi na unyevu mwingi. Viwango vya joto huwa katika wastan wa kati ya nyuzi joto 13 mpaka 30, Ina nyakati tofauti za mvua na ukame na huwa inakumbwa na upepo wa msimu unaovuma toka Bahari ya Hindi mashariki kusini mwa jiji hili.

Moja ya vivutio vikubwa vya kihistoria katika jiji la Arusha ni pamoja na "Hati za uhuru wa Tanganyika" zilitiwa sahihi na Uingereza mwaka 1961 jijini Arusha huku pia Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitshwa katika jiji hili mwaka 1967 na serikali ya kwanza ya Tanzania chini ya baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere katika maeneo maarufu ya mnara wa saa yaliyopo kati kati ya jiji.

Nje ya hayo pia makubaliano ya "Arusha Accords" ya kusitisha vita nchini Rwanda na Burundi yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993, jambo ambalo ina ifanya jiji la Arusha kuwa jiji la kipekee nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuwa mji wa kidplomasia na mashirikiano ya kimataifa.

Kiuchumi mkoa wa Arusha unatagemea sana shughuli za kilimo, hasa uzalishaji wa maua na mbogamboga (flowers and vegetables) ambao soko kubwa la mazao hayo ni Ulaya. Lakin pia kaskazini mwa jiji hilo na mkoa wote wa Arusha hulima kahawa pia, japo kuwa wakulima wengi wadogo wadogo wa kahawa waliathiriwa vibaya na mgogoro wa kahawa wa miaka ya karibuni katika soko la dunia. Nje ya kilimo pia jiji la Arusha lina viwanda kadhaa kwa mfano viwanda vya tairi, mimea na madawa.

Pia mkoa wa Arusha ni chanzo pekee cha madini ya Tanzanite duniani, madini haya yanazalishwa kwa wingi sana na makampuni kadhaa ya madini ikiwa ni pamoja na kampuni ya Tanzanite one.

Utalii pia unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa jiji la Arusha karibu 56% ya mapato ya mkoa na jiji hilo inachangiwa na sekta ya utalii, utalii mkoani Arusha inachukua nafasi ya pili kwa mchango wa mapato Tanzania (GDP income). Hii ni kutokana na eneo la jiji kuwa karibu na vivutio maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro uliopo mkoa wa Kilimanjaro, Serengeti na Ngorongoro, Arusha pia imekuwa maarufu kwa watalii wanaotembelea Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii katika mikoa ya karibu.

Changamoto za jiji la Arusha.

Changamoto zilizopo katika jiji hili ni pamoja na miundombinu mibovu katika sehemu nyingi za viunga vya jiji hili, uchafu wa mazingira, usalama mdogo na ukosefu wa ubunifu katika kuendeleza jiji hilo.

Mfano tu ni kuwa barabara ya kutoka Mromboo kuja mtaa wa Mbauda ni nyembamba sana kitu kinacho pelekea msongamano mkubwa wa magari hasa eneo la Kona ya Mbauda, pia barabara za Mureti, Ngaramtoni, Ngaranyuki na ile barabara inayoenda kiwanda cha "Nation Mill" imechakaa jambo linalopelekea usumbufu hasa kipindi cha masika pale mvua inaponyesha.

Soko la Kilombero limekuwa eneo linalo ongoza kwa uchafu katika eneo la katikati ya jiji la Arusha, ni jambo la kawaida kukuta harufu ya uchafu ukiwa mkabala na soko hilo, pia masoko ya jioni yaliyopo pale Mbauda na pale eneo la Mrombo ni hatari Sana kwa afya hasa eneo la nyama choma kando ya barabara ya kwa Mrombo.

Uchafu wa mazingira katika mitaa ya Ngaramtoni na Ngarenaro ni ishara ya umakini mdogo katika usafi wa mazingira na utunzaji wa mazingira katika jiji hilo. Baadhi ya mitaa kama Sakina, Kaloleni na barabara ya Nairobi wanafanya vizuri katika usafi wa jiji hilo.

Kero nyingine kubwa jijini Arusha ni stendi ya mabasi na daladala kuwa katikati ya jiji na kusababisha msongamano mkubwa wa magari na mabasi ambayo hulazimika kuingia katikati ya jiji bila ulazima wowote, kero nyingine ambayo niliipata ni baada ya kuzungumza na wafanya biashara wa mazao wanao toka mikoani ni kuhusu "Mzani" wa halmashauri ulipo karibu na soko la Kilombero.

Mzani umekuwa kero nyingine kubwa kwa kusababisha msongamano wa barabara hiyo inayo ingia jijini kwa sababu ya maroli na fuso nyingi kulazimika kuingia kupima katika mzani huo, kitu ambacho ingeweza kuwekwa nje ya mji na kupelekea kupunguza msongamano eneo hilo.

Changamoto nyingine ni usalama mdogo hasa maeneo mengi ya jiji kuwa na uwezo mdogo wa kukabiliana na uhalifu, ukosefu wa fursa hasa za utalii kwa wakaazi wa Arusha ni moja ya sababu ya kuwepo wimbi la ukosefu wa ajira jambo ambalo lingeweza kupunguzwa pakubwa sana kama mamlaka husika zingeweza kuwekeza katika kuinua fursa za utalii kwa ushiriki pamoja na jamii ya jiji na mkoa huo kwa ujumla.

Nini Maoni Yangu?

Kwanza naishauri mamlaka ya jiji kuihamisha stendi kuu ya mabasi katikati ya jiji kuipeleka nje ya jiji kwa kutenga maeneo ya stendi ya mabasi yatokanayo Dar es salaam na maeneo ya mashariki ya Arusha kuwa na stendi yao eneo la barabara ya Moshi, huku stendi ya mabasi yatokanayo Mwanza na maeneo ya magharibi ya nchi na yale yanayotoka Kenya kuwa na stendi yao barabara ya Mwanza, Kama ilivyo jiji la Mwanza kuwa na stendi ya Nyegezi kwa mabasi yote yatokayo Dar es salaam na mikoa mwingine ya mashariki mwa nchi na ile ya Nyakato Buzuruga kwa mabasi yote yatakayo Musoma, na nchini Kenya.

Pili naishauri mamlaka kukarabati na kupanua barabara za Mrombo,Mbauda,Mureti,Ngarenaro na ile ya kuingia mjini kwenda kituo cha "Chini ya mti"

Tatu naishauri mamlaka kuongeza nguvu ya usafi katika maeneo korofi kwa uchafu wa mazingira kwa kuongeza magari ya taka, kuongeza siku za kuzoa taka kutoka tatu mpaka moja (yani uchafu uweze kuondolewa kila siku asubuhi hasa soko la kilombero) na pia kuongeza nguvu kazi za watu katika sekta ya usafi ikiwa ni pamoja na kutunga kanuni za jiji juu ya utunzaji mazingira na usafi wa jiji.

Jambo jingine naloweza kuishauri halmashauri ya jiji la Arusha ni kuweka mkakati wa kuziondoa Haice kama daladala na badala yake waanze kuruhusu Costa kufanya kazi mbadala wa hiace kwa mjini ili kupunguza hadha ya usafiri na ustaarabu wa kugombania usafiri kwakuwa hiace ni ndogo hivyo ulazimika kuchukua abiria wachache.

Kingine ambacho ni muhimu ni mipango miji ili kuufanya jiji la Arusha kuendana na hadhi ya jiji hilo, mpangilio wa jiji ni muhimu kwa jiji lolote lile la kisasa katika ustawi wake.

Fursa Jijini Arusha.

Katika fursa za uwekezaji jijini Arusha ni viwanda vya Saruji, Nondo, Mabati na vifaa vya ujenzi kwa ujumla hii ni kutokana na mahitaji makubwa ya vifaa vya ujenzi katika jiji hilo kutokana na ungezeko kubwa la wakaaji linalo endana na kasi ya ujenzi katika jiji hilo.

Pia mahitaji ya chakula kama nafaka ni makubwa sana hasa mchele, mahindi, Maharagwe, Njugu, karanga, na Mtama, Nilizungumza na wafanyabiashara wa soko la nafaka la Mbauda wengi wao walisema kuwa kwa siku moja zaidi ya jumla ya tani 8 ya mchele, tani 4 ya maharagwe, tani 9 ya mahindi na 5 ya karanga hutoka kwenye soko lao kila siku huku hii Ikiwa ni idadi ndogo kulingana na mahitaji ya walaji wa jiji hilo.

Kwa maelezo ya wafanya biashara hao wanadai kuwa idadi hiyo ni 47% ya mahitaji yao yote ya chakula jijini humo, natumai kupitia machache haya mkuu wangu wa mkoa wa Arusha kaka yangu Mrisho Gambo atayapokea haya na kuyafanyia kazi kama changamoto ili kutatua matatizo haya kwa lengo la kuufanya mji wa Arusha kuwa jiji la kisasa.

Nitaendelea kuwaletea "Jicho langu la Uchambuzi", katika maeneo na sehemu nilizo tembelea katika ziara yangu hii inayoendelea.

Asanteni

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu.

Mawasiliano:
+255679555526
FB_IMG_1560866715752.jpeg
 
Kuna mkakati wa kujenga stendi mbili kubwa maeneo ya Olasiti na Moshono, ile ya olasiti ni magari yote yatakayokuwa yanaingia kutokea njia ya Dodoma na ile ya moshono ni magari yatakayokuwa yanatokea njia ya Moshi. Tatizo la ucheleweshwaji wa stand hizi ni siasa tu, jiji kuwa na mbunge wa upinzani serikali imechukua kama fimbo ya kuzorotesha maendeleo ya jiji.
 
umbali kutoka moshi mjn hadi arusha mjn ni km 85 tuu na mwendo wa bus/coaster ni angalau saa 1.5 tuu

kwa sasa ni sahihi kabisa mtu kusema miji hiyo miwili imeungana...yaani kutoka mji mmoja kuelekea mwingne ni makazi ya watu mwanzo mwisho, hakuna mapori.
 
Madini ya tanzanite yapo mererani ambapo zamani ilikuwa ni Arusha ila now imekuwa mkoa wa Manyara, baada ya Arusha kugawanywa na kuwa mikoa miwili yaani Arusha na Manyara

Ila mkoa mzuri lakini issue ya uchafu kweli waiangalie kwa jicho la tofauti na iisue ya barabara
 
"Nje ya hilo nilipata fursa ya kujifunza mambo kadhaa juu ya jiji la Arusha, jiji ambalo ndio jiji la 3 kwa ukubwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha jiji hilo lina idadi ya wakazi wa Wilaya ya Arusha Mjini (Jiji la Arusha) kuwa inafikia 416,442, idadi ambayo huifanya kuwa jiji la pili kwa idadi ya watu wengi nyuma ya Dar es salaam"

Sidhani kama hizi taarifa ya Arusha kuwa na population kuzidi Mwanza kama zipo sahihi.
 
umbali kutoka moshi mjn hadi arusha mjn ni km 85 tuu na mwendo wa bus/coaster ni angalau saa 1.5 tuu

kwa sasa ni sahihi kabisa mtu kusema miji hiyo miwili imeungana...yaani kutoka mji mmoja kuelekea mwingne ni makazi ya watu mwanzo mwisho, hakuna mapori.
Ilitakiwa kujenga barabara ya njia 6 kutoka Moshi hadi Arusha sio hako ka kichochoro cha East Africa wanachojenga.
 
Umbali wa Moshi to Arusha ni 80km.
Ukifuata mwendo wa basi kubwa kama hakuna foleni njiani unatumia dakika 80 mpaka 90.

Mwendo uliotaja hapo labda coaster ambayo imeanza safari ikiwa na abilia 7 so inaokoteza njiani.
 
Pale sokoni Kilombero ni hatari kwa uchafu tena usuombe uingie kule kipindi cha mvua, huwa najiuliza jiji la Arusha halina bwana afya. Kingine ni wamama kupanga bidhaa za chakula chini hasa nyakati za jioni hasa ili barabara ya mianzin kuelekea ilboru kwa kweli Arusha inatia aibu sana utadhani viongozi wa mkoa hawaoni hii hali. Stendi ya kilombero pale ni vumbi tupu na ipo mjini kabisa.
 
"Nje ya hilo nilipata fursa ya kujifunza mambo kadhaa juu ya jiji la Arusha, jiji ambalo ndio jiji la 3 kwa ukubwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha jiji hilo lina idadi ya wakazi wa Wilaya ya Arusha Mjini (Jiji la Arusha) kuwa inafikia 416,442, idadi ambayo huifanya kuwa jiji la pili kwa idadi ya watu wengi nyuma ya Dar es salaam"

Sidhani kama hizi taarifa ya Arusha kuwa na population kuzidi Mwanza kama zipo sahihi.
Yuko sahihi ila nadhani mtoa mada kuna baadhi ya maneno aliruka ambapo kulingana na google inasema "wilaya ya arusha mjini (jiji la arusha) inafikia idadi ya wakazi 416,442 pamoja na wilaya inayozunguka ya arusha dc inafikia 323,198 idadi ambayo huifanya kuwa ya pili kwa watu wengi nyuma ya jiji la Dar es salaam"
 
"Nje ya hilo nilipata fursa ya kujifunza mambo kadhaa juu ya jiji la Arusha, jiji ambalo ndio jiji la 3 kwa ukubwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha jiji hilo lina idadi ya wakazi wa Wilaya ya Arusha Mjini (Jiji la Arusha) kuwa inafikia 416,442, idadi ambayo huifanya kuwa jiji la pili kwa idadi ya watu wengi nyuma ya Dar es salaam"

Sidhani kama hizi taarifa ya Arusha kuwa na population kuzidi Mwanza kama zipo sahihi.
Weka taarifa sahihi
 
Mleta uzi kakosea mambo mengi sana kwenye uzi wake moja wapo ni hilo nahisi hakufanya utafiti wa kutosh, ila kwa swala la stendi na uchafu wa soko la Kilombero namuunga mkono.
 
Kabisa kwa stendi ya kilombero ni aibu kubwa kusema kuna uongozi
 
"Nje ya hilo nilipata fursa ya kujifunza mambo kadhaa juu ya jiji la Arusha, jiji ambalo ndio jiji la 3 kwa ukubwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha jiji hilo lina idadi ya wakazi wa Wilaya ya Arusha Mjini (Jiji la Arusha) kuwa inafikia 416,442, idadi ambayo huifanya kuwa jiji la pili kwa idadi ya watu wengi nyuma ya Dar es salaam"

Sidhani kama hizi taarifa ya Arusha kuwa na population kuzidi Mwanza kama zipo sahihi.
Ni sahihi kwa halmashauri ya majiji Arusha ni ya pili nje ya Dar
 
JICHO LANGU LA UCHAMBUZI, NILIPO KUWA JIJINI ARUSHA. (THE GENEVA OF AFRICA)

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Tuesday -18/6/2019.
Karatu DC, Manyara - Tanzania.

Jiji la Arusha ni sehemu yote ya wilaya ya Arusha ndani ya mkoa wa Arusha, Eneo la jiji hilo lilianzishwa rasmi tarehe 1, Julai 2005 kupitia tangazo maalumu la rais Benjamin Mkapa.

Mji wa Arusha ambao leo ndio sehemu ya jiji la Arusha ilianzishwa kama mji mwaka 1948 (Incorporated Town) chini ya utawala wa ukoloni wa Kingereza. Jiji hili ni maarufu sana kwa utalii na shughuli za kidplomasia, hasa jiji hili hufahamika kama "Geneva of Africa" (yani Geneva ya Afrika).

Kutoka mkoa wa Kilimanjaro yani Moshi mjini mpaka jiji la Arusha ni Km 107.1 ambayo huchukua saa 2 kwa usafiri wa basi na 2:30 kwa usafiri wa Costa, Ikiwa utaingia Arusha kwa usafiri wa ndege itakuchukua nusu saa tu (dk30) kutoka Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambao umbali wake kutoka uwanja huo mpaka jijini Arusha ni 60 Km.

Tarehe 9/6/2019 nilianza ziara yangu ya utembezi katika jiji la Arusha, ziara yangu hii ilifatia baada ya kukamilisha ziara binafsi ya mji wa Namanga kutokea Kenya.

nilipokuwa Arusha nilipata wasaa wa kujifunza mengi sana, pamoja na kupata fursa ya kuwatembelea baadhi ya rafiki zangu ambao tulisoma wote chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa sasa wengi wapo Arusha kishughuli, moja ya rafiki yangu ambae tulikutana na kuzungumza mengi kwa upana pamoja na kupeana fursa mbali mbali ni Wakili (advocate) Gadi Silasi ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa kampuni ya mawakili ya Grobal advocate company iliyopo mtaa wa Kaloleni umbali wa Km 1.8 kutoka kati kati ya jiji la Arusha.

Nje ya hilo nilipata fursa ya kujifunza mambo kadhaa juu ya jiji la Arusha, jiji ambalo ndio jiji la 3 kwa ukubwa nchini Tanzania, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 inaonesha jiji hilo lina idadi ya wakazi wa Wilaya ya Arusha Mjini (Jiji la Arusha) kuwa inafikia 416,442, idadi ambayo huifanya kuwa jiji la pili kwa idadi ya watu wengi nyuma ya Dar es salaam.

Jiji hili limezungukwa na baadhi ya maandhari mazuri sana ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama, jiji lipo kando ya Mlima Meru kwenye upande wa mashariki mwa Bonde la Ufa, lakini kubwa zaidi kuna mbuga ya wanyama ya Arusha (Arusha national park) katika upande wa kaskazini mashariki, Ikumbukwe kuwa jiji la Arusha ndio jiji pekee Tanzania ambalo mbuga ya wanyama ipo mjini na jiji la pili Afrika kuwa na mbuga ya wanyama katikati ya jiji nyuma ya jiji la Nairobi nchini Kenya.

Hali ya hewa ya jiji hili ni nzuri sana. Mbuga zingine za wanyama za Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Tarangire na mlima Kilimanjaro zipo karibu kuzunguka jiji hilo, hivyo kuifanya Arusha kuwa kitovu cha utalii na eneo muhimu katika soko la utalii nchini.

Lakini pia jambo moja la kufurahisha katika nyanja za kidplomasia katika jiji hili la Arusha ni kwamba jiji hili ndio makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu na Mahakama ya Afrika Mashariki huku kuanzia mwaka 1994 mjı huu ulifanywa kuwa makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR).

Pia jiji la Arusha lipo katika mwinuko wa mita 1400 kusini mwa Mlima Meru, jambo ambalo hufanya hali ya hewa ya jiji hili kuwa yenye ubaridi na unyevu mwingi. Viwango vya joto huwa katika wastan wa kati ya nyuzi joto 13 mpaka 30, Ina nyakati tofauti za mvua na ukame na huwa inakumbwa na upepo wa msimu unaovuma toka Bahari ya Hindi mashariki kusini mwa jiji hili.

Moja ya vivutio vikubwa vya kihistoria katika jiji la Arusha ni pamoja na "Hati za uhuru wa Tanganyika" zilitiwa sahihi na Uingereza mwaka 1961 jijini Arusha huku pia Azimio la Arusha la kujitegemea lilipitshwa katika jiji hili mwaka 1967 na serikali ya kwanza ya Tanzania chini ya baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere katika maeneo maarufu ya mnara wa saa yaliyopo kati kati ya jiji.

Nje ya hayo pia makubaliano ya "Arusha Accords" ya kusitisha vita nchini Rwanda na Burundi yalipitishwa mjini Arusha mwaka 1993, jambo ambalo ina ifanya jiji la Arusha kuwa jiji la kipekee nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuwa mji wa kidplomasia na mashirikiano ya kimataifa.

Kiuchumi mkoa wa Arusha unatagemea sana shughuli za kilimo, hasa uzalishaji wa maua na mbogamboga (flowers and vegetables) ambao soko kubwa la mazao hayo ni Ulaya. Lakin pia kaskazini mwa jiji hilo na mkoa wote wa Arusha hulima kahawa pia, japo kuwa wakulima wengi wadogo wadogo wa kahawa waliathiriwa vibaya na mgogoro wa kahawa wa miaka ya karibuni katika soko la dunia. Nje ya kilimo pia jiji la Arusha lina viwanda kadhaa kwa mfano viwanda vya tairi, mimea na madawa.

Pia mkoa wa Arusha ni chanzo pekee cha madini ya Tanzanite duniani, madini haya yanazalishwa kwa wingi sana na makampuni kadhaa ya madini ikiwa ni pamoja na kampuni ya Tanzanite one.

Utalii pia unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa jiji la Arusha karibu 56% ya mapato ya mkoa na jiji hilo inachangiwa na sekta ya utalii, utalii mkoani Arusha inachukua nafasi ya pili kwa mchango wa mapato Tanzania (GDP income). Hii ni kutokana na eneo la jiji kuwa karibu na vivutio maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro uliopo mkoa wa Kilimanjaro, Serengeti na Ngorongoro, Arusha pia imekuwa maarufu kwa watalii wanaotembelea Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii katika mikoa ya karibu.

Changamoto za jiji la Arusha.

Changamoto zilizopo katika jiji hili ni pamoja na miundombinu mibovu katika sehemu nyingi za viunga vya jiji hili, uchafu wa mazingira, usalama mdogo na ukosefu wa ubunifu katika kuendeleza jiji hilo.

Mfano tu ni kuwa barabara ya kutoka Mromboo kuja mtaa wa Mbauda ni nyembamba sana kitu kinacho pelekea msongamano mkubwa wa magari hasa eneo la Kona ya Mbauda, pia barabara za Mureti, Ngaramtoni, Ngaranyuki na ile barabara inayoenda kiwanda cha "Nation Mill" imechakaa jambo linalopelekea usumbufu hasa kipindi cha masika pale mvua inaponyesha.

Soko la Kilombero limekuwa eneo linalo ongoza kwa uchafu katika eneo la katikati ya jiji la Arusha, ni jambo la kawaida kukuta harufu ya uchafu ukiwa mkabala na soko hilo, pia masoko ya jioni yaliyopo pale Mbauda na pale eneo la Mrombo ni hatari Sana kwa afya hasa eneo la nyama choma kando ya barabara ya kwa Mrombo.

Uchafu wa mazingira katika mitaa ya Ngaramtoni na Ngarenaro ni ishara ya umakini mdogo katika usafi wa mazingira na utunzaji wa mazingira katika jiji hilo. Baadhi ya mitaa kama Sakina, Kaloleni na barabara ya Nairobi wanafanya vizuri katika usafi wa jiji hilo.

Kero nyingine kubwa jijini Arusha ni stendi ya mabasi na daladala kuwa katikati ya jiji na kusababisha msongamano mkubwa wa magari na mabasi ambayo hulazimika kuingia katikati ya jiji bila ulazima wowote, kero nyingine ambayo niliipata ni baada ya kuzungumza na wafanya biashara wa mazao wanao toka mikoani ni kuhusu "Mzani" wa halmashauri ulipo karibu na soko la Kilombero.

Mzani umekuwa kero nyingine kubwa kwa kusababisha msongamano wa barabara hiyo inayo ingia jijini kwa sababu ya maroli na fuso nyingi kulazimika kuingia kupima katika mzani huo, kitu ambacho ingeweza kuwekwa nje ya mji na kupelekea kupunguza msongamano eneo hilo.

Changamoto nyingine ni usalama mdogo hasa maeneo mengi ya jiji kuwa na uwezo mdogo wa kukabiliana na uhalifu, ukosefu wa fursa hasa za utalii kwa wakaazi wa Arusha ni moja ya sababu ya kuwepo wimbi la ukosefu wa ajira jambo ambalo lingeweza kupunguzwa pakubwa sana kama mamlaka husika zingeweza kuwekeza katika kuinua fursa za utalii kwa ushiriki pamoja na jamii ya jiji na mkoa huo kwa ujumla.

Nini Maoni Yangu?

Kwanza naishauri mamlaka ya jiji kuihamisha stendi kuu ya mabasi katikati ya jiji kuipeleka nje ya jiji kwa kutenga maeneo ya stendi ya mabasi yatokanayo Dar es salaam na maeneo ya mashariki ya Arusha kuwa na stendi yao eneo la barabara ya Moshi, huku stendi ya mabasi yatokanayo Mwanza na maeneo ya magharibi ya nchi na yale yanayotoka Kenya kuwa na stendi yao barabara ya Mwanza, Kama ilivyo jiji la Mwanza kuwa na stendi ya Nyegezi kwa mabasi yote yatokayo Dar es salaam na mikoa mwingine ya mashariki mwa nchi na ile ya Nyakato Buzuruga kwa mabasi yote yatakayo Musoma, na nchini Kenya.

Pili naishauri mamlaka kukarabati na kupanua barabara za Mrombo,Mbauda,Mureti,Ngarenaro na ile ya kuingia mjini kwenda kituo cha "Chini ya mti"

Tatu naishauri mamlaka kuongeza nguvu ya usafi katika maeneo korofi kwa uchafu wa mazingira kwa kuongeza magari ya taka, kuongeza siku za kuzoa taka kutoka tatu mpaka moja (yani uchafu uweze kuondolewa kila siku asubuhi hasa soko la kilombero) na pia kuongeza nguvu kazi za watu katika sekta ya usafi ikiwa ni pamoja na kutunga kanuni za jiji juu ya utunzaji mazingira na usafi wa jiji.

Jambo jingine naloweza kuishauri halmashauri ya jiji la Arusha ni kuweka mkakati wa kuziondoa Haice kama daladala na badala yake waanze kuruhusu Costa kufanya kazi mbadala wa hiace kwa mjini ili kupunguza hadha ya usafiri na ustaarabu wa kugombania usafiri kwakuwa hiace ni ndogo hivyo ulazimika kuchukua abiria wachache.

Kingine ambacho ni muhimu ni mipango miji ili kuufanya jiji la Arusha kuendana na hadhi ya jiji hilo, mpangilio wa jiji ni muhimu kwa jiji lolote lile la kisasa katika ustawi wake.

Fursa Jijini Arusha.

Katika fursa za uwekezaji jijini Arusha ni viwanda vya Saruji, Nondo, Mabati na vifaa vya ujenzi kwa ujumla hii ni kutokana na mahitaji makubwa ya vifaa vya ujenzi katika jiji hilo kutokana na ungezeko kubwa la wakaaji linalo endana na kasi ya ujenzi katika jiji hilo.

Pia mahitaji ya chakula kama nafaka ni makubwa sana hasa mchele, mahindi, Maharagwe, Njugu, karanga, na Mtama, Nilizungumza na wafanyabiashara wa soko la nafaka la Mbauda wengi wao walisema kuwa kwa siku moja zaidi ya jumla ya tani 8 ya mchele, tani 4 ya maharagwe, tani 9 ya mahindi na 5 ya karanga hutoka kwenye soko lao kila siku huku hii Ikiwa ni idadi ndogo kulingana na mahitaji ya walaji wa jiji hilo.

Kwa maelezo ya wafanya biashara hao wanadai kuwa idadi hiyo ni 47% ya mahitaji yao yote ya chakula jijini humo, natumai kupitia machache haya mkuu wangu wa mkoa wa Arusha kaka yangu Mrisho Gambo atayapokea haya na kuyafanyia kazi kama changamoto ili kutatua matatizo haya kwa lengo la kuufanya mji wa Arusha kuwa jiji la kisasa.

Nitaendelea kuwaletea "Jicho langu la Uchambuzi", katika maeneo na sehemu nilizo tembelea katika ziara yangu hii inayoendelea.

Asanteni

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu.

Mawasiliano:
+255679555526View attachment 1131436
Wewe ni msomi uchwara. Karatu haiko Manyara.
 
Moshi - Arusha ni kilometa 107?? Halafu masaa mawili na nusu? Mwongo sana.
 
Back
Top Bottom