Jamani asanteni sana, nami nilikuwa abiria mmojawapo humo. Na nimeahirisha na safari nipo hapa Arusha, tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda sote japo dereva wetu na wengine watatu walipelekwa hospitali Tengeru. Aisee nimejifunza mengi sana kupitia tukio hili, jamani nyie wenye simu kubwa msipende kupiga picha kabla ya kuokoa watu. Wakati tumemaliza kuruka madirishani wengine pale Mbele.
.dereva alikuwa amebanwa hakuweza kutoka hivyo alibakia palepale lakini cha ajabu watu wengi walikuwa busy kupiga picha na vijana wengine walikuwa wanatafuta mali za kuiba...jamani nafsi za watu tuzipe uzito na tusaidie wengine na sio kukimbilia kupiga picha.
Traffic wa barabarani jamani wasaidieni abiria kwa kudhibiti magari asubuhi...wanachokifanya madereva wanawahi kutoka stendi alafu wanakimbilia kupakia abiria njiani hivyo hukimbizana kupakia wote yaani awe anaenda moshi au moro wao husomba tu. Hiki ndicho kilichotuponza wenzenu nusura tuage dunia....ilikuwa mida ya saa kumi na mbili hivyo abiria wengi tulikuwa tukijiweka vizuri Kwenye siti zetu...kwakweli spidi ilikuwa si mchezo...brake zilimgomea jamaa hivyo akaamua kupiga nyuma lakini isingepiga track ya mchanga nadhani ingekuwa stori zingine hapa maana alikuwa akilielekeza kule upande wa chini ambako nahisi tungepoteza nafsi zetu.
Gari inatakiwa itoke stendi saa kumi na mbili kamili lakini gari imetoka saa kumi na mbili kasoro dakika tano. Jamani traffic wasaidie yaani yaachiane mda hawa watu wanakimbilia abiria huko njiani ni hatari....